ROHO MTAKATIFU KATIKA KANISA Kitabu cha mafundisho ya ROHO MTAKATIFU ili kupokea nguvu ya kukusaidia katika mafanikio ya kimwili na kiroho. ROHO MTAKATIFU KATIKA KANISA Kimeandikwa na: Rev Anthony Mwakifwamba +255 762 282 777 na +255 718 613 491 P.O. BOX 2256, Dodoma City, Tanzania Na kuchapishwa na Copyright ©2019 Haki zote zimehifadhiwa hauruhusiwi kunakili, kunukulu wala kuchapisha maneno ya kitabu hiki kwa lengo la kuuza kitabu hiki bila idhini ya mwandishi. 1 sehemu ya kwanza Roho Mtakatifu ni nani? Kutokana na biblia katika agano la kale a) Roho Mtakatifu anatumbulishwa kama Roho ya Mungu Mwanzo 1:1-2 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. b) Anatambulishwa kama uweza Hesabu 11:26 Lakini watu wawili walisalia kambini, jina la mmoja aliitwa Eldadi, na jina la wa pili aliitwa Medadi; na roho ile ikawashukia; nao walikuwa miongoni mwao walioandikwa, lakini walikuwa hawakutoka kwenda hemani; nao wakatabiri kambini. Kutoka 35:30-31 Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli, Angalieni, Bwana amemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda; 31 naye amemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na akili, na ujuzi, na kazi ya ustadi kila aina; c) Roho mtakatifu anatambulishwa kama Muumbaji Ayubu 33:4 Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai. Kutokana na biblia agano jipya. 2 a) Anatangazwa rasmi kuwa ni mtenda kazi pamoja na Mungu Mathayo 3:11 Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. Luka 3:16 Yohana alijibu akawaambia wote, Kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto; Marko 1:8 Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu. b) Anatambulishwa kama kiongozi Mathayo 4:1 Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi. Hii maana yake aliongozwa na Roho mpaka mlimani. Luka 2:27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria, c) Anajulikana kama msemaji ndani yetu Mathayo 10:20 3 Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu. d) Anajulikana kama mtoa pepo Mathayo 12:28 Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia. e) Anajulikana kama Mwalimu Luka 12:12 kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa ile ile yawapasayo kuyasema. f) Anajukana kama ni Mungu lakini pia ni Yesu Yohana 4:24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. 2Korintho 3:17 Basi <Bwana> ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. Warumi 8:26 na 34 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. 34Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea. Sasa hapa anajukana kama Yesu kwa sababu ya kutombea kama tulivyotangulia pale kwenye Warumi 8:26. 4 g) Anajulikana kama msaidizi Yohana 14:26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. Rumi 8:26a Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, h) Anajulikana kama Roho wa kweli Yohana 16:13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. 1Yohana 4:6 Sisi twatokana na Mungu. Yeye amjuaye Mungu atusikia; yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Katika hili twamjua Roho wa kweli, na roho ya upotevu i) Anajulikana kama nguvu itendayo kazi ndani yetu Matendo 1:8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. j) Anajuliakana kama Roho wa Hekima Matendo 6:10 lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema naye. 5 k) Anajulikana kama mtoa vipawa Matendo 2:38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 1Korintho 12:8-9 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; 9 mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho Yule mmoja; l) Anajulikana kama shuhuda ndani yetu Warumi 8:16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; 1Korintho 12:3 Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu. Ebrania 10:15a Na Roho Mtakatifu naye amshuhudia; kwa maana, ………… m) Anajulikana kama mwombezi wetu Warumi 8:26c Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. 6 n) Anajulikana kama Roho wa utakaso Warumi 15:16 ili niwe mhudumu wa Kristo Yesu kati ya watu wa Mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi Mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu. 2Thesalonike 2:13 Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli; o) Anajulikana kama mchunguzi(mpelelezi) 1Korintho 2:10-11 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. 11 Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. p) Anajulikana kama mtenda kazi ndani yetu 1Korintho 12:11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye. Roho Mtakatifu ni tofauti na malaika ambao wao wanayomaumbo kamili japokuwa wakati mwingine walijionyesha kama wanadamu wa kawaida, ila Roho Mtakatifu yeye huja kama nguvu wala huwezi kumwona atakapokuja ila utagundua kuwa amekuja kutokana na ile kazi atakayoifanya ndani ya mtu au mahali pale Matendo 2:1-4 inasema Hata 7 ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. 2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. 3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. 4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. Kazi za Roho Mtakatifu ni zipi? Wakati anatambulishwa na Yesu kati ya wanafunzi wale kumi na moja, Yesu anamtaja kama msaidizi atakayewasaidia kufanya yote aliyowaamuru kuyafanya. Yohana 14:16-18 inasema Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumta-mbui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. 18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu. Kufundisha Yohana 14:26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. Kutuongoza na kutupeleka kwenye kweli yote(kwenye neo la Mungu) 8 Yohana 16:13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. Kutuombea Warumi 8:26c Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Kutushuhudia ndani yetu Warumi 8:16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; Kutuunganisha na mbingu 1Yohana 5:8-9 Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja. 9 Kisha wako watatu washuhudiao duniani], Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja. Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe. 9 (Yupo mbinguni lakini yupo tena duniani). Kuponya 1Korintho 12:9a …………..na mwingine karama za kuponya katika Roho Yule mmoja; Kutupa nguvu ya kushindana na kila hali ya kipepo Matendo 1:8a Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; Kutufunulia mafumbo ya mbingu na kutupasha habari ya mambo yajayo 1Korintho 2:10 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Yohana 16:13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. 10 ROHO MTAKATIFU KATIKA KANISA sehemu ya pili Roho Mtakatifu anakaa wapi? Ukimwangalia katika nafasi ya Mungu utamwona yupo mbinguni 1Yohana 5:8 inasema, Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja. Lakini ukimtazama kama msaidizi utamwona yupo duniani 1Yohana 5:9 inasema, 9 Kisha wako watatu washuhudiao duniani], Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja. Pia Roho Mtakatifu anaweza kuishi ndani ya mtu na huyo mtu akajulikana kama hekalu 1Korintho 3:16; Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Na 1Korintho 6:19,20 inasema, Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; 20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu. Kitendo cha Roho Mtakatifu kushuka na kukaa kwa mtu kinajulikana kama kuvuviwa, ama uvuvio wa Roho Mtakatifu. Yohana 20:22 inasema, Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. Kwa kuwa Roho Mtakatifu haonekani katika umbo lake basi anaposhuka anakuwa kama nguvu Fulani yenye utiisho 11 mkubwa, na akisha kaa ndani ya mtu, huyo mtu anajaa nguvu au uwezo wa kufanya jambo Fulani, ndiyo maana tunasema mtu huyu amejaa Roho Mtakatifu Matendo 2:4 inasema Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. Na Mtendo 1:8. Inasema, Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. Kwa mfano kama akitaka watu wajifunze neno la Mungu basi anakuja kama mwalimu, ama akitaka kuponya anakuja kama nguvu ya kuponya, akitaka kutoa unabii basi utakuta anakuja kama nabii, na akishakuja ndani ya mtu lazima huyo mtu awe kama mtu aliyetumwa na mamlaka isiyo ya kwake. Tunawezaje kumpokea Roho Mtakatifu? Ili tuweze kujazwa na Roho Mtakatifu ni lazima tuwe tumemwamini yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yetu ndipo tufuate hatua zinazofuatia : Kufundishwa Neno la Mungu ama kusikia Neno la Mungu. Matendo 2:33-37 33 Basi yeye, akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia. 34 Maana Daudi hakupanda mbinguni; bali yeye mwenyewe anasema, Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti upande wa mkono wangu wa kuume. 35 Hata nitakapowaweka adui zako 12 chini ya miguu yako. 36 Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo. 37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Matendo 10:34,35,39-44 Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo; 35 bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye. 39 Nasi tu mashahidi wa mambo yote aliyoyatenda katika nchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu; ambaye walimwua wakamtundika mtini. 40 Huyo Mungu alimfufua siku ya tatu, akamjalia kudhihirika, 41 si kwa watu wote, bali kwa mashahidi waliokuwa wamekwisha kuchaguliwa na Mungu, ndio sisi, tuliokula na kunywa pamoja naye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu. 42 Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudia ya kuwa huyu ndiye aliyeamriwa na Mungu awe Mhukumu wa walio hai na wafu. 43 Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi. 44 Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno. 13 Kwa kuwekewa mikono Matendo 8:14-16 Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana; 15 ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu; 16 kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu. Matendo 19:2-6 akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. 3 Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. 4 Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu. 5 Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. 6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri. Kusoma Neno la Mungu na kuomba Matendo 4:31 Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri. 14 Kumtukuza, kumshukuru na kumsifu Yesu Kristo kwa muda mrefu. Yohana 7:39 Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa. NB: Roho mtakatifu hatolewi kwa kipimo bali anatolewa kwa imani, Yohana 3:34 inasema, Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo. Pia unapompokea Roho Mtakatifu anakupa na karama zake wala Roho Mtakatifu hatoi karama zake kwa fedha bali kwa kutubia uovu au dhambi na kunyenyekea mbele zake mkimtafuta yeye zaidi kuliko kuvitafuta vitu vyake, Matendo 8:18-22 inasema, Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema, 19 Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemwekea mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu. 20 Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali. 21 Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu.22 Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili kama yamkini, usamehewe fikira hii ya moyo wako. 15 ROHO MTAKATIFU KATIKA KANISA sehemu ya Tatu Dalili za mtu aliyempokea Roho Mtakatifu Kwa kuwa Roho Mtakatifu hujidhihirisha kama nguvu, basi kuna sababu zote kuwa anapokushukia utakuwa na dalili za kushukiwa, tuzitazame hizi dalili: a) Kunena kwa Lugha ambayo kikawaida hujawahi kusema hapo kwanza Matendo 2:4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. Matendo 10:44-46 Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno. 45 Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu.46 Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu.................. b) Unahisi nguvu ndani yako inayokupa ujasiri katika mambo ya Kiroho yanayolingana na maagizo ya Yesu. Matendo 4:31 16 Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri. c) Unapata awezo wa kushinda mambo ya kale kabla ya kumpokea Yesu, ulikuwa mlevi, mvuta sigara nakadhalika, sasa unajikuta ukiwa kama mtu mpya, ambapo tunaita kuzaliwa upya katika roho. Yohana 3:5,8 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? 5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. 6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. 8 Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho. Matendo 1:5 ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache. d) Unapata Uhuru mkubwa nafsini mwako, na uhuru huu hauwezi kuvuka mipaka ya Neno la Mungu. 2Korintho 3:17 Basi <Bwana> ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. 17 Warumi 8:21 kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu. Yohana 8:34-36 Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. 35Wala mtumwa hakai nyumbani siku zote; mwana hukaa siku zote. 36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli. e) Utii wa Neno la Mungu unaongezeka ndani yako, na utii wa uongozi wa Roho Mtakatifu kwa watu wengine waliojazwa na Roho Mtakatifu kama wewe unazidishwa. 1Korintho 14:32-33 Na roho za manabii huwatii manabii. Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu. Dalili zinazoashiria kuwa unaroho zidanganyazo ambazo zinajifanya kuwa ni Roho Mtakatifu. a) Huwezi kujazwa na Roho halafu ukamsema vibaya Yesu Kristo, ama ukakosoa maandiko ya uzima na Neno la Mungu. 18 1Korintho 12:3 Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu. b) Mara baada ya kile unachohisi umejazwa na Roho halafu ukawa kila ukiomba unahamishwa ufahamu wako na kutokujielewa katika maombi, ujue hapo ni roho zingine zilizo ndani yako(kutokujitambua wakati wa maombi). Maana baada ya kumpokea Roho Mtakatifu uombaji wako unabadilishwa na kuomba kwa uhuru, wala fahamu zako hazihamishwi, hivyo unakuwa unaomba kwa roho lakini pia kwa akili. 1Korintho 14:15,33 Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; nitaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia. 33Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu. c) Mtu akiwa hajajazwa na Roho Mtakatifu hawezi kunena kwa lugha, lakini pia kila atakapotoka kunena kwa lugha au katika kuomba huwa hawezi kuwa na tunda la Roho. Bado anakuwa msengenyaji, chuki, hasira, mbinafsi na matendo mengine yanayofanana na hayo au mwingine anakuwa na hofu ndani yake, hawi huru, kwa sababu kile kilichoko ndani yake ni roho zidanganyazo. 19 2Timotheo 1:7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi. Warumi 8:15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. d) Hawezi kujizuia kutenda dhambi, ikiwa atatenda dhambi nafsi yake inakuwa haina hukumu Warumi 6:18 Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wa miili yenu. Kwa kuwa kama mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa. 1Wakorintho 11:31-32 Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa. Ila tuhukumiwapo, twarudiwa na Bwana, isije ikatupasa adhabu pamoja na dunia. e) Mtu anafundishwa, na kukaa nyumbani mwa Bwana lakini bado anaenenda gizani. 20 1Yohana 5:18 Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi. 2Korintho 11:14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Matendo ya giza yanatajwa katika Waefeso 5:9-11 na Wagalatia 5:16-21 kuwa ni: uasherati, uchafu, ufisadi, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, . 21 ROHO MTAKATIFU KATIKA KANISA sehemu ya Nne Usiziamini kila roho Kuna roho zingine ni roho zidanganyazo wala si roho zinazotokana na Mungu, hivyo tunapaswa kuzijaribu ikiwa tunapatwa na mashaka nazo. 1Timotheo 4:1-3 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; 2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; 3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli. Hivyo hatupaswi kuziamini kila roho, tunaweza kuzitambua kwa namna mbalimbali zikiwemo njia za kulinganisha maandiko na hali za hizo roho. 1Yohana 4:3 Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani. Kwanza kabisa lazima kila roho inayotokana na Mungu imkiri Kristo kuwa ni Mungu na alikufa na kufufuka, pia ndiye atakayeuhukumu ulimwengu. 22 Yohana 8:31 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; Kila nabii anapotoa unabii ujue ni Bwana anasema, kama ni Bwana anasema basi ni lazima Neno la Bwana lihusike, kama hakuna neno basi hakuna unabii; na kila nabii asiye tumia maandiko ya neno la uzima ni mwongo. Kumbukumbu la torati 18:20, 22 Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa. 22Atakaponena nabii kwa jina la Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena Bwana; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope. Nabii akinena jambo kwa kulitolea unabii na hilo jambo lisitokee basi atakuwa amenena yeye mwenyewe kwa kujikinai na wala Bwana hajasema, hivyo huyo nabii anaweza kuwa ni nabii wa uongo ama asiyetaka kunena maneno kutoka kwa Bwana, na neno usimwogope linaenda mbali zaidi ya kuogopa, maana nyingine tunaweza kusema usimpokee. Yohana 16:13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. 23 Mtu atakayesema kama Mungu, yaani ikawa kama yeye ndiye anayesema basi huyo ndiye nabii wa uongo, maana kila nabii wa Mungu husema kama kinywa cha Mungu, anasema kama mtu aliyetumwa kusema, hivyo kwake yeye kusema Bwana kasema ni kawaida yake, na atakaposema huwa hatafuti hekima nyingine zaidi ya ile aliyotumwa, na pia halazimishi ujumbe wake upokelewe, maana kazi yake ni kusema tu wala si kutaka atakayoyasema yafuatwe. Mathayo 15:4 Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe. Mtu mwenye Roho Mtakatifu anafuata kanuni zote za Yesu alizozisema, ikiwa mtu huyo atasema kwa lugha ya malaika au lugha ya wanadamu na akawa hana heshima kwa watu waliomzidi umri ama kuwadharau basi mtu huyo hana Roho Mtakatifu badala yake anaroho zidanganyazo. 1Korintho 13:8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika. Kanuni kuu kuliko zote ambazo Yesu alizitaka tuzifuate ni upendo, kama mtu akiwa anafanya ishara za Roho Mtakatifu halafu akawa hana upendo basi mtu huyo ni dhahili kabisa kuwa hana Roho Mtakatifu bali anaroho zidanganyazo. 24 Wafilipi 2:3 Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kutoka 35:29 Wana wa Israeli wakaleta sadaka za kumpa Bwana kwa moyo wa kupenda; wote, waume kwa wake, ambao mioyo yao iliwafanya kuwa wapenda kuleta kwa hiyo kazi, ambayo Bwana aliamuru ifanywe kwa mkono wa Musa. Roho Mtakatifu akishuka hutupeleka kwenye mapenzi ya Mungu wala sisi hatujipeleki wenyewe, hivyo ndani yetu tunaanza kupata shauku ya kutimiza yale anayoyataka wala si kwa lazima ya mtu fulani, bali tunajikuta wenyewe tunavutwa kufanya sawasawa na apendavyo Mungu. Isaya 42:8 Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu. Galatia 5:25-26 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. 26 Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana. Wakolosai 1:29 Nami najitaabisha kwa neno lilo hilo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu. Wafilipi 2:13 25 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema. 1Korintho 12:11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye. Roho Mtakatifu anapokuwa ndani ya mtu yule mtu hawezi kujitukuza wala kujiona na uwezo wa kutenda kazi zaidi ya wengine. Zaburi 33:11 Shauri la Bwana lasimama milele, Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi. Roho mtakatifu hajipingi mwenyewe, anapoamua jambo lifanyike katika yeye lazima lifanyike kama alivyoamua wala hawezi kugeuka tena akasema nilikosea au hapana hili halipo sawa hivyo fanya kivingine, bali yeye akisema moja leo na kesho akija atasema ileile moja ya jana. 2Korintho 13:1 Hii ndiyo mara ya tatu ya mimi kuja kwenu. Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa. Kila neno la Roho Mtakatifu ni muhimu kulipima kwa kusubiri lithibitike kwa watu zaidi ya mmoja, au kwa kuomba ishara ya kuhakikisha lile neno. 26 Wakolosai 3:15 Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. Endapo utataka kufanya maamuzi fulani, angalia kiwango chako cha imani halafu angalia amani iliyoko ndani yako, usiangalie njia au mpenyo wa kufanya ila angalia amani iliyo ndani yako. Kwa sababu Roho Mtakatifu anakaa ndani yako basi yeye atakuvuta na kutia msukumo mkubwa ndani yako, pengine hata kwa machozi, na unapoamua kutokana na huo msukumo ndani yako kuna mahali pa kuanzia kama utaanza na hatua kuelekea kufanya ama kutoa maamuzi(starting point). 27 ROHO MTAKATIFU KATIKA KANISA Sehemu ya tano Roho mtakatifu anapokuwa ndani yako unakuwaje? Utaichukia dhambi 1Yohana 3:6 na 9 Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua. 9Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. 1Yohana 5:18 Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi. Kwako dhambi inakuwa ni kama jambo linalokereketa, na lenye kukupoteza, hivyo unajikuta unaichukia dhambi sana, wala huoni amani katika mazingira ya dhambi. Unajawa na amani ya Kristo ndani yako. 1Korintho 14:33 Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu. 28 Ndani yako hauoni jambo la kukukwaza, kila jambo kwako ni kama maji yanayopita taratibu na kupotea kabisa, huna shaka na maudhi yoyote kutoka kwa mtu yoyote bali ni amani tu moyoni, hii inasababisha uchukuliane na watu wote ilivyo sawa sawa. Ila sasa hapa wivu wa Bwana unajaa ndani yako, mambo ambayo yataweza kukukwaza ni yale yanayomtukanisha Kristo au Roho Mtakatifu. Utapenda kusoma neno la Mungu mara kwa mara. Luka 8:21 Akawajibu akasema, Mama yangu na ndugu zangu ndio hao walisikiao neno la Mungu na kulifanya. Ebrania 4:12 Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. 1Petro 1:23 Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele. Utajikuta unafuraha zaidi unaposoma maandiko yenye uzima, na kusikia mafundisho ya neno la Mungu kuliko kitu chochote kile katika maisha yako. 29 Utapenda kuomba kila wakati. Yuda 1:20 Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu, Thesalonike 5:17 ombeni bila kukoma; Mathayo 14:23 Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake. Matendo 6:4 na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile Neno. Yakobo 5:16 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. Utamshuhudia Kristo kwa watu wengine. Marko 16:15 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. 30 Luka 9:6 Wakaenda, wakazunguka katika vijiji, wakihubiri injili, na kupoza watu kila mahali. Warumi 1:16 Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia. Warumi 15:20 kadhalika nikijitahidi kuihubiri Injili, nisihubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine; 1Korintho 9:18 Basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa Injili bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili. Shauku yako ni kuona watu wote wanamjua Kristo, hivyo utajikuta unatabia ya kumshuhudia Kristo kwa mtu yoyote mahali popote. 31 Utajawa na utendaji wa tunda la Roho Wagalatia 5:22-25 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.24 Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.25 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Ndani kunavutwa zaidi katika kuyatenda na kuyaona mambo mema, na huu ndio uchaji hasa. Utapenda kumwadhimisha Mungu maishani mwako. Warumi 15:5-6 Na Mungu mwenye saburi na faraja awajalie kunia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa mfano wa Kristo Yesu; 6 ili kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Ukikaa utajikuta unanena kwa lugha, au unamtukuza Mungu, na maneno ya Mungu hayaishi kinywani mwako hata ukiwa peke yako kwa mfano: asante Yesu, Mungu yupo, Haleluya n.k. 32 Unajawa na hofu ya Mungu. 2Korintho 5:11 Basi tukiijua hofu ya Bwana, twawavuta wanadamu; lakini tumedhihirishwa mbele za Mungu. Nami natumaini ya kuwa tumedhihirishwa katika dhamiri zenu pia. 1Petro 3:2, na 15 wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu. 15 Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. Ndani yako utajikuta hufanyi jambo kama zamani bila kujali, hapana ndani yako utaona maamuzi yako yanajali sana kama unamkosea Mungu au la, kila utakachofanya utajihoji kwanza kama ni halali kwako kufanya hivyo au la. Unakua katika imani. Matendo 3:16 Na kwa imani katika jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua; na imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote. Warumi 15:13 Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu. 33 Kila unachokifanya utakifanya kwa imani inayotokana na neno la Mungu, hivyo kila wakati unajikuta unakua zaidi kiimani na kujikuta roho yako inafanikiwa zaidi. Unajaa nguvu za kiroho. Warumi 15:18-19 Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yangu, Mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo,19 kwa nguvu za ishara na maajabu, katika nguvu za Roho Mtakatifu; hata ikawa tangu Yerusalemu, na kando kando yake, mpaka Iliriko nimekwisha kuihubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu; Kiwango chako cha nguvu za Mungu kinakua na kuongezeka, utiisho wa kiungu unajaa ndani yako, maana yeye atendaye kazi ndani yako ndiye mwenmye sehemu ya nguvu iliyopo ndani mwako. Na hizi nguvu ndizo zinazoitwa zawadi za Roho Mtakatifu au Karama za Roho Mtakatifu. 34 ROHO MTAKATIFU KATIKA KANISA Sehemu ya sita Karama za Roho Mtakatifu. Hizi ni karama ambazo zinajulikana pia kama karama za rohoni. 1Korintho 14:1. Juu ya karama za rohoni, tunamafundisho kadha wa kadha tunayoweza kuyaona kupitia neno la Mungu Biblia, lakini tunajifunza kutoka katika sehemu tatu tu katika Biblia. Warumi 12 inazungumzia juu ya karama hizi, 1Wakorintho sura ya 12 na 14 pia zinazungumzia juu ya hizi karama, na tena katika Waefeso 4:7 inazungumzia hizi karama za Roho Mtakatifu ama karama za Rohoni. Mungu kupitia watumishi wake aliowapa neema ya kuandika kwa ajili yetu anakusudio la kututaka tujue kuwa kila utendaji wa kazi katika kanisa leo tunahitaji karama za Roho Mtakatifu ili tufanikiwe kutimiza kila makusudi yake aliyoyakusudia katika maisha yetu. Tunapoanza kuziangalia hizi karama kwanza tujue karama ni kitu gani ili tutakapoanzakuziangalia utendaji wake tuwe tumajua maana na ni kitu gani. Karama ni nini? Ni kitu kinachotolewa na Mungu kupitia roho Mtakatifu ili kuuhudumia mwili wa Kristo ambao ndio kanisa. 1Korintho 12:7 na 27, 35 Hizi karama zinatolewa kwa kufaidiana, (iwe mfaida wengine). 1Korintho 12:7 na 27, 7Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. 17-18 Kama mwili wote ukiwa jicho, ku wapi kusikia? Kama wote ni sikio ku wapi kunusa? Bali Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka. Kwa nini ziitwe karama? Lugha ya hili neno inatafsiriwa kutoka kwenye lugha ya kigiriki ambayo ni "karismaton" ambayo inamaana ya zawadi kwa "kiswahili" na kimombo ni "gift". Hivyo kwa wagiriki walipokuwa wakitoa zawadi waliziweka katika mafungu mawili, fungu la kwanza ni zawadi anazopewa mtu kutokana na kazi aliyoifanya na zawadi anazopewa mtu asizostahili ambazo hasa ndizo zinazoitwa "Karismaton" kwa kigiriki. Mtu anapokea zawadi hizi akiwa tayari amemkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake; hivyo huja baada ya Yesu kuingia ndani ya mtu. Na mara baada ya kupokea karama hizi, hazimwondoi Yesu katika maisha ya mtu huyo, Yesu anashika namba moja ndipo karama zifuatie, hivyo mtu mwenye hizi karama anamuhesabu Yesu ndiye mwanzilishi wa karama hizi, na ndiye kichwa cha kanisa na yeye huyo mtu anajihesabu ni mwili wa Kristo ama kanisa(hekalu). Kwa hiyo bila Yesu hakuna karama za Roho, na bila karama za Roho hakuna uwezo wa kutenda kazi za Yesu. 36 Matendo 1:4 Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu; Yesu anawaambia wale tenashara wasitoke mpaka waipokee ile ahadi ya kuwaletea msaidizi mwingine ambaye ni Roho Mtakatifu, alijua kama watatoka na kwenda kufanya kazi hawataweza kabisa kwa ufahamu wao wa kibinadamu, hivyo walihitaji zaidi ufahamu wa kiungu ndani yao ili waweze kufanya yote aliyowaamuru, na njia pekee ya kufanya kwa uwezo wa kiungu ni kungoja wajazwe na Roho Mtakatifu; utaona baada ya kujazwa na Roho Mtakatifu ndipo walipoweza kupata ujasiri wa kuhubiri injili, na kufanya zile kazi ambazo Yesu alizitenda. Karama za rohoni zinamfanya muumini kutenda kazi alizozitenda Yesu na zaidi ya zile alizozitenda. Yohana 14:12 Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. Warumi 12:5-8 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa 37 moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha. Tuziangalie hizi karama ni zipi? 1Korintho 12:4-11 1. Neno la hekima Hizi ni karama zinazoongozwa na maneno au maamuzi sahihi, kwa wakati sahihi, na kwa mahali sahihi, lakini sawasawa na maandiko yanavyosema. 1Korintho 2:12,13 inasema, Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. Mtu hawezi kufanya au kunena maneno yanayotoka kwa Mungu isipokuwa kwa kupewa na Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu, na hakuna hekima inayopita hekima zote kama si hekima ya Kiungu inayotolewa na Roho Mtakatifu. Kwa kigiriki neno hekima ni "sofia" Hekima ni mtu kusema, kufanya na kutenda jambo sahihi kwa watu sahihi, mahali sahihi, kwa muda sahihi na kwa lugha sahihi. 38 2. Karama ya maarifa (gnosis) Hii ni karama inayohusika katika namna ya kutatua changamoto fulani, kuongoza watu fulani ama kubuni jambo litakalokuwa ni msaada kwa kanisa, lakini kila ubunifu wake unaongozwa na neno la Mungu kutoka katika maandiko matakatifu. 1Korintho 12:8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; 1Korintho 13:2a Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, ………. Hivyo mtu mwenye hii karama hakaukiwi maarifa kinywani mwake, na hata katika kila atakachokifanya kitakuwa katika maarifa ya Mungu. 3. Karama ya Imani Kila mtu anapaswa kuwa na imani sawa na neno la Mungu katika Waebrania 11:6 linsema, Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. Acha imani hii ya ujumla wa kila mtu awe nayo lakini mbali na hii kuna ile ambayo anapewa mtu kama karama ndani yake ili kuwa msaada kwa kanisa,na hii imani inakuwa ni ile iliyozidi kawaida ya mwanadamu. 39 Imani hii inatumika kupitisha mambo ambayo yanaonekana hayapiti katika uwezo wa kawaida, kutia moyo mahali ambapo kunakuvunjika moyo, na kuvusha watu toka katika kila hali ya mateso au changamoto fulani. Karama hii inaweza kulifanya kanisa kuwa na matumaini ya ushindi wakati wote, hivyo ndani ya kanisa ni lazima kuomba sana kuwa na aina hii ya karama. 1Korintho 12:1-9a Basi, ndugu zangu, kwa habari ya karama za roho, sitaki mkose kufahamu.2 Mwajua ya kuwa mlipokuwa watu wa Mataifa, mlichukuliwa kufuata sanamu zisizonena, kama mlivyoongozwa. 3 Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu. 4 Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. 5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. 6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. 7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. 8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; 9mwingine imani katika Roho yeye yule; 4. Karama ya uponyaji Hii karama ni ya muhimu sana katika kulitangaza jina la Yesu Kristo, na mahali penye aina hii ya karama watu wengi wanakimbilia, kwasababu watu wengi wanatamani kuishi wakiwa na afya bora pasipo magonjwa. Lakini magonjwa ni sehemu ya mateso kwa mwanadamu, hata hivyo si lazima 40 mpaka hii karama tu ndipo watu waponywe magonjwa, hapana, isipokuwa uponyaji ni wa namna apendavyo Mungu. 1Korintho 12:1-2,7-9 Basi, ndugu zangu, kwa habari ya karama za roho, sitaki mkose kufahamu. 2 Mwajua ya kuwa mlipokuwa watu wa Mataifa, mlichukuliwa kufuata sanamu zisizonena, kama mlivyoongozwa. 7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. 8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; 9mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; Tunasema hii ni karama ya muhimu kwa sababu karama ni zawadi pasipo kustahili, hivyo ni kitu kinachoishi ndani ya mtu, sasa uponyaji ukiwa unaishi ndani ya mtu moja kwa moja mtu huyo atakuwa mara kwa mara amejikita zaidi kwenye maswala ya uponyaji, mfano: kujaribu kumgusa mtoto kichwa na kujua jotoridi la mwili na kumpatia dawa ya maumivu kisha mtoto kupona maumivu ya kichwa haimaanishi wewe ni daktari(mganga), bali utakapoonana na daktari atakueleza maelezo yanayoweza kukusaidia zaidi katika hilo jambo, yeye atatumia vipimo na kugundua aina ya ugonjwa na kumpatia dawa inayostahili wala siyo tu hiyo ya kutuliza maumivu. Hii niifananishe na hiyo karama ya uponyaji, haihusishi kutuliza tu bali inasababisha tiba kabisa kwa mgonjwa au mkwa mwenye changamoto, uponyaji huu unaweza kuwa ni wa nafsi, au mwili ama roho. Sasa haijalishi kuna mtumishi ameweka mikono kwa mgonjwa mara Yule mgonjwa akapona ndio ikawa ni kipimo cha kuwa na karama 41 ya uponyaji la hasha, tuangalie habari za Anania na Sauli ambaye baadaye aliitwa Paulo…. Matendo 9:12-15 naye amemwona mtu, jina lake Anania, akiingia, na kumwekea mikono juu yake, apate kuona tena. Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemu; hata hapa ana amri itokayo kwa wakuu wa makuhani awafunge wote wakuitiao Jina lako. Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli. Hili fungu linaonesha namna Mungu anavyoweza kumtumia mtu kuponya hata kama hiyo siyo karama yake, yeye anaponya mara moja kwa ajili ya kusudi la Mungu. Ukilinganisha na mtu mwenye karama ya kuponya ambayo hata nguo zake zinatembea na upako huo wa kuponya.Amewekewa zawadi ndani yake na kila wakati hata kama yeye hajui juu ya mgonjwa katika kundi lakini anapoonekana tu mgonjwa anaweza kupona, tazama hili fungu katika Biblia: Matendo 19.12 hata wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizotoka mwilini mwake, magonjwa yao yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka. Paulo anaponya kwa uweza wa Mungu wala si kwa uweza wake wala si kwa nguvu zake ila nguvu hiyo ipo ndani 42 yake, hivyo yeye anatumika kama chombo cha kuhifadhia uponyaji tu wala uponyaji sio wake. Matendo 9.34 Petro akamwambia, Ainea, Yesu Kristo akuponya; ondoka, ujitandikie. Mara akaondoka. Hapa ni kwa nini aseme Yesu akuponya ikiwa yeye Petro ndiye yupo pale na Yesu haonekani pale? Jibu rahisi ni kwamba Petro anaishi ndani yake Yesu na Yesu anaishi ndani yake Petro, hata kile akifanyacho Petro ni matokeo ya kile alichokifanya Yesu ndani yake. 5. Karama ya miujiza Kwani umewahi kuona au kusikia wahubiri wanapokuja kwenu kila siku Mungu anajifunua kwa namna tofauti na kuwatumia wahubiri kuponya na kufungua papo hapo? Miujiza ni kitu cha ajabu kinachotokea bila kutegemea papo hapo, hapa hausubiri kesho ni jambo linalofanyika ana kwa ana. 1Korintho 12:7-10a 7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. 8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; 9mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;10na mwingine matendo ya miujiza; 43 Huu ni uweza wa Mungu ndani ya mtu ili Mungu ajifunue kuwa yupo mahali pale na watu wapate kumwamini Yesu. Matendo 9.33-35 Akamwona mtu mmoja huko, jina lake Ainea, mtu huyo amelala kitandani miaka minane; maana alikuwa amepooza. Petro akamwambia, Ainea, Yesu Kristo akuponya; ondoka, ujitandikie. Mara akaondoka. Na watu wote waliokaa Lida na Sharoni wakamwona, wakamgeukia Bwana. Tunaona mara baada ya Ainea kupokea muujiza watu wote wanamgeukia Bwana, hivyo kusudi kubwa la muujiza ni ili watu wamtambue Yesu Kristo anayehubiriwa mahali pale. 6. Karama za unabii Hizi ni aina za karama ambazo Roho Mtakatifu anamtumia mtu katika maeneo matatu, moyo, macho na kinywa. Mtu aliyepewa hizi karama anajulikana kama nabii, hapo mwanzo nabii aliitwa mwonaji 1Samweli 9:9 (Hapo zamani katika Israeli, mtu alipokwenda kuuliza neno kwa Mungu, husema hivi, Haya! Twende kwa mwonaji; maana mtu aitwaye sasa Nabii hapo zamani aliitwa Mwonaji.) Mwonaji ni macho ya Mungu, na ni kinywa cha Mungu pia, hivyo nabii ni kinywa cha Mungu na ni macho ya Mungu. Huyu mtu (nabii) huzungumza na Mungu na kusema na watu wa Mungu juu ya yale aliyozungumza naye, naye huwa kama mtu aliyetumwa, wala hazungumzi kwa mamlaka kanakwamba 44 yanatoka kwake, isipokuwa anazungumza kama mtu aliyetumiwa na Mungu kuzungumza, kwa mfano: “Bwana asema” ndiyo hasa anavyoanza au kumaliza ujumbe wake. Na nabii hutoa unabii ili kulijenga kanisa wala si vinginevyo, pia nabii ni mtu aliyechini ya mchungaji maana naye inampasa kuchungwa chini ya mchungaji tutamuelezea nabii zaidi katika zile huduma tano za kanisa. Basi karama hii ya unabii inatumiwa na Mungu kuzungumza na kanisa ndani ya kanisa kwa lengo la kulijenga kanisa. Mtu mwenye hii karama anaona na kusikia mambo au maelekezo ya Mungu kwa kanisa. 7. Karama za kupambanua roho Ndani ya kanisa kunakuwa na muingiliano mwingi sana wa kiroho, na ukizingatia haya mambo ya rohoni yanahitaji muongozo sahihi katika kuyafanya na kukubaliana nayo, shetani ni roho na Mungu ni roho isipokuwa tofauti yao ni kwamba Mungu ndiye chanzo cha mambo yote tunayoyafahamu hapa ulimwenguni mfano elimu, pesa, madini, ndoa, uzao, sheria na siasa, lakini shetani ni mfuatiliaji tu wa mambo yote tunayoyajua, katika kufuatilia, yeye kwa kuwa ana uadui na wana wa Mungu hivyo anatumia hila nyingi kuhakikisha wana wa Mungu wanapotea njia sahihi ya kumwabudu Mungu na kumfuata Mungu, hivyo atatumia ulimwengu wa roho kupotosha, na ndiyo maana sasa tunahitaji sana hii karama ya kupambanua roho ili tuzifahamu hila za adui ndani ya kanisa. Isaya 21:2 45 Nimeonyeshwa maono magumu; atendaye hila anatenda hila, mharibu anaharibu. Panda juu, Ee Elamu; husuru, Ee Umedi; mimi ninakomesha maombolezo yake yote. Hii karama inasaidia kumjua roho yupi atendaye kazi ndani ya kanisa, ikiwa kunauvamizi wowote wa kipepo ndani ya kanisa tukiwa nah ii karama tutautambua haraka kabla haujaleta madhara kwa kanisa. 8. Karama za aina za lugha Hizi ni aina za karama ambazo zinahusisha ulimi na matamko. Karama hizi zipo katika mafungu mawili: i) lugha za wanadamu, ii) lugha za malaika; katika hizi aina za karama mtu anayepewa hizi karama huwa anajikuta akizungumza aina mbalimbali za lugha za wanadamu au lugha za malaika pasipo kwenda chuo wala shule ya lugha. Lugha za wanadamu ni lugha zinazozungumzwa na makabila au mataifa mbalimbali, mfano Kiingereza, Kiswahili, au Kichina, ama lugha zingine zinazojulikana na watu wa hiyo lugha. Matendo 2:2-9 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. 3Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. 4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. 5 Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu. 6 Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe. 7 Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? 8 Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa 46 nayo? 9 Warparthi na Wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapadokia, Ponto na Asia, Bila shaka umeona hizi lugha walizokuwa wakinena, lakini hakikuwashangaza kusikia wakikinena hizo lugha bali kilichowashangaza ni pale waliposikia wakinena lugha za watu wa mataifa mbalimbali ikiwa wao ni taifa jingine ambapo hawakuwahi kuzungumza hapo kabla. Sasa mtu anaponena kwa hii lugha ya wanadamu basi aweze kuwepo na mfasiri ili kutafsiri yale yanayosemwa hapo, ili watu wasioijua hiyo lugha waweze kuelewa kile ambacho Roho Mtakatifu anasema; hapo ndipo tunapoweza kusema ni bora kukaa kimya kuliko kunena kwa hii lugha ikiwa hakuna anayeweza kutoa tafsiri ya hiyo lugha, kwa mfano katika fungu la hapo juu la Matendo ya Mitume 2:2-9 watu waliokuwepo nje ya lile jengo waliposikia walishangaa kusikiwa wakinena lugha za mataifa yao, hivyo ni vizuri kama wanaosikiliza wakaelewa maana ya yale unayonena la sivyo hakuna sababu ya kunena kwa lugha za wanadamu mbele yao. 1Korintho 14:27-28 Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri.Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu. Lakini mtu anaponena kwa lugha za malaika ndipo tunapoesama mtu huyu anazungumza na Mungu na lengo kubwa la Roho Mtakatifu ni kumjenga huyo mtu anayenena hii lugha wala hata yeye hajui kile anachokizungumza wakati huo bali anaijenga nafsi yake. 1Korintho14:2-5 Maana yeye 47 anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake. 3 Bali yeye ahutubuye, asema na watu maneno ya kuwajenga, na kuwafariji, na kuwatia moyo. 4 Yeye anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake; bali ahutubuye hulijenga kanisa. 5 Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kuhutubu, maana yeye ahutubuye ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri, ili kusudi kanisa lipate kujengwa. Kunena kwa lugha hii ni vizuri sana wala hapana masharti unapokuwa ukinena kwa hii lugha ili mradi uwe kweli katika Roho, japo kama utahutubu (utafundisha)ni vizuri zaidi ya kunena ili mtu asiyefahamu mambo ya Roho Mtakatifu aweze kuyafahamu yale unayosema. NB: 14 Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda. 15 Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; mtaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia. Mtu anayenena kwa lugha anaweza kukumbuka, anaweza kujitambua mahali alipo, anaweza kujijua na kijitawala wala hawezi kupoteza ufahamu wake kwa sababu ya kuzama katika maombi, isipokuwa atazama katika maombi bila kuyahisi mambo ya mwilini mfano uchovu, njaa, au mambo ya mwilini yanayoshindana na roho yake. Hivyo mtu akinena halafu hawezi kujitawala huyo atakuwa amevamiwa na pepo wala siyo Roho Mtakatifu. 9. Karama za tafsiri za lugha 48 Hizi ni karama zinazotegemea kusikia na kuzungumza kile unachokisikia kwa kutoa ufafanuzi zaidi kutoka kwenye maneno uliyoyasikia kwa mtu anayenena kwa lugha ngeni, 1Korintho 14:12-15 Vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa. 13 Kwa sababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kufasiri. 1 Wakorintho 12 : 1-31 Utendaji wa Karama za rohoni hautufikishi kukutana na Mungu na kutufikisha Mbinguni ni kwa ajili ya kulijenga kanisa pekee(mioyo na nafsi au kusanyiko la watu wa mahali pamoja). 1Korintho 13:2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Hili fungu linazungumzia utendaji wa karama hizi; karama zote haziwezi kumfanya mtu akawa kitu mbele za Mungu, isipokuwa akiwa na hizi karama basi awe na upendo. Upendo wa kweli unaomfanya Mungu kuwa wa kwanza na kuwafanya watu kuwa wa pili halafu wewe mwenyewe kuwa wa mwisho katika kujali na kuhudumu. 49 Sifa za upendo wa kweli 1Korintho 13:4-8 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; 5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; 6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; 7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. 8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika. Katika hizi karama za rohoni tunaweza kuzipata kwa kuzihitaji na kumwambia Mungu atoaye karama atujalie na sisi tuweze kuwa nazo, lakini hutuwi nazo ili zitusaidie katika mambo yetu binafsi bali ili kuujenga mwili wa Kristo (Kanisa kama watu wanaomtafuta Kristo katika kutaniko moja). Bila shaka ulipomaliza kukisoma hiki kitabu kuna mambo mazuri umeyafurahia sana ambayo utayatendea kazi, naomba nikupe angalizo, usiache kukusanyika kama ilivyo desturi, ili kama yamkini utaendelea kujazwa na Roho Mtakatifu kila siku na kila wakati, maana ujazo wa Roho Mtakatifu unaendelea kila siku , kila muda, na kila mahali, ambapo wewe unatakiwa uwe umejazwa na uzidi kujazwa, kila unapojazwa na Roho Mtakatifu unapelekwa kwenye kiwango kingine cha kiroho. Ukitaka ufanikiwe sana katika kila kitu lazima uwe umejazwa na Roho Mtakatifu kila wakati, maana yeye nndiye 50 anayetupeleka katika kweli yote. Mtu aliyejazwa na Roho Mtakatifu anauwezo wa kushinda dhambi hata kama ni dhambi ya namna gani lazima Roho Mtakatifu atamkumbusha sawa sawa na neno lake. Mungu akubariki sana kwa kusoma kitabu hiki, na ni imani yangu kuwa umefunguliwa sana na kubarikiwa sana na jumbe za kitabu hiki, Amina Utukufu. +255 762 282777, na +255 718 613491 revmwakifwamba@gmail.com 51 MWISHO ROHO MTAKATIFU KATIKA KANISA Kimeandikwa na: Rev Anthony Mwakifwamba +255 762 282 777 na +255 718 613 491 P.O. BOX 2256, Dodoma City, Tanzania Na kuchapishwa na Copyright ©2019 Haki zote zimehifadhiwa hauruhusiwi kunakili, kunukulu wala kuchapisha maneno ya kitabu hiki kwa lengo la kuuza kitabu hiki bila idhini ya mwandishi. 52