Uploaded by faith.shimba

Misingi ya Imani ya Kikristo

advertisement
MISINGI YA IMANI YA KIKRISTO
Faith Shimba
KANISA LA PENTEKOSTE KIJITONYAMA Parishi ya Mwananyamala
0
Yaliyomo
MISINGI YA IMANI YA MKRISTO – MISINGI YA IMANI YETU. ........................... 0
UMUHIMU WA KUWA NA MSINGI SAHIHI ........................................................... 0
MSINGI NI NINI? ...................................................................................................... 0
UANAFUNZI -- DISCIPLESHIP ..................................................................................... 2
Mwanafunzi ni nini? ....................................................................................................... 2
Gharama za uanafunzi: ................................................................................................... 3
Matokeo ya uanafunzi: .................................................................................................... 3
Wajibu wa mwanafunzi: ................................................................................................. 3
KUTUBIA KAZI ZISIZO NA UHAI................................................................................. 4
TOBA NI NINI? ............................................................................................................. 4
KAZI ZISIZO NA UHAI................................................................................................ 4
IMANI KWA MUNGU. ..................................................................................................... 5
MAFUNDISHO YA MABATIZO. .................................................................................... 6
Ubatizo katika mwili mmoja. .......................................................................................... 6
Ubatizo katika Roho Mtakatifu ....................................................................................... 6
KUWEKEA MIKONO ....................................................................................................... 8
Kuwekea mikono nini? ................................................................................................... 8
Sababu za kuwekea mikono: ........................................................................................... 8
Umuhimu wake katika kanisa. ........................................................................................ 8
Maswali ya kujadili: ........................................................................................................ 9
UFUFUO WA WAFU ...................................................................................................... 10
Mifano ya mifano ya ufufuo katika biblia: ................................................................... 10
Kuna maeneo matatu ya ufufuo tunayopaswa kuya angalia ......................................... 10
Ufufuo wa Yesu kristo. ................................................................................................. 10
Ufufuo wa kiroho wa waaminio. .................................................................................. 10
Ufufuo ujao utatokea lini? ............................................................................................ 10
Waaminno watafufuliwa. .............................................................................................. 11
Ufufuo wa wale wote walio lala mauti. ........................................................................ 11
Kiti cha hukumu cha kikristo ........................................................................................ 11
HUKUMU YA MILELE .................................................................................................. 12
Hukumu maana yake nini?............................................................................................ 12
Hukumu ya milele ni nini? ............................................................................................ 12
Kwnini kuwe na hukumu? ............................................................................................ 12
1
Hakimu ni nani? ............................................................................................................ 12
Hukumu hii itatokea lini?.............................................................................................. 13
Tayari imetokea: ....................................................................................................... 13
Inaendelea kutokea: .................................................................................................. 13
Itatokea wakati ujao .................................................................................................. 13
Itatokea wapi? ............................................................................................................... 13
Nini kitatokea? .............................................................................................................. 13
1
MISINGI YA IMANI YA MKRISTO – MISINGI YA IMANI YETU.
UMUHIMU WA KUWA NA MSINGI SAHIHI
Waebrania 5 : 11 – 6 : 3
1 kor 3 : 10 – 15
Luka 6 : 46 – 49
1 petro 2 : 5
MSINGI NI NINI?
Msingi ni kitu ambacho juu yake jengo hujengwa.
Ni kitu ambacho hutia nguvu jengo liweze kusimama imara.
Kama wanafunzi wa Yesu maisha yetu ya kiroho ni jengo, katika maandiko jengo
hili limepewa majina mbalimbali. Mfano: ‘hekalu la Roho Mtakatifu’, ‘hekalu la
Mungu’, (1 kor 6 19, 1 kor 3 :16, 1 kor 3 : 9, 1 petro 2 : 5.).
Msingi wa jengo hili ni nani?
1 kor 3 :11.
Unajenga juu ya nini?
Luka 6 :46 – 49.
Msingi wa maisha yetu ya kikristo ni wa muhimu sana kiasi kwamba haiwezekani
kuendelea kukua kiroho bila kuwa nao.
Waebrania 6: 1 - 3 inaorodhesha mafundisho ya msingi ambayo ukristo wetu
unapaswa kujengwa juu yake. Mafundisho haya ndiyo tunayo yaita mafundisho
ya msingi au MISINGI YA IMANI YETU KAMA WAKRISTO
Dalili za uchanga kiroho katika maisha ya mkristo :
1. Uvivu wa kusikia Ebrania 5:11
2. Kutokuwa na wajibu Yohana 15:16
3. Kutoshiriki katika kanisa zaidi ya kuongeza idadi Rumi 12,13,14, 1
Korintho 12-14
4. Kukosa maarifa ya kutofautisha mema na mabaya 1Korintho 13:11,
Ebrania 5:13-14
5. Kuyumbishwa Efeso 4:14
Sababu za uchanga kiroho: Ebrania 6:7-8
1. Hawajazaliwa mara ya pili
2. Kutokujali
3. Kutokutii (kiburi)
4. Kuruhusu mambo ya dunia kutawala
Maswali ya mjadala:
1. Ni mambo ya aina gani tuna hitaji kuyaondoa katika maisha yetu ili tuweze
kuufikia mwamba ambao ni Yesu? Je, uko tayari kufanya hili kwa msaada
wa Roho mtakatifu?
2. Kwa nini mafanikio, michezo, falsafa, mapokeo, hekima za wanadamu na
dini si misingi sahihi ya kujengea maisha yako hata kwa sehemu ndogo tu?
3. Ni mambo ya aina gani tunahitaji kuyaondoa katika maisha yetu ili tuweze
kujenga juu ya mwamba? Ili mafuriko na dhoruba zikija nyumba zetu
zisiangamie?
1
UANAFUNZI
Yesu anapo-okoa mtu anamwita kuwa mwanafunzi siyo muumini au mshirika au
mfuasi wake. Hatukuitwa kuwa wafuasi wa Yesu bali wnafunzi wa Yesu.
1.
2.
3.
4.
5.
6.
Mwanafunzi ni nini?
Mwanafunzi ni nani?
Sifa za mwanafunzi ni zipi?
Gharama za uanafunzi
Matokeo ya uanafunzi
Wajibu wa mwanafunzi
Maswali:
1. Nini tofauti kati ya mwanafunzi na mfuasi?
2. Nini tofauti kati ya neno mwanafunzi lilivyotumiwa wakati wa Biblia na
tunavyolitumia leo? Je kuna athari yoyote?
3. Je mimi ni mwanafunzi? Toa maelezo kuthibitisha jibu lako
4. kuna tofauti gani kati ya wanafunzi wa kwanza wa Yesu na wanafunzi wa
nyakati hizi? Unafikiri hili linasababishwa na nini?
5. Je yawezekana kuwa mshiriki na hata mhudumu wa injili bila kuwa
mwanafunzi?
6. Je yawezekana kutimiza agizo kuu la Yesu bila kuwa mwanafunzi?
Mwanafunzi ni nini?
Mathetes ni neno la kiyunani lililotafsiriwa mwanafunzi katika biblia. Neno
hili lilikuwa likitumiwa kumaanisha mtu aliyeamua kwa hiari yake kujifunza
jambo au shughuli Fulani toka kwa mtu mwingine ambaye alikuwa akiifahamu
shughuli au jambo ambalo mtu huyu alitaka kujifunza. Mafunzo haya yalikuwa
ni ya vitendo na yalimlazimisha mwanafunzi huyu kuhamia nyumbani kwa
mwalimu wake ili ajifunze si shughuli ile tu bali na mfumo mzima wa maisha ya
mwalimu wake kwani baada ya kuhitimu mwanafunzi huyu alitazamiwa kuwa
kielelezo cha mafundisho na maisha ya mwalimu wake, yaani alitazamiwa kuishi
kama mwalimu wake alivyoishi na kutencda kama mwalimu wake.
“mwnafunzi hamzidi mwalimu wake lakini akihitimu huwa kama mwalimu
wake”
Mjadala:
1. Mwanafunzi ni nani basi?
2. Sifa za mwanafunzi ni zipi?
1
Gharama za uanafunzi:
Filipi 3: 7-8.
Mathayo 13: 44-46.
Mathayo 8: 18-22.
Luka 9: 57-60.
2 korintho 8:9.
Luka 9: 23-24.
Galatia 6: 14 -17.
Matokeo ya uanafunzi:
1. Kukua kiroho (je kuna kukomaa kiroho?)
2. Huduma
3. Vipawa na karama
4. matunda
5. Toba
6. Huduma
7. Roho mtakatifu.
Wajibu wa mwanafunzi:
Mathayo 28 18-20
Mathayo 10: 5-15
Marko 16:16
Matendo 1:8-
1
KUTUBIA KAZI ZISIZO NA UHAI.
Waebrania 6 :1
Yohana 14 : 23 -24
Yohana 16 – 13 – 15
Waefeso 2 : 10
Wito wa kwanza kwa mwenye dhambi ni kutubu, wito wa kwanza kwa mkristo
ni kutubia kazi zisizo na uhai.
TOBA NI NINI?
Ni mabadiliko ya mtazamo na mwenendo yanayoleta mabadiliko ya
matendo na tabia. (2 nyakati 7: 14).
Finney alisema “toba inamaanisha uamuzi wa akili na moyo kuachana na
upinzani wowote ule na Mungu katika kila jambo. Hii ina maana kwamba
kuamini Mungu ni sahihi na mwenye dhambi ana hatia kabisa, na kuacha kabisa
kutoa sababu na visingizio kwa ajili ya dhambi”
KAZI ZISIZO NA UHAI.
1. Kazi isiyo na uhai ni kitu chochote uanachokifanya ambacho
hakikuanzishwa na Mungu.
2. Kazi isiyo na uhai ni yoyote ile tuifanyayo isiyo na uhai wa Mungu ndani
yake.
3. Ni chochote kile tunacho kifanya kwa wakati usio sahihi,au tukiwa na
ajenda ya siri. Ni chochote kitokanacho na mawazo mazuri au ambacho
hakizai matunda.
Kuna aina mbili za kazi zisizo na uhai:
1. Lolote lile tulilolifanya kabla ya kuokoka
2. Lolote lile tunalolifanya baada ya kuokoka ambalo Mungu hajatutuma
kulifanya. Ufunuo 3: 1 – 2, kutoka 2: 11 – 12.
Ni lazima kufuata mfano wa Yesu. Yohana 5 :19,30, 17: 16, 8:28, 14: 10.
Hatuna sababu yoyote ya kufanya kazi zisizo na uhai. Yohana 14 :16, 16: 13- 14.
Maswali ya kujadili:
1. Je kuna kazi zisizo na uhai katika maisha yako?
2. Je, kuna maeneo katika maisha yako ambayo unafahamu Mungu hapendi
yawe hivyo yalivyo? Unafanya nini nayo?
1
IMANI KWA MUNGU.
Waebrania 11: 1 – 3, 6.
Warumi 10 :17
Mathayo 17 : 20
Warumi 1 : 17.
Imani katika muktadha wa somo letu hapa ina maana ya “kuwa na hakika,
usalama, uthabiti katika mwingine na maneno yake’. Kuwa na Imani kwa
Mungu kuna kuhusisha kuhamisha tumaini na tegemeo lako kutoka kwako na
kuwa kwa Mungu.
Imani kwa Mungu ina kua kwa namna gani?
1. Kwa kuwa na mtazamo sahihi. Wafilipi 2 : 5 – 8.
2. Kwa kutambua kwamba imani ni kitu halisi. Ebrania 11 : 1, hesabu 23 : 19.
3. Kwa kutambua kwamba imani ni zawadi kutoka kwa Mungu. Waefeso 2:8.
4. Imani ina endelea kwa kadri tunavyo mfahamu Mungu. Kumbu 7: 9,
Zaburi 9 : 10, 1 thesalonike 5 :24.
5. Imani ni matokeo ya kuwa msikivu na mtendaji wa neno. Warumi 10:7,
mathayo 17 : 20.
6. Imani inakuja kwa kupata uzoefu wa yale ambayo Mungu anakutendea.
Yohana 2 : 11, Yohana 11:15.
7. Imani inakua kwa kadri tunavyo ukumbuka uaminifu wake.
Imani siyo mtazamo wa kimawazo wa kibinadamu katika kukabili matatizo.
1. Ni asili ya Mungu mwenyewe. Ebrania 11 : 3.
2. Imani kwa Mungu ni mfumo wa maisha ya mkristo aliyezaliwa mara ya
pili.
Maswali ya kujadili.
1. Kwanini chochote kisicho tokana au kufanywa kwa imani kimekufa?
2. Nini maana ya maandiko haya “ tunaishi kwa imani siyo kwa kuona”( 2
kor 5 : 7)
3. Imani yaweza kujidhihirisha?(Galatia 5:6).
1
MAFUNDISHO YA MABATIZO.
Waebrania 6 : 1- 2
1 kor 12 : 12 – 14
Mathayo 28 : 19
Luka 11 : 13
Mathayo 3 : 11 – 12
Kuna aina nne za ubatizo ambazo wakristo wanapaswa kubatizwa.
1. Ubatizo kwa Roho mmoja katika mwili mmoja -- Nafasi
2. Ubatizo wa maji
-- ushahidi hadharani
3. Ubatizo katika roho mtakatifu
-- uwezo
4. Ubatizo wa moto
-- utakaso
Ubatizo katika mwili mmoja.
Huu ni ubatizo ambao wakristo wote ni laziima waupate ama sivyo siyo wakristo.
1 kor 12 :12 – 14, Efeso 4 : 4 – 5.
Aina nyinginezo za ubatizo ni fahari ya mkristo ambayo kristo aliinunua kwa
damu yake
Twaweza kwenda mbinguni bila kuwa na aina nyingine za ubatizo lakini ni
lazima kupata ubatizo huu ili kurithi uzima wa milele.
Bila ubatizo huu aina nyingine za ubatizo hazina maana yoyote.
Ubatizo huu una ondoa tofauti ziwazo zozote zile kati ya wakristo wa madhehebu
na mahali, tamaduni za aina mbalimbali.
Ubatizo katika Roho Mtakatifu
Si kwamba Mungu anatupa nafasi katika mwili wa kristo tu bali pia anatupatia
uwezo wa kuishi katika nafasi hiyo.
Yohana 1 : 33, Matendo 1 : 8, Efeso 5 : 18, Matendo 2 : 14, Matendo 4 : 31 – 33.
Ili kubatizwa au kujazwa na Roho mt. tunapaswa kuwa na mioyo safi, kutubu
dhambi, kuwasamehe wengine. 1 Yohana 1 7 – 7, luka 6 : 37 – 38.
Ubatizo wa Roho mt. hutolewa kwa wale wanaoutamani na kuutafuta kwa imani,
Galatia 3 : 2 – 5,
Ubatizo huu si wa kusotea na kutafuta kwa kujidhili na kujitesa, ni zawadi ya bure
kutoka kwa Mungu. Luka 11 ; 11 – 13..
Ubatizo wa maji :
Mathayo 28 : 18 – 19
Yesu aliagiza wale wote watakao mwamini wabatizwe.
Ubatizo maana yake ni:
Ishara au dalili au tendo linaloonyesha kwamba mhusika ameamua kwa hiari
yake mwenyewe baada ya kusikia, kujifunza na kutafakari bila kushawishiwa
1
kumfuata Yesu na anatangaza kwa ulimwengu kwamba sasa yeye ni mwanafunzi
wa Kristo.
Tendo hili hufanywa na mtu ambaye amesikia neno la Mungu, ameliamini na
kisha kutubu dhanbi na kukiri kuwa Yesu kristo ni b wana na ya kwamba alikufa
kwa ajili ya dhambi zake na kufufuka kutoka kwa wafu.
Marko 16 : 16, Matendo 2 : 38.
Tendo la kuzama majini na kuibuka tena wakati wa ubatizo ni picha inayoonyesha
yale yanayotokea kwa mwamini:
Alikufa … nilikufa pamoja naye Rumi 6 : 6 – 7.
Ubatizo una ashiria kuifia dhambi. Tu wafu kwa habari ya dhambi. 2 kor 5 : 17,
rumi 8 : 10.
ii.
Alizikwa … Nilizikwa pamoja naye Rumi 6 : 3 – 4
Ubatizo ni kwa wale walioifia dhambi tu.waliotubu na kuziacha dhambi.
Wakolosai 2 : 12, 1 Petro 3 : 21, Wagalatia 3 : 27.
iii.
Alifufuka …. Ninao uzima mpya Rumi 6 : 4 – 5
wakolosai 3 : 1 – 4.
iv. Alipaa … Nilipaa pamoja naye Efeso 2 : 6
Hitimisho
Rumi 6 : 8 – 11
Katika ubatizo tuna watangazia watu na ulimwengu wote kwamba sisi tu viumbe
vipya tukiwa mali ya ufalme wa Mungu.
Maswali ya kujadili
Je unajisikia kama sehemu ya mwili wa kristo duniani kote?
Je unafahamu kristo anataka uwe wapi katika mwili wake na nini anachotaka
ukifanye? Kama ni ndiyo je waridhika na nafasi hiyo?
Bila kujali kama umebatizwa kwa maji au la, je waishi maisha yanayoonyesha kile
ambacho ubatizo huo umekusudiwa? (Galatia 2 : 20)
1
KUWEKEA MIKONO
Waebrania 6 : 1 – 2
1 Timotheo 5 : 22
Marko 16 : 17 – 18
2 Timotheo 1 : 6.
Wito wa Roho mtakatifu kwetu ni kututaka sisi tukue na kufikia cheo cha kimo
cha kristo. Ili hili liweze kutokea ni lazima msingi wa maisha yetu ya kiroho uwe
umejengwa ipasavyo.
Fundisho hili la kuwekea mikono ni mwendelezo kutoka kwa yale yaliyotangulia
na linatuchukua kutoka katika kujiangalia wenyewe na kuanza kuwaangalia
wengine tukiwa kama vyombo vya baraka vya kristo.
Kuwekea mikono nini?
Ni kitendo cha mtu kumwekea mtu mwingine mikono yake akiwa na lengo
maalum lenye makusudi ya kiroho.
Sababu za kuwekea mikono:
Kuleta uponyaji. Luka 4:40, luka 13 : 13, yakobo 5 : 14 – 16, matendo 9 : 17, matendo
28 : 8 – 9, marko 16 : 17 -18.
Kutoa baraka. Mathayo 19 : 13, marko 10 : 13 – 16, ufunuo 1 : 17.
Kuleta ubatizo wa Roho mtakatifu. Matendo 8 : 14 – 24, matendo 9 : 10 – 17,
matendo 19 : 6.
Kuleta karama za roho. 1 timotheo 4 : 14, 2 timotheo 1 : 6, rumi 1 : 11.
Kuwaweka watu wakfu kwa ajili ya kazi. Matendo 13 : 2 – 3, matendo 6 : 1 – 6.
Lazima uangalifu uwepo katika kuwekea watu mikono. 1 Timotheo 5 : 22
Umuhimu wake katika kanisa.
Kwa ajili ya huduma. Marko 10 : 43 – 45. Kutumia mikono yetu inaweza kuwa njia
mojawapo ya kuonyesha huduma zetu kwa watu wengine.
Kwa ajili ya kutoa. Luka 6 : 38, matendo 3:6. Tunapowekea mikono tunatoa uzima
wa Mungu ulio ndani yetu kwa watu wengine.
Kutia nguvu wito. Matendo 13 : 1 – 3
Kuwekea mikono ni sehemu ya mwili unaofanya kazi ipasavyo. Tukichukua
uzima kutoka kwa Yesu na kuwapatia wengine kupitia kuwekea mikono.
1
Maswali ya kujadili:
1. Je tuwe na hofu kwamba twaweza kupata kitu kisicho sawa kwa
kuwekewa mikono na watu wengine na hivyo tuepuke kuwekewa
mikono? Jadili.
2. Je waamini Mungu aweza kukutumia kuwapa watu wengine uzima?
1
UFUFUO WA WAFU
Yohana 5 : 19 – 30
1 kor 15 : 1 – 58
Rumi 6 : 1 – 14
Ufunuo 11 : 18
1 Thesalonike 4 : 13 – 5 : 11.
Ufufuo maana yake ni “kuinuliwa” au “kunyanyua juu”. Pia inamaanisha
kusababisha kusimama au kunyanyua juu, kuamsha kutoka usingizini na kutoka
kwa wafu.
Mifano ya mifano ya ufufuo katika biblia:
1 wafalme 17 : 17 – 24, 2 wafalme 4 : 32 – 35, 2 wafalme 13 : 21,marko 5 : 35
– 43, luka 7 : 11 – 17, yohana 11 : 1 – 45, matendo 9 : 36 – 42, matendo 20 : 9 – 12.
Kuna maeneo matatu ya ufufuo tunayopaswa kuya angalia
1. ufufuo wa Yesu ( wakati uliopita)
2. Ufufuo wa kiroho wa Waaminio ( wakati uliopo)
3. ufufuo wa mwisho wa wale wlio makaburini ( wakati ujao)
Ufufuo wa Yesu kristo.
Mathayo 28 : 6, Luka 24 : 36 – 53, Matendo 1 : 3.
Ufufuo wa Yesu kristo unatatuambia nini?
Mathayo 28 : 18, Efeso 1 : 17 – 23, Matendo 17 : 31, Rumi 1 : 4, Rumi 4 : 25,
Rumi : 8 – 9, Ebrania 10 : 12, 1 Petro 1 :3.
Ufufuo wa kiroho wa waaminio.
2 Kor 5 : 14 – 17, Galatia 2 : 19 – 20, Kolosai 2 : 12, Efeso 2 : 1,5 – 6.
Nini ushahidi wa ufufuo huu?
Uzima mpya. Rumi 6 : 4
Mtazamo mpya. Rumi 6 : 11
Bwana mpya. 2 Kor 5 : 15
Malengo mapya. Kolosai 3 : 1 – 4.
Ufufuo ujao utatokea lini?
Siku ya mwisho. Yohana 6 : 39 – 54.
Katika ufufuo wa siku ya mwisho. Yohana 11 : 20 – 23.
Atakapo kuja. 1 Kor 15 : 20 – 23.
Wakati wa tarumbeta ya mwisho. 1 Kor 15 : 51 – 52.
Bwana mwenyewe atakapokuja. 1 Thesalonike 4 : 16 – 17..
1
Ufufuo unapaswa kuleta matokeo gani katika maisha ya mkristo?
1. Kutuepusha na kufanya kama tunavyotaka wenyewe. 1 Kor 15 : 32 – 34.
2. Kumtumikia bwana. 1 Kor 15 : 58..
Waaminno watafufuliwa.
1. Kwa uzima wa milele. Danieli 12 : 2 – 3.
2. Wakiwa na mwili kama wa kristo. Rumi 6 : 5, Filipi 3 : 20 – 21, 1 Yohana 3 :
2.
3. Wakiwa na mwili sawa na mapenzi ya Mungu.. 1 Kor 15 : 38.
4. 1 kor 15 : 42, 1 Kor 15 : 43a, 1 kor 15 : 44, Kolosai 3 : 4, Yohana 17 : 24, Ufunuo
20 : 6, Zaburi 17 : 15.
Ufufuo wa wale wote walio lala mauti.
Yohana 5 : 28 – 29.
Siku ya ufufuo ni siku ya malipo. Luka 14 : 12 – 14, Ufunuo 11 : 18, ufunuo 21 11 –
15.
Kiti cha hukumu cha kikristo
Kwanini kiti hiki?
Yeremia 32 : 14.
Ili kutoa hesabu ya matendo yetu
Ili kupewa thawabu. 1 Kor 3 : 10 – 15, Danieli 12 : 3, 1 kor 9 : 24 – 25, 2Timotheo 4
: 7 – 8, Yakobo 1 : 12, 1Petro 5 : 1 – 4.
Maswali ya kujadili:
1. Je unao ushahidi wowote wa ufufuo wa kiroho katika maisha yako?
2. Je, tumtumikie BWANA kwa sababu tutapewa thawabu?
3. kama matendo yetu yote yatawekwa dhahiri siku ya hukumu, kwanini
wakristo wengi bado wanaishi maisha ya unafiki?
4. je tutapaswa kutoa hesabu ya yale yote tunayofanya hapa duniani hata
kama ni wanafunzi wa Yesu? Je hili linaleta tofauti gani katika maisha yetu?
1
HUKUMU YA MILELE
Waebrania 6 : 1 – 2
Rumi 2 : 5 – 11
Mathayo 25 : 31 – 46
2Petro 3 : 3 – 15
Waebrania 10 : 24 – 39
Mathayo 24 : 1 – 51
Hukumu maana yake nini?
Maana yake ni “kutenga”, “kutofautisha kati ya ..” “kumfanya mhusika kutoa
hesabu ya..” “ kuhoji” n.k.
Majina mengine ya hukumu ya milele: Malaki 4 : 5, Rumi 2 : 5, 2Petro 3 : 7,
Ufufunuo 6 : 16 – 17.
Hukumu ya milele ni jambo la hakika wala siyo la kubahatisha au kudhaniwa.
Matendo 17 : 30 – 31, Isaya 45 : 23 – 24.
Watakao husika ni wale wote wasio sehemu ya ufalme wa Mungu. Ufunuo 21 : 8,
luka 16 : 19 – 31.
Matokeo ya hukumu hii yatakuwa ni ya kutisha sana. Isaya 2 : 19, Ufufunuo 6 : 16
– 17, Ebrania 10 : 31.
Hukumu ya milele ni nini?
1. Kutupwa katika ziwa la moto
2. Kuwa katika kundi moja na shetani na malaika wake
3. Kuwa katika giza na kulia na kusaga meno
4. Aibu na kudharauliwa milele
5. Mauti ya pili
6. Kutengwa milele ne Mungu.
Mathayo 18 : 8 – 9, Mathayo 25 : 41, Mathayo 25 : 46, Mathyo 25 : 30,
Daniel 12 : 2, Ufufunuo 20 : 14 – 15, 2Thesalonike 1 : 9 – 10.
Kwnini kuwe na hukumu?
1. Kwa sababu ya dhambi.
2. Kwa sababu ya uasi
3. Kwa sababu ya kutotenda haki
4. Kwa sababu ya kutokutii
5. Kwa sababu ya kutokuamini
6. Kwa sababu ya makosa
7. Kwa sababu ya matendo maovu
Rumi 2 ; 12, 2Petro 2 : 9, Yuda 6, Yohana 3 : 18, Rumi 5 : 18, Yohana
3 : 19.
Hakimu ni nani?
1. Mungu. Matendo 17 : 31, Rumi 3 : 6, Ebrania 12 : 23, 1Petro 4 :5.
1
2.
3.
4.
5.
6.
Mwana. Yohana 5 : 22 – 27, Matendo 10 : 42.
Watakatifu. 1Kor 6 : 2 – 3.
Kanuni zipi zitatumika kutoa hukumu?
Kiasi cha nuru alichopata mtu. Mathayo 10 : 14 – 15, Mathayo 12 : 41.
Ufahamu usio na kikomo wa Mungu. Yohana 8 : 15 -16, Ufunuo 20 : 12,15,
Rumi 2 : 2.
7. Maneno ya Mungu. Yohana 12 : 48 -50.
8. Wajibu binafsi wa mtu. Rumi 14 : 10 – 12.
9. Mwenendo wa mtu. 2Kor 5: 10, Rumi 2 : 5 -6, 1Petro 1 : 17, Ufunuo 20 : 12.
1Petro 1 :17, Mathayo 25 : 31 – 46, Mathayo 12 :50, 2Thesalonike 1 : 5 – 10,
Rumi 2 : 12, Zaburi 9 : 8; 96:13; Matendo 17 : 31, Rumi 2 :5, 2Timotheo 4 : 8,
Ufunuo 19 : 11, 1Kor 4 : 5, Rumi 2 : 16, 2Thesalonike 1 : 8.
Hukumu hii itatokea lini?
Tayari imetokea:
1. Shetani. Yohana 16 : 11, Kolosai 2 :15.
2. Kwa ulimwengu. Yohana 12 :31.
3. Mwanadamu. Yohana 3:18;5:24, Rumi 5 : 9;8:1.
Inaendelea kutokea:
1. kwa wenye dhambi. Rumi 1 : 18 – 32.
2. Wakristo. 1 Kor 11 : 31 – 32
Itatokea wakati ujao
1. baada ya kifo. Ebrania 9 :27.
2. Siku ya mwisho. Yohana 12 : 48, Mathayo 10:15;11:22-24,12:36, Matendo 17
: 31,Rumi 2:5, 1Kor 3 :13, 2Thes 1:10,2Petro2:9;3:7,1Yohana4:17.
3. Kristo atakaporudi. Mathayo 25:31,1Kor4:5,2thes1:7-10,2Tim4:1,Yuda 14 –
15.
Itatokea wapi?
1. katika kiti cha enzi ya utukufu wake, kwa mataifa. Mathayo 25 : 31-46
2. katika kiti kikubwa cheupe. Ufunuo 20 : 11 – 15.
3. Katika kiti cha hukumu cha kristo, kwa wakristo. Rumi 14 : 10, 2Kor 5 : 10.
Nini kitatokea?
2Thes 1:8-9; Ufunuo 11:18, Mathayo 25:46, ufunuo 20:15
Maswali ya kujadili.
7. Kama Mungu ni wa upendo kwanini awahukumu watu kwenda kwenye
moto wa milele?
1
1
1
Download