Hadithi Za Kiswahili Jibu maswali yafuatayo 1. Jina la msichana mwenye anaongelewa kwa hadithi ni? Cindarella. 2. Baba wa Cindarella alikuwa na bibi ngapi? Alikuwa na bibi wawili, bibi wa kwanza ambaye ni mama wa Cindarella aliaga dunia. 3. Cindarella alikuwa na ndugu ngapi wa kambo? Wawili. 4. Babake Cindarella alipoenda kazini nini ilifanyika? Mama yake wa kambo, alimfanya Cindarella awe kama mfanyikazi wa nyumba na alimtesa sana. 5. Ndugu zake wa kambo, Cindarella walimpenda? La hasha, ndugu zake wa kambo hawakumpenda kwa sababu ya urembo yake. 6. Askari wa mfalme alitangaza nini? Aliwatangazia kwamba wanakijiji wote wahudhurie hafla ya mtoto wa mfalme. 7. Hafla hiyo ilikuwa ifanyike wapi? Katika nyumba ya mfalme. 8. Ajili ya hafla hiyo ilikuwa nini? Ilikuwa kwa ajili ya kuchagua mtoto wa kike ambaye atakuwa mkewe wa mtoto wa mfalme. 9. Ni nani alimsaidia na kumwezesha Cindarella kuenda katika hafla ya mtoto wa mfalme? Mjumbe wake kutoka kwa mama yake. 10 .Mamake Cindarella wa kambo na watoto wake walihukumiwa jela miaka mingapi na kwa nini? Walihukumiwa jela kwa miaka mitatu kwa sababu ya kumdanganya mlinzi wa mfalme. Lakini baadaye, Cindarella aliwatakia msamaha na walitoka gerezani.