KWAYA YA MTAKATIFU YOHANE PAULO WA PILI PAROKIA YA KUNG’ARA KWA YESU KRISTO MBEZI MSHIKAMANO ; Kyp02_choir ; kwaya ya Mt.Yohane Paulo II ; Kyp02@gmail.com YAH: MWALIKO WA SIKUKUU YA YOHANE. Tunayofuraha kukualika Mwalimu Philipo, Mwalimu wa kwaya ya Mt. Maria Goretti Tabata, katika sikukuu yetu ya Mtakatifu Yohane Paulo wa pili itakayofanyika siku ya jumapili tarehe 22/10/2023 parokiani kuanzia saa 1:30 tukianza na misa takatifu na kumaliza na tafrija fupi ya kiparokia, aidha kutakuwa na mafungo siku ya jumamosi 21/10/2023, ambayo yatahusisha semina yenye mada isemayo “UTUME WA UIMBAJI NA UKRISTO WETU”, Kitubio na Misa takatifu. Kadhalika tungependa kama ungeweza kujumuika nasi katika zoezi letu la mwisho siku ya ijumaa tarehe 20/10/2023. Wako katika utume J.MBURA Mwalimu wa Kwaya.