Uploaded by kimamboeberhart

Bible Study Guide: Truth & Scripture Examination

advertisement
Tumwamini nani?
Hili ndilo swali linaloulizwa na karibu kila mtu
hapa duniani. Ni nani asemaye ukweli. Kila mahali
•
Tafadhali wasiliana na Kanisa la Waadventista Wasabato
lililo karibu nawe, au tuandikie kwa anwani hii:
Kibidula Bible Studies
P.O. Box 17
Mafinga/Iringa
Tanzania
•
Yachunguzeni
Maandiko!
umejaa udanganyifu, dhuluma, rushwa, uonevu,
vita, n.k. Tunatoka wapi? na tuko wapi? na
tunakwenda wapi? Ni nani anayeweza kutuambia
ukweli?
Kwa bahati nzuri Mungu, aliyeumba vitu
vyote, anayejua kila kitu, na anayeweza kila kitu,
ametuandikia barua ya kututoa mashaka. Mungu
mwenyewe anajibu maswali yetu yote katika
barua hiyo. Barua hiyo inaitwa Biblia.
Biblia siyo mkusanyiko wa mawazo ya
wanadamu. Waandishi wake waliongozwa na
Roho Mtakatifu.
1. Biblia yenyewe inajishuhudiaje?
“Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa
mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa
kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki.”
2 Tim. 3:16.
“Unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya
mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa
Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” 2 Pet. 1:21.
“Maandiko hayawezi kutanguka.” Yn. 10:35.
Biblia inajishuhudia kuwa imevuviwa, iliandikwa
na watu walioongozwa na Roho Mtakatifu, na haiwezi
kutanguka wala kukosolewa.
2. Je, Mungu ana uwezo gani unaomfanya kuwa mkuu
kuliko miungu mingine?
SOMO LA 1
Printed by:
Light Bearers Ministry
USA
Barua Toka Kwa Mungu
“Kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni
Mungu, wala hapana mwingine; Mimi ni Mungu, wala
hapana aliye kama mimi; nitangazaye mwisho tangu
mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka
bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda
mapenzi yangu yote.” Isa. 46:9-10.
3. Ni sehemu zipi za Biblia ambazo Yesu alizitumia katika
mafundisho yake?
“Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza
katika Maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye
mwenyewe.” Lk. 24:27.
Torati ya Musa, yaani vitabu 5 vya kwanza katika
Biblia.
Manabii, yaani, Isaya, Yeremia, Ezekieli, Yoshua,
Samweli, Wafalme, Waamuzi na manabii wadogo 12.
Maandiko ya Agano la Kale yamegawanywa katika
sehemu kuu tatu - Torati, Zaburi, na Manabii.
4. Je, Agano la Kale linazungumza habari za nani?
Yesu akajibu, akawaambia, “Mwayachunguza Maandiko,
kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa
milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia.”
Yn 5:39. “Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno
yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya
kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika
Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi.” Mdo.
24:44. Zingatia: Wakati wa Yesu, Agano Jipya lilikuwa
halijaandikwa. Maandiko yaliyokuwapo ni Agano la Kale
peke yake.
5. Kwa nini mambo yaliyowapata wazee wa zamani
yaliandikwa?
“Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano,
yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya
zamani.” 1 Kor. 10:11.
“Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa
yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja
ya Maandiko tupate kuwa na tumaini.” Rum. 15:4.
Mungu alitegemea kwamba, kwa kujifunza matukio
ya Biblia, tungeweza kuuelewa vizuri zaidi upendo wake
na namna anavyojishughulisha na wanadamu.
6. Je, kujifunza Maandiko kunatusaidiaje?
“Na ya kuwa tangu utoto umeyajua Maandiko
Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate
wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. Kila andiko,
lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa
kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na
kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe
kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.”
2 Tim. 3:15,16,17.
7. Je, Yesu alisema tunaweza kuupata wapi ukweli?
“Uwatakase kwa ile kweli; Neno lako ndiyo kweli.”
Yn. 17:17.
Wanadamu hawaujui ukweli na wengi wao hawajui
kuuelezea. Ndiyo maana kuna taabu na shida nyingi
zisizo na ufumbuzi.
Biblia inasema, “Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo
kweli itawaweka huru.” Yn 8:32.
8. Je, Yesu aliwaambia Masadukayo walikuwa wanapotea
kwa sababu gani?
“Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa
hamyajui Maandiko wala uweza wa Mungu.” Mt. 22:29.
9. Ni kwa nini mtu wa jinsi ya mwili hawezi kuyaelewa
Maandiko?
“Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo
ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala
hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi
ya rohoni.” 1 Kor. 2:14.
10. Je, Yesu alisema ni nani atakayetuongoza na kututia
katika kweli yote?
“Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli,
atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana
hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote
atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha
habari yake.” Yn 16:13.
Biblia inatuambia “Tena ipokeeni chapeo ya
wokovu, na Upanga wa Roho ambao ni Neno la
Mungu” (Efe. 6:17). Hatuwezi kuujua ukweli wa
mipango ya Mungu kwa ajili ya maisha yetu kama Roho
hatatuongoza katika kuisoma Biblia na kututafsiria yale
aliyowavuvia waandishi kutuandikia.
11. Mtume anatuambia nini juu ya Biblia?
“Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu,
mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa
halali neno la kweli.” 2 Tim. 2:15.
Siyo kusoma tu. Tujitahidi! mpaka tuonekane
kuwa tumekubaliwa na Mungu. Inahitajika jitihada ili
tuyaelewe mambo ya kina katika Neno la Mungu.
12. Waberoya walisifiwa kwa jambo gani?
“Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa
Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa
uelekevu wa moyo, wakayachunguza Maandiko kila
siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.”
Mdo. 17:11.
Waliyachunguza Maandiko kila siku, ili waone kama
waliyokuwa wameyasikia yalikuwa sahihi au la. Leo hii
kama kila mtu angechunguza Maandiko aone kama yale
anayofundishwa kanisani ni sahihi au la, kungekuwa na
mabadiliko makubwa katika Ulimwengu wa Kidini. Si
wengi wanaopenda kuiga mfano wa Waberoya. Hebu
tufanye agano na Mungu kwamba tutatumia njia hiyo
hiyo kuutambua ukweli.
C. Baada ya kuangamizwa, Babeli isingekaliwa tena.
“Na Babeli, huo utukufu wa falme, uzuri wa kiburi cha
Wakaldayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora hapo
Mungu alipoiangamiza.” “Haya! juu ya mlima usio na
miti inueni bendera, wapazieni sauti zenu, wapungieni
mkono, kwamba waingie katika malango ya wakuu.”
(Isa. 13:19,2). “Na Babeli utakuwa magofu, makao ya
mbwa-mwitu, ajabu, na mazomeo, pasipo mtu wa kukaa
huko.” Yer. 51:37.
13. Je, Biblia inaulinganisha na nini msaada tunaoupata
kutokana na kujifunza Biblia?
“Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia
yangu.” Zab. 119:105.
14. Tutafanyaje ili tusitende dhambi?
“Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata
Neno lako.” Zab. 119:9.
D. Misri kutokuwa na amri tena kati ya Mataifa.
“Nami nitawarejeza Wamisri walio katika hali ya
kufungwa, nami nitawarudisha hata nchi ya Pathrosi,
hata nchi ya kuzaliwa kwao; na huko watakuwa ufalme
duni. Utakuwa duni kuliko falme zote, wala hautajifunua
tena juu ya Mataifa; nami nitawapunguza, ili wasitawale
tena juu ya Mataifa.” Eze. 29:14,15. “Nami nitaikausha
mito, na kuiuza nchi, na kuitia katika mikono ya watu
wabaya; nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa, na watu
wote walio ndani yake, kwa mkono wa wageni; mimi,
BWANA, nimenena neno hili.” Eze. 30:12,13.
Je, Unabii unathibitishaje kama Biblia imevuviwa?
Biblia inasema
“Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu
sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.
Tazama, mambo ya kwanza yamekuwa, nami nayahubiri
mambo mapya; kabla hayajatokea nawapasheni habari zake.”
Isa. 42:8,9. “Kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana
mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu,
wala hapana aliye kama mimi; nitangazaye mwisho tangu
mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka
bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda
mapenzi yangu yango.” Isa. 46:9,10.
Utabiri wa Biblia juu ya mambo ambayo yangetokea
baadaye, unathibitisha uvuvio wa Biblia, mambo hayo
yanapotokea.
E. Majanga ya kushtua dunia na hofu kadiri
tunavyoelekea siku za mwisho.
“Tena, kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na
nyota; na katika nchi dhiki ya Mataifa wakishangaa
kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake; watu
wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia
mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za
mbinguni zitatikisika.” Lk. 21:25,26.
Angalia mifano ifuatayo
A. Kuinuka na kuanguka kwa falme nne zilizotawala dunia:
Babeli, Umedi na Uajemi, Uyunani na Rumi.
(Danieli 2,7,8.)
B. Koreshi kuwa Mpiganaji ambaye angeiteka Babeli.
“Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi
(mtiwa mafuta) wake, ambaye nimemshika mkono
wake wa kuume, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami
nitalegeza viuno vya wafalme; ili kufungua milango
mbele yake, hata malango hayatafungwa. Nitakwenda
mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza;
nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukatakata mapingo ya chuma; nami nitakupa hazina za gizani,
na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya
kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam,
Mungu wa Israeli.” Isa. 45:1-3.
“Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa
jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya
sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.”
1 Kor. 10:11
F.
Kuporomoka kwa maadili katika siku za mwisho.
“Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho
kutakuwako na nyakati za hatari. Maana watu watakuwa
wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha,
wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii
wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda
wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji,
wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi,
wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda
Mungu; wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana
nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.” 2 Tim. 3:1-5.
G. Unabii juu ya matukio katika maisha ya Yesu.
“Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza
katika Maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye
mwenyewe.” Lk. 24:27. “Kwa maana aliwashinda
Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akionyesha
kwa maneno ya Maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo.”
Mdo. 18:28.
Kwa kuwa wakati huo Agano Jipya lilikuwa
halijaandikwa, ni wazi kuwa Maandiko
yanayozungumziwa hapa ni Agano la Kale.
Utabiri wa Agano la Kale juu ya Masihi ulikuwa
dhahiri na ulitimizwa na Yesu wa Nazareti kiasi
cha kumfanya Yesu mwenyewe na Apolo kuutumia
kuwathibitishia Wayahudi kuwa Yesu alikuwa ndiye
Masihi.
Unabii
Maandiko ya
Agano la
Kale
Kuzaliwa Bethlehemu Mika 5:2
Kuzaliwa na Bikira
Isa. 7:14
Kuwa wa ukoo wa
Yer. 23:15
Daudi
Jaribio la kuuawa na Yer. 31:15
Herode
Kusalitiwa na rafiki
Zab. 41:9
Kutimia katika
Agano Jipya
Kuuzwa kwa vipande
30 vya fedha
Kusulibiwa
Nguo zake kupigiwa
kura
Kutokuvunjwa
mifupa
Kuzikwa katika
kaburi la tajiri
Mwaka, Siku, na Saa
ya kifo chake
Kufufuka siku ya tatu
Zek. 11:12
Mt. 26:14-16
Zek. 12:10
Zab. 22:18
Yn. 19:16-18,37
Mt. 27:35
Zab. 34:2;
Kut. 12:46
Isa. 53:9
Yn. 19:31-36
Dan. 9:26,27;
Kut. 12:6
Hosea 6:2
Mt. 27:45-50
Mt. 2:1
Mt. 1:18-23
Ufu. 22:16
Mt. 2:16-18
Yn. 13:18,19,26
Mt. 27:57-60
Mdo. 10:38-40
Moja kati ya uthibitisho mkuu kwamba Biblia si kitabu cha
kawaida tu kilichoandikwa na watu wema, ni uwezo wake
wa kubadili maisha ya watu. Inaweza kumbadilisha mtu
mwovu kabisa na kumfanya kuwa Mkristo mwaminifu.
Inaweza kumfanya mtu asiye mwaminifu, kutaka kurejesha
alichochukua, au kusahihisha uongo aliosema.
Ni uwezo gani wa ajabu ulio katika kitabu hiki
unaobadilisha kiajabu matamanio na makusudi ya watu? Ni
uwezo wa kufanya miujiza wa Roho wa Mungu anayefanya
kazi kupitia kitabu hiki kutuonyesha Mwana–Kondoo wa
Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.
Je, ungependa kuielewa Biblia vizuri zaidi?
Je, utatenga muda maalum kila juma kwa ajili ya kujifunza
Biblia?
Kwa kutambua kwamba Biblia ni barua ya Mungu
inayokueleza mapenzi yake, je, unakusudia kuishi sawasawa
na neno lake kama asemavyo katika Biblia?
Uamuzi Wangu:
Download