RIPAMO & CO. ADVOCATES, P.O.BOX 1081, K.K.K.T BUILDING, GROUND FLOOR, ROOM NO. 06 INDIA STREET +255717192671/+255742949604 mosharp8@gmail.com 13th January, 2021 RPM/ADV/L. 10/2021 KATIBU MKUU KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA, DAYOSISI YA KASKAZINI KATI, S.L.P 519, ARUSHA. FAX: 2508039 Bwana Yesu Asifiwe, YAH: OMBI LA KUPANGISHIWA CHUMBA NAMBA 07 NA KUFANYA UBORESHAJI WA CHUMBA HICHO KWA KUWEKA MLANGO. Husika na mada tajwa hapo juu Sisi RIPAMO & CO. ADVOCATES ofisi ya sheria hapa Arusha, chumba namba 06 kwenye jengo la Kanisa (K.K.K.T) Dayosisi ya Kaskazini Kati sakafu ya kwanza; tunaleta ombi kwako na kamati yako teule kuhusu kupangishiwa chumba namba 07 iliyopo karibu kabisa na chumba chetu (chumba namba 06) kwa kuwa ofisi yetu imepanuka kwa uhitaji (chumba cha wakili mwandamizi, wakili msaidizi, katibu wa ofisi, sehemu ya kabati la vitabu, sehemu ya shelves ya nyaraka mbalimbali na majalada), chumba namba 06 imekuwa ndogo. Nasi tunapenda kuendelea kuwa wapangaji katika jengo hili zuri. Kutokana na uhitaji huo wa kuwa na sehemu kubwa zaidi tunaomba kupewa chumba hicho. Maombi yetu ya kupewa chumba namba 07 yanaambatana na ombi la kuweka mlango kati ya vyumba hivi viwili (06 na 07) ili kuunganisha ofisi yetu. Ikiwa ombi letu litakubaliwa tutafanya hivyo kwa garama zetu wenyewe pasipo kuhitaji kurudushiwa. Pia marekebisho hayo yatafanyika chini ya ushauri wa wataalamu wa ujenzi. Ni matumaini yetu kuwa ombi letu litapata kibali kwako; aidha tunatanguliza shukrani zetu Kwa niaba ya RIPAMO & CO. ADVOCATES Wako mwaminifu ………………………… RICHARD PATRICE MOSHA (WAKILI) RIPAMO & CO. ADVOCATES, P.O.BOX 1081, K.K.K.T BUILDING, GROUND FLOOR, ROOM NO. 06 INDIA STREET +255717192671/+255742949604 mosharp8@gmail.com