Uploaded by Rev Mwakifwamba

PROFILE YA KANISA.docx

advertisement
ADONAI
MISSION CHAPEL
PROFILE
KUHUSU KANISA
ADONAI MISSION CHAPEL
Profile ya ADONAI MISSION CHAPEL ni melezo mafupi ya mtazamo na mwelekeo wetu
kama kanisa kwa kipindi cha miaka mitano mpaka miaka 10 ijayo.
KUHUSU
KANISA
ADONAI MISSION CHAPEL
Maana ya Adonai
Adonai ni neno la kigiriki ambalo limetumika kwenye Biblia ili
kuelezea sifa moja wapo ya Mungu.
CONTENTS:
 KUHUSU KANISA
 MIRADI
 MISIMAMO YETU
 MAONO YETU
 HATUA TULIZOCHUKUA
Sifa yake kuu inayojulikana kuwa hakuna kama yeye yaani “Mungu
mwenye enzi yote” Ama tuseme Bwana wa mabwana.
Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA;
nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu
Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.
Kutoka 6:2-3.
Makao makuu ya kanisa
ADONAI MISSION CHAPEL Lina ofisi mama/Ofisi Kuu yake Jijini
Dodoma.
Nembo ya kanisa ADONAI MISSION CHAPEL
o
Rangi nyekundu ni alama ya Ushindi kupitia Damu ya Yesu
o
Rangi ya Bluu ni alama ya Ubatizo wa maji mengi
o
Rangi Nyeupe ni alama ya Utakatifu
o
Ramani ya Dunia inaashiria injili kuhubiriwa ulimwenguni
kote
o
Msalaba unaashiria ukombozi tulioupata msalabani
o
Biblia inaashiria Neno la Mungu ni Hai.
1
MBEBA MAONO YA KANISA
ADONAI MISSION CHAPEL
Reverent Apostle Anthony J Mwakifwamba
Mbeba maono.
Ni mtu yeyote aliyepatiwa maono na Mungu ili ayatumize katika utume alioitiwa na Mungu katika jamii.
Mungu alipomsemesha Mtume na Mchungaji wa kanisa letu la ADONAI MISSION CHAPEL, alimpa
watu watatokao msaidia kutimiza maono ya Mungu kwa jamii hii.
Siku ya kujiliwa ilipotimia Mungu aliamsha kazi alizoziweka ndani ya Mtume wake Mchungaji Anthony
Mwakifwamba, na kati ya kazi zenyewe mojawapo ni kuufikia umma wa jamii ya ulimwenguni katika
kuhubiri injili ya kweli ya Kristo Yesu.
Wito ulipoanzia
Wito huu ulianza mwaka 2014 katika mkoa wa Dodoma.
Haikuwa rahisi kuanza moja kwa moja. Katika safari ya kutimiza mambo makubwa ya Mungu yaliyo
ndani ya mtu lazima kwanza huyo mtu apewe darasa hadi darasa, na kila darasa mwisho wake kuna
jaribio au mtihani anaotakiwa kuufanya na akifaulu atavuka kwenda darasa lingine.
Baadhi ya madarasa aliyopitia:
1.
2.
3.
4.
Alipitia nyakati za kukataliwa
Alipitia nyakati za kukatishwa tamaa
Alipitia nyakati za dhiki na shida za kifedha
Alipitia nyakati za kubarikiwa na kupoteza Baraka zote kwa kipindi kifupi
Namna pekee iliyomfanya avuke ni kupitia watumishi wengine wa ndani nan je ya nchi, maana kila
alipokuwa akipitia hali hizo zote alikuwa akitafuta Zaidi suluhisho lake na kujikuta anapata ufumbuzi
kupitia watumishi wanaoandika vitabu na wanaotoa semina au mahubiri yao kupitia vyombo mbalimbali
vya kimtandao.
Safari hii haijawahi kuwa rahisi na hata sasa bado haijawa rahisi, bali inahitaji moyo na kujituma sana ili
kufanikisha maono ya Mungu, hata kama Mungu ndiye aliyekutuma lakini utahitaji kukaza mkanda
vizuri kabisa ili utimize yale uliyoandikiwa uyatimize.
Yeremia 48:10
Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya Bwana kwa ulegevu;…………………
2
Ilimgharimu kusoma Zaidi juu ya Elimu ya Mungu(theology) tunu aliyoipata ilikuwa ni katika chuo kikuu
cha AMO (African Ministries Outreach) Cha Africa Kusini chenye makao makuu yake Marekani.
Aliweza kupata Shahada ya kwanza hapo mwaka 2021.
3
MIRADI
Ili kutimiza maono haya yote inahitaji kufanya mambo kadha wa kadha yatakayo sababisha mipango
yote iende, hususani katika hali hii ya kiulimwengu, ambapo pesa ndiyo inayoleta maamuzi katika
kufanikiwa ama kufeli.
Mipango hii ndiyo tunayoiita miradi.
Tunamiradi kadhaa tunayofanya na tuanayotarajia kuifanya hapo baadaye, kuzalisha maendeleo
chanya kwa watenda kazi na kwa kanisa lote kwa ujumla.
Orodha ya miradi tuliyoanza kuifanya
1. Kuwa na eneo la kanisa mama
2. Kuandika vitabu vya kijamii na kiroho
3. Kufanya maombezi kwa watu wenye shida na wenye mizigo
Baadhi ya vitabu vyetu ni kama vile:






Jinsi ya Kuushinda Ufalme wa Adui yako
Kijana Aishije
Maombi yenye matokeo
Kushinda wakati wa Mateso na Kukataliwa
Ninawezaje Kufanikiwa Kiroho na Kimwli
Roho ya Ushawishi
Orodha ya miradi tunayotarajia kuifanya
1. Kufanya ujenzi wa kanisa
2. Kuanzisha radio station na Television
3. Kuanzisha shule ya awali na Msingi
4. Kuanzisha chuo cha watenda kazi wa kiroho
5. Kufungua matawi nje ya nchi na ndani ya nchi
6. Kujenga ukumbi wa mikutano na semina
4
MISIMAMO
YETU
Mambo yote tunayoamini tumeyaamini baada ya kuyasikia kutoka kwa Mungu
Tumeshika hayo mambo kana kwamba ndiyo misimamo yetu na kupelekea hiyo misimamo kuwa ndiyo
tamko letu la Imani la pamoja.
Tunaiita hiyo misimamo ni Imani yetu.
1. Biblia ni maandiko matakatifu ya Mungu.
2. Neno la Mungu ni lile ambalo Mungu analisema kwa ajili ya kutuvusha mahali Fulani,
yawezekana likawa linatoka kwenye Biblia au linalotoka kwa unabii.
3. Kuhusu upako
4. Kuna upako wa Roho Mtakatifu unaofanywa nay eye mwenyewe
5. Kuna upako wa mtumishi wa Mungu unaofanywa na mtumishi wake Mwenyezi Mungu.
6. Na Mengine ambayo tunayaamini utayapata katika kitabu chetu cha Mwongozo wa Kanisa au
Kanuni za Imani za kanisa katika Sura ya 17, uk. Wa 64.
5
MAONO
YETU
Maono yetu ni mambo tuliyopewa na Mungu ili tuyafanye.
Haya ni mbali na yale ambayo tunayafanya ili tupate fedha, bali ni yale tuliyoitiwa na Mungu na
kutufanya kuanzisha kanisa badala ya kujiunga na makanisa mengine, huu utofauti ndio tunaouita
maono.
Maono haya yalimjia Mtume na Mchungaji wa kanisa hili kama ifuatavyo:
 Mafundisho ya Imani ya Kristo kupitia injili ya kweli.
 Upendo
 Imani kamili-Tunamwamini Yesu ndani ya Mioyo yetu na siyo kimazoea tu kama wengine
maana kama Yesu alishachukua magonjwa pale msalabani basi sisi hatuhitaji tena kumwambia
Mungu atuponye badala yake tutaamini kuwa tuna uponyaji kamili ndani yetu, ni kiwango tu cha
kuamini na kupokea uponyaji huo kutoka kwenye kifo cha Kristo. Namengine mengi
aliyoyafanya pale msalabani.
 Mungu hatambui dini za duniani-Katika kitabu cha Yakobo 1:27 inasema dini ya kweli na isiyo
na taka mbele za Mungu ni hii, kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na
kujilinda na dunia pasipo mawaaa. Mtu atakayeyafanya haya atahesabiwa kuwa miongoni mwa
wana wa Mungu.
 Mavazi na muziki katika kanisa
o Mavazi yenye adabu na heshima mbele za watu ndiyo
yanayokubaliwa na Mungu , kuna mavazi ya kikahaba
yanatambuliwa na Biblia, na kuna mavazi ya heshima
yanatambuliwa na Biblia.
o Muziki na uchezaji wa Muziki ni vitu vinavyoweza kuondoa utukufu
wa Mungu na pia unaweza kumpa Mungu utukufu, hii inategemea
na muhusika katika Muziki wenyewe jinsi alivyouandaa muziki
wake na kuuwasilisha mziki, na mpokeaji alivyoupokea muziki na
namna ya kuucheza.
6
HATUA TULIZO
CHUKUA
Hatua ni hali ya uwajibikaji ambayo inachukuliwa na kuanza kutendewa kazi.
Tumeanza kuwatembelea wahitaji nyumba kwa nyumba na kufanya nao ibada,
Tumeanza kuyafanyia kazi maono yote kwa kufundisha na kutoa semina mbalimbali zilizo rasmi na
zisizo rasmi.
Tanzania, Rwanda, na Indonesia ni mahali ambapo tumeanzia na hatimaye ulimwenguni kote kama
ilivyo maana ya Jina la kanisa letu.
Askofu Mkuu,
Apostle REV. Anthony J Mwakifwamba
P.O.Box 2256, Dodoma,
41217 Ilazo, Daraja dogo, Merriwa street,
House 10.
7
Download