Uploaded by Emmanuel John

Year-III-Review-Mtakuja-Development-Project-Swahili

advertisement
Mtakuja Development Project 2011
Mtakuja Development Project
Shughuli za mwaka wa tatu – Juni 2010 hadi Mei 2011
Mtakuja Village – Kilimanjaro Region – Tanzania
The Mtakuja Development Project is an initiative supported by FD Kilimanjaro, an international
NGO registered in the Netherlands and Tanzania.
1|P ag e
Mtakuja Development Project 2011
MAENDELEO ENDELEVU NA USHIRIKI WA JAMII
Chama cha Maendeleo ya Jamii Mtakuja
kimekuwa na tabia ya kuwa na mikutano
ya kila mwezi.
Kuunda umiliki wa ndani - Bodi ya vikao
vya chama imepokea mafunzo 8 kutoka
Floresta juu ya masomo kama uongozi na
ujenzi wa taasisi.
Rasimu ya katiba - Rasimu ya katiba ya
chama ilitolewa.
VICOBA – Vikundi saba vya benki ya vijiji ya jamii viliundwa mapema mwaka 2009.Wakati wa
mwaka wa tatu wa mradi huo, vikundi viliendelea kukuza akiba zao na kupokea mafunzo.
Kukopa kunakadiriwa kufanyika ni kati ya Tshs. 7 m. Jumla ya akiba kwa ajili ya makundi yote ni
mpaka kufikia Tsh. 11 m (au € 5000).
SACCOS – Ofisi ya SACCOS ( Chama cha Ushirika cha kuweka na kukopa) ilifunguliwa katika kijiji
cha Mtakuja. Uanzishwaji wa SACCOS unapaswa kuongeza upatikanaji wa huduma za kuweka
akiba kitaaluma zaidi na huduma za mikopo. Wakulima katika mpango wetu wa umwagiliaji
wana fursa ya kupatiwa mikopo.
MAPATO & KILIMO
Uanzishwaji wa chama cha uwezo wa ndani. Kamati ya wanachama 15 iliundwa ikiwa na
wawakilishi wa kijiji. Baada ya muda fulani, kamati itachukua jukumu la usimamizi wa jumla na
usimamizi wa mradi na hasa mpango wa umwagiliaji.
Uzalishaji mazao. Wakulima 95 walichaguliwa na kulima nusu ekari katika mashamba ya mfano.
Waliamua kuanza na mahindi na mavuno yanatarajiwa mwezi Septemba. Wanawake ni 60% ya
wakulima waliochaguliwa.
Wakulima viongozi - wakulima viongozi 8
na wakulima viongozi wasaidizi 8 walipewa
mafunzo na kuanza kazi yao kwa kujitolea.
Mkulima kiongozi na msaidizi kwa pamoja
huongoza vishamba vya umwagiliaji yenye
wakulima 24 katika mashamba ya mfano.
Wao hupata mafunzo ya kila mara na
hufanya kazi kwa bidii sana.
Mseto wa mazao ya biashara - Majaribio
kwa mazao mengine yenye faida
yameanzishwa.
2|P ag e
Mtakuja Development Project 2011
AFYA
Kambi ya matibabu kwa watoto - Kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Uholanzi
uchunguzi wa matibabu kwa watoto (MCC) na katika ushirikiano wa karibu na hospitali ya TPC
na kituo cha afya cha kijiji walikuwa wenyeji wa kambi ya pili ya kila mwaka ya matibabu.
Watoto 1,226 wenye umri chini ya miaka 10 walifanyiwa tathmini, kutibiwa na inapokuwa
muhimu walihamishiwa kwa watoa huduma za afya wa kawaida na timu ya wataalamu wa afya
11 kutoka MCC. Mwaka huu wataalamu kwa ajili ya ulemavu, macho na meno walijiunga na
kambi.
Huduma ya mtu binafsi - Watoto wenye haja ya huduma ya matibabu ya haraka wamekuwa
wakisaidiwa na FDK kwa upasuaji kuanzia kukarabati ‘cleft palate’, upasuaji wa shida ya njia ya
mkojo na upasuaji wa mguu iliyopinda ‘club foot’. Upasuaji wote ulikuwa ukifanyika hapa
Tanzania.
Kusaidia watoto wenye ulemavu – FDK wanashirikiana na shirika lisilo la kiserikali CCBRT
(Comprehensive Community Based Rehablitation in Tanzania) kutoa miundo ya ukarabati
waviungo kwa watoto wenye ulemavu katika kijiji cha Mtakuja. Hesabu ilitolewa ya watoto
wenye ulemavu na wao kusaidiwa kutokana na ushirikiano huo.
Kituo cha elimu ya kuzuia magonjwa – Kwa
msaada kutoka Rotary Club (SoetBaarm/Ahlen) kituo cha elimu ya kuzuia
magonjwa kilijengwa. Hiki ni kituo cha afya
vijijini cha mkazo maalum juu ya kuzuia
maambukizi kwa njia ya mafunzo,
maonesho na kuwezesha upatikanaji wa
habari. Pia huduma za afya ya msingi
itatolewa. Timu ya wafanyakazi wa afya ya
jamii imepatiwa mafunzo ya kutumikia
jamii.
ELIMU
Chakula cha mchana shuleni - Kwenye shule mbili za msingi na shule tatu za awali vyakula vya
mchana 180,310 vilitolewa kwa wanafunzi 968.
Taa za nishati ya jua – Taa 500 zinazotumia nishati ya jua zimegawanywa kwa wanafunzi wa
shule ya msingi. Kwa njia hiyo wakati wa giza wanaweza kufanya kazi zao za nyumbani
wanazopewa kutoka shule na kuboresha matokeo yao.
Masaa ya ziada ya mafundisho – Walimu katika shule za msingi wamefundisha masaa 8,188 ya
ziada baada ya masaa ya kawaida ya shule na hapo hupokea motisha kidogo kila mwezi kutoka
FDK.
3|P ag e
Mtakuja Development Project 2011
Shule ya awali na uwanja wa michezo – Shule ya msingi ya awali iliyo katika kitongiji cha
Wamasi cha jirani – Remiti- Mtakuja kimemalizika na kufunguliwa rasmi. Kando yake uwanja
wa michezo ulianzishwa. Kina sifa mbalimbali na
madhumuni ya kuwawezesha watoto wadogo kukuza
vipaji.
Mipango ya udhamini - Programu ya mwaka ya
udhamini wa wanaohitimu shule ya msingi iliendelea
kwa wanafunzi 10 wengine wenye kufanya vizuri
kupelekwa kwenye shule binafsi ya sekondari iliyopo
Mtakuja.
Msaada katika shule za sekondari - Ilitoa bajeti kusaidia
shule ya sekondari Mtakuja katika ujenzi wa madarasa
ya ziada ili kutosheleza ukuaji mkubwa wa idadi ya
wanafunzi katika shule.
Mafunzo ya ufundi stadi - Mpango wa udhamini kwa
ajili ya mafunzo ya ufundi umeshaanza. Wanafunzi 6
waliochaguliwa wanajifunza ujuzi wa vitendo.
MIUNDOMBINU
Barabara - TPC Ltd imesaidia kujenga karibu km 4 za barabara kuwezesha kufika katika shamba
la mfano, ikiwa ni pamoja na barabara ndogo ndani ya shamba.
Umeme – Ujenzi wa usambazaji wa nishati, km 4 za miundombinu umeme, ikiwa ni pamoja na
transformer, ilifanywa na kampuni ya usambazaji wa umeme Taifa, ilikamilika Januari 2011.
Uunganishaji na maandishi yote yalikamilika mwezi Machi.
Mpango wa umwagiliaji – nusu ya eneo la mpango wa umwagiliaji, hektari 20 umemalizika.
Mpango huu hutumia mfumo wa bomba msukumo, ambapo mabomba makuu na matawi yake
yamefukiwa ardhani. Ilikuwa ni kazi kubwa yenye vikwazo vingi lakini ilimalizika baada ya kupata
umeme. Hivi sasa utaratibu wa vinyuyizii unatumika kumwagilia vishamba 96 ya nusu eka kila
kimoja.
Maji – Mnamo Julai 2009 visima viwili
vilichimbwa na vinafanya kazi sasa. Maji
yanatumika kwa ajili ya umwagiliaji lakini
pia vituo vya maji ya matumizi ya
nyumbani vimeanzishwa.
Ofisi ya shamba – ofisi ilijengwa katika
eneo la shamba la mfano na kutumika
kama eneo la vikao na kuhifadhia vifaa. Ni
yenye muundo wa veranda kubwa yenye
kukidhi aina mbalimbali za mikutano na
vikao vya kijiji.
4|P ag e
Mtakuja Development Project 2011
WAFANYAKAZI
Watumishi - FD Kilimanjaro ina wafanyakazi wawili ambapo wameajiriwa kwa muda mrefu. Zablon
Sarakikya ni afisa programu ya kilimo anashughulika na shamba la mfano lakini pia ana jukumu
muhimu kuwasiliana na uongozi wa kijiji. Stela Msarikie kutoka Mtakuja ni afisa ustawi wa jamii na
ana jukumu muhimu la kudumisha mawasiliano na kushirikisha wanajamii, hasa wanaoishi katika
mazingira magumu. Kijiji kimeajiri walinzi watatu na msadizi wa umwagiliaji kwa ajili ya shamba la
majaribio.
Mwaka wa tatu – kuendelea kuweka mpango katika vitendo
Kama inavyoonekana hapo juu, katika mwaka wa tatu Mradi wa Maendeleo Mtakuja
umeshatekeleza shughuli nyinngi, kupitia katika maeneo yetu makuu ya programu afya, elimu, kilimo
na mapato na miundombinu.
Kulinda uendelevu na matokeo ya kudumu ya utekelezaji wa kazi za mradi hata baadaya kipindi
cha muda wa mradi.
Tunatafuta kushirikisha jamii wakati wote,
kuanzia kufanya maamuzi mpaka mipango ya
fedha na michango yote. Mikutano inaandaliwa
katika ngazi za vitongoji na mikutano na
viongozi wa kijiji hufanyika mara kwa mara na
mara nyingi huwa sio rasmi.Imekuwa wazi
kwamba wigo wa mradi na fursa zake ni vigumu
kueleweka kwa wanajamii wengi, lakini uelewa
wao ni muhimu kwa mafanikio ya mradi ya
muda mrefu. Kama mmoja wa washirika wetu
wa Tanzania anasema:”Mbali na mambo
mengine umasikini unaathiri mawazo ya watu
na tabia”.
Katika miaka ijayo, usimamizi wa majukumu ya
mradi yatatakiwa kuchukuliwa na wanajamii.Kuunda chombo kwa ajili ya hili, kamati ya mradi
iliundwa ikiwa na wanachama 15, ambao wanatakiwa kupitishwa katika chama na kuwezeshwa na
halmashauri ya kijiji. Hii inathibitisha kuwa ni njia yenye ugumu lakini yatupasa kuifuata.
Kuongeza mapato ya mwaka ya wanajamii kupitia kuongeza mapato kutokana na kilimo na
shughuli nyingine za kibiashara, wakati huo tunahakikisha kila mtu katika jamii anapata milo
mitatu kwa siku kwa mwaka mzima.
Hatua kubwa ilikuwa mwanzo wa kilimo katika mashamba ya majaribio. Sasa hectari 20 za mwanzo
zinalimwa na wakulima 96 waliochaguliwa na wanajamii. Ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa
nishati ya umeme ulianza Aprili 2010 na ulichukua muda mrefu kuliko ilivyotegemewa mpaka kupata
umeme wa uhakika Januari 2011. Shamba la mfano ni kitovu cha mradi huu, mpango wa kuongeza
hectari 20 nyingine tayari upo katika matayarisho. Matokeo yanayotegemewa kama pato la kilimo
5|P ag e
Mtakuja Development Project 2011
katika shamba lililomwagiliwa inatakiwa kuthibitisha ongezeko kubwa la usalama wa chakula wa
watu kwa muda ikiwepo na kuongeza ardhi ya kumwagiliwa – kuongeza pato la kilimo itapelekea
ongezeko la ngazi za pato la ziada. Kilimo ni mpango w amuda mrefu haitasababisha mfululizo wa
ukuaji kiuchumi, bali kitaboresha usalama wa watu katika chakula, kinga dhidi ya majanga ya
kiuchumi,kuboresha hali za kiafya na kutoa msingi kwa ajili ya watu kuendeleza vyanzo vingine vya
mapato na shughuli nyingine za kiuchumi.
Mashamba ya majaribio inaonekana kuwa na
mazao ya mahindi yenye afya wakati mazao ya
katika maeneo mengine ya kijiji yalishindwa kwa
sababu ya ukame. Ilihitaji juhudi kubwa kufikia
hapa, wanajamii walifanya kazi kwa pamoja ili
kusafisha eneo la majaribio, kuondoa vichaka,
miti na visiki vya miti na kuchimba mitaro kwa
ajili ya mabomba na kuondoa visiki 100 vya miti
mikubwa.
Wakulima viogozi wa Mradi na wasaidizi wa
wakulima viongozi ni mfano wa wanakijiji wenzao na kucheza nafasi ya kijamii katika jamii. Wapo 16
wanaume na wanawake waliochaguliwa kutoka kwa wanajamii ili kuongoza wakulima katika juhudi
zao za kilimo.
Shamba la majaribio kwa sasa hutumiwa na wakulima 96 na mara baada ya kukamilika, ekari 100 ya
ardhi iliyomwagiliwa itawezesha karibu wakulima 190 (ikiwa ni pamoja na wakulima viogozi) kwa ajili
ya kulima nusu eka kwa msimu. Wakulima wa kwanza walichaguliwa na viongozi wa vitongoji kwa
kuangalia jitihada zao za kufanya kazi ya jamuiya na katika kuandaa shamba. Kupitia mfululizo wa
mikutano ya hadhara katika ya vitongoji. Majina ya wakulima waliochaguliwa yaliwekwa wazi kwa
umma. Wakulima wengi ni wanawake na vitongoji kuwakilishwa kufuatana na idadi yao ya wakazi.
Kuongeza upatikanaji na utumiaji wa huduma za afya ya msingi ndani ya nchi na ziada ya huduma
maalumu zaidi, wakati huo kuboresha afya kwa ujumla na uelewa wa masuala ya afya na
magonjwa.
Mwaka wa 3 umeona hatua muhimu katika kufikia malengo ya programu ya afya. Kwa msaada
kutoka kwa klabu ya Rotary ya Soet-Baarm (Uholanzi) na Ahlen (Ujerumani) mradi umejenga kituo
cha afya kwa lengo maalum juu ya kinga na kuanzisha timu ya wafanyakazi wa afya ya jamii.
Wafanyakazi wa afya ya jamii wana kawaida ya kutoa mafunzo ya msingi – kwa kuzunguka au
majumbani - huduma za afya, lakini pia kutafuta na kuhamasisha na kuongoza vizuri wagonjwa na
familia ili kupata huduma zetu za afya.
Kwa sababu kuna zahanati na hospitali karibu si vizuri sana kujenga zahanati au kliniki nyingine.
Matatizo ya afya kwa Mtakuja yanaonesha kuwa kuna masuala mengi ya afya kuhusiana na hali duni
ya maisha, usafi wa mazingira, ukosefu wa elimu, usafi, dawa za kuzuia na chanjo; kwa ufupi kinga.
Kwa sababu hizi inaonekana bora zaidi kuwa na lengo la kuzuia na huduma za afya ya msingi. Kituo
cha kuzuia kitakuwa kuzingatia wenyeji wote wa Mtakuja (4500) kwa kuzuia na upande wa Kusini wa
kijiji kwa ajili ya huduma za afya ya msingi (ina karibu watu 2200).
6|P ag e
Mtakuja Development Project 2011
Wafanyakazi wa afya ya jamii wamechaguliwa
kutoka kijijini na kupata mafunzo kutoka
Hospitali ya TPC na Wizara ya Afya. Ni
wanawake 3 na wanaume 2 na kwa sasa
wanafanya kazi kikamilifu katika kijiji kuelimisha
watu katika usafi wa mazingira, afya na huduma
ya afya ya msingi. Pamoja na kituo, nyumba za
wafanyakazi zimejengwa kwa ajili ya malazi ya
baadhi ya wafanyakazi wa afya ya jamii ya
utunzaji wa kituo na
inapopatikana kwa
dharura.
Kazi ya kituo cha kuzuia magonjwa na wafanyakazi wa afya ya jamii ni:










Kupima uzito wa watoto,
Ushauri wa lishe,
Huduma za kabla na baada ya kujifungua,
Huduma ya kupima upungufu wa damu na usambazaji wa kuongeza madini ya chuma,
Kampeni ya vitamini A,
Kampeni dhidi ya minyoo,
Chanjo,
Elimu ya akina mama,
Elimu katika usafi na usafi wa mazingira.
Kambi ya Kituo cha matibabu, mara moja kwa mwezi kwa ajili ya walemavu, mara moja kwa
mwezi kwa ajili ya huduma za meno, mara mbili kwa mwaka kwa matatizo ya jicho na mara
mbili kwa mwaka kwa ajili ya matatizo ya Masikio Pua na Koo.
 Upimwaji wa VVU / UKIMWI na ushauri mara moja kwa mwezi,
 Rufaa ya matatizo ya afya kwenda hospitali ya TPC au kwa mtaalamu.,
 Huduma ya kufuatiliwa baada ya
wagonjwa kurudi nyumbani,
 Muendelezo wa maonyesho ya taarifa za
matibabu,
 Kituo kwa ajili ya wafanyakazi wa afya ya
jamii,
 Kushirikiana na taasisi na mashirika husika.
Mnamo Agosti 2010 tukiwa pamoja na shirika
lisilo la kiserikali Kontrollerna Matibabu kwa
Watoto (MCC) kwa ajili ya shirika la wataalamu
wa kujitolea katika huduma za afya tulipanga
kambi ya pili ya matibabu. Timu ya watu 11 ya kujitolea wenye historia mbalimbali za afya, walikuja
Mtakuja kufanya tathmini ya afya ya msingi ya watoto na kutoa huduma ya juu kwa ajili ya safu ya
tathmini ya matibabu na huduma za afya.Tathmini ililenga sana juu ya utapiamlo masuala mengi
yanayohusiana na afya, ikiwa ni pamoja na minyoo , upungufu wa damu, upungufu wa vitamini na
matatizo ya ngozi na mambo mengine.
7|P ag e
Mtakuja Development Project 2011
FD Kilimanjaro iliwashirikisha hospitali ya TPC katika kutoa huduma ya awali za kufuatilia, ikiwa ni
pamoja na maabara ya uchambuzi wa sampuli za kinyesi, mkojo na damu. Kwa kuwashirikisha TPC
hospitali ni uhakika kwetu sisi kwamba watoto wowote waliokutwa na matatizo ya afya, ambayo
inahitajika kufuatilia au huduma ya kuendelea
watapata huduma bora inayohitajika. Katika
mtukio mengi FD Kilimanjaro waligharamia
gharam zote za ufuatiliaji. Wakati wa kambi ya
pili ya matibabu timu ya MCC iliwahudumia
watoto 1223. Wafanyakazi wa MCC walifanya
kazi pamoja na timu ya wanawake kutoka
ambao walifanya kazi kama watafsiri na
wakalimani.
Wakati wa kambi ya mwaka 2010, TPC hospitali
ilitoa muuguzi mfanyakazi wa VVU / UKIMWI
kwa taarifa na ushauri nasaha kwa familia
zinazopenda kupata elimu na mtaalamu wa meno kwa ajili ya kuangalia meno na kutoa maelekezo
ya namna ya kusafisha meno. Mwaka 2010 pia tulimtambulisha mshirika wetu katika huduma ya
afya Comprehensive Community Based Rehabilitative Care Tanzania (CCBRT) ndani ya kambi. Wao ni
maalum kwa watoto walemavu na walitambua kesi zaidi ya 20 kubwa sisi tulitoa msaada na
ufuatiliaji kwa mwaka mzima. Wengine walifanyiwa upasuaji, wengine kupokea zana maalum na
mazoezi. Kila wiki baadhi ya watoto wenye ulemavu wanatembelewa na kupata huduma.
Kuongeza upatikanaji na matumizi ya elimu bora ya awali, msingi na sekondari na kukuza
machaguo kwa ajili ya elimu ya ufundi na elimu ya watu wazima.
Elimu inabakia sehemu muhimu ya mradi huu. Katika mwaka wa 3 tuliendelea kupanua mipango ya
chakula cha mchana katika shule za msingi na kupanua wigo shule 3 za chekechea. Tuliendelea na
programu ya masaa ya ziada ya masomo ambapo wanafunzi wa shule za msingi hupata masomo ya
ziada baada ya masaa ya kawaida ya shule na wakati wa likizo. Shughuli hizi bado hazijaonyesha
ongezeko katika matokeo ya elimu.
Wakati wa mwisho wa mwaka 2010 wa shule, asilimia 39% tu ya wanafunzi walifaulu mitihani yao ya
mwisho na kuwawezesha kuendelea shule ya
sekondari. Tunafanya kazi katika hili kwa
kusaidia shule za msingi katika programu ya
kuboresha matokeo kwa kuongeza idadi ya
vitabu kutoka kitabu kimoja kwa wanafunzi
watano hadi kitabu kimoja kwa wanafunzi
wawili. Pia vifaa vya elimu vya ziada
vilinunuliwa kama madaftari, ubao wa rangi,
vitabu vya rejea, rula n.k. Elimu ya msingi
inaathiriwa na sababu nyingi, moja ni kwamba
wazazi hawatambui umuhimu wake.
8|P ag e
Mtakuja Development Project 2011
Mwishoni sisi tunatoa msaada kwa mashule katika jitihada zao za kuboresha ufahamu wa kiingereza
kwa mwanafunzi kupitia madarasa ya ziada.
Mwaka 2010 tulikamilisha ujenzi wa chumba cha darasa la shule ya awali ya msingi katika kitongoji
cha Wamasai kiitwacho Remiti. Darasa hilo ni sehemu muhimu ya Shule ya Msingi Mserikia na chini
ya usimamizi wa mwalimu mkuu wa shule hiyo. Watoto wadogo wa Kimasai sasa wanaweza kuanza
shule katika umri wa miaka 4 au 5, Na wakati huo hakuna kukabiliana na mwendo mrefu katika njia
ya vichakaiendayo Shule ya Msingi Mserikia. Kama ilivyo katika mipango yetu jamii imetoa mchango
mkubwa wa fedha na nguvukazi. Wizara ya elimu imeleta mwalimu mpya na jamii imeajiri
mfanyakazi msaidizi wa elimu ambaye anajua lugha ya Kimasai. Sasa darasa lina wanafunzi 42.
Uwanja wa michezo kama shughuli tofauti ulitengenezwa katika shule ya chekechea na watu wa
kujitolea. Kucheza ni muhimu na husaidia sana katika maendeleo ya mtoto na pia wanafurahia.
Mnamo Agosti 2010 mpango wa udhamini wa sekondari uliendelea katika awamu yake ya
pili.Programu ina mpango wa kupeleka wanafunzi wanaofaulu vizuri kutoka kwenye shule mbili za
msingi Mtakuja kwenda kwenye shule ya kibinafsi ya sekondari iliyopo kijijini. Katika wahitimu 10 wa
mwaka jana 8 katika yao wamefaulu vizuri sana na kuendelea na kidato cha II.Wahitimu wengine 10
wamechaguliwa na wameshaanza kidato cha I.
Wanafunzi wamepokea misaada kwa asilimia 70
hadi 100 na wanasaidiwa kwa miaka minne ya
shule ya sekondari,inategemea na matokeo
mazuri ya kila mwisho wa mwaka.
FD Kilimanjaro imeanzisha programu ya
udhamini wa mafunzo ya ufundi stadi kwa
kusaidia wadhaminiwa 6 wa mafunzo ya ufundi
stadi.Uchaguzi wa makini ulifanyika kwa kufuata
hatua ya kuangalia wanajamii wanaopendelea kuomba udhamini waombaji watakaofanikiwa
watafanyiwa usahili. Tulichagua wasichana 4 na wavulana 2 kujiunga na kozi kama: umeme na
mabomba.
FEDHA ZA 2010
FD Kilimanjaro ilikuwa na bajeti ya Euro 370000 kwa mwaka 2010 ambayo ilitumika kama ifuatavyo:
9|P ag e
Mtakuja Development Project 2011
Kuendelea mbele mwaka wa nne
Kwa kuangalia mwaka nne tunategemea mwaka mwingine wa furaha. Mchakato muhimu utafanyika
wa kuanzisha msingi wa uendelevu wa mradi huo na kurasimisha na kuendeleza umiliki wa ndani.
Tutaendelea kusonga mbele na kupanua shamba la mfano na kuwawezesha wakulima. Ushirikiano
na makampuni utaendelea kugunduliwa kwa kupanda maua, mbegu n.k. Mwaka 2011 tutaanza
kutumia kituo cha kuzuia magonjwa na kutarajia mambo mengi kutoka kwa wafanyakazi wa afya ya
jamii ili kupambana na matatizo ya afya ya kawaida kuhusiana na afya na lishe. Kambi nyingine ya
matibabu itapangwa pamoja na MCC. Mwezi Septemba wafanyakazi wa filamu watatengeneza
makala nyingine kama walivyofanya mwaka 2009. Ni tathmini ya kuonekana ya mradi na ni matokeo
ya maisha katika kijiji, lakini pia kutumika kwa ajili ya kubadilishana habari kati ya kijiji na washirika.
Tunaendeleza programu zetu za udhamini ili kuongeza nafasi za ajira. Mradi unahitaji kuangalia kwa
umakini zaidi shughuli za kielimu kuangalia namna gani matokeo ya shule ya msingi yataboreshwa;
kitu kingine tulichopanga ni ujenzi wa nyumba za walimu kuboresha mazingira yao yakuishi. Kwa
kujenga makazi madogo pamoja na kujenga kituo cha kuzuia tunataka kujenga mazingira salama ya
kuishi na pia kufurahia maji katika maeneo ya jirani kwa kufanya hivyo kuvutia walimu. Mwaka 2011
tunategemea kuanzisha ushirika na Heifer International kuleta programu ya mifugo Mtakuja,
programu hii itawezesha familia zenye matatizo zaidi waweze kujipatia vyanzo vya mapato na nafasi
ya kuboresha lishe yao kwa kuanzisha unywaji wa maziwa, mayai au nyama katika mlo wao. Pia
tunaendelea kuwezesha familia kwa kununua taa za ruzuku za nishati ya jua kuleta mwanga usiku
kwenye nyumba zao na kuwezesha watoto wanaokwenda shule kujisomea usiku. Baadhi ya mawazo
mapya yatakuwa yanaendelea kugunduliwa kama vile uhifadhi wa chakula na matumizi ya gesi asilia.
Pamoja na hayo yote, tutaendela kuendeleza programu zetu na kuendelea kujenga ushirikiano
ambao tumeshaujenga hadi sasa, na kuendelea kutafuta ushirikiano mpya wenye faida na mashirika
mengine ya kushirikiana nayo.
10 | P a g e
Mtakuja Development Project 2011
www.fdkilimanjaro.org
Tunawashukuru washirika wetu wote na wanaotusadia:
TPC Ltd. Na Hospitali ya TPC, Kliniki ya Macho KCMC, Floresta Tanzania,Kituo cha Mafunzo ya Kilimo
Kilimanjaro (KATC), AquaTech Ltd, Comprehensive Community Based Rehabilitation in Tanzania
(CCBRT), D-light, FERT & USAWA, Wilaya ya Moshi Vijijini, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro,
Medical Checks for Children (MCC), Mama International, Zero-kap, na Stichting End of Poverty.
Wadhamini wa fedha wa awali na wadhamini waanzilishi wa FD Kilimanjaro ni Stichting FEMI. Mradi
wa Maendeleo Mtakuja umepokea msaada wa ziada kutoka Stichting DIRA 1, The Rotary Club Soest
Baarn ( na washirika wa shirika la Rotary Ahlen, Germany), De Wilde Ganzen, MCC, Rooms
Katholieke Stichting Bijzondere Gezondheidszorg (SBG) na Net4Kids; wote ni wa Uholanzi. Kwa
Tanzania tunashukuru tumepokea msaada kutoka kwa Rural Energy Agency (REA), Programu ya
ushirikishwaji na kuwezeshwa katika maendeleo ya kilimo (PADEP) na Kampuni ya TPC.
11 | P a g e
Download