SEMINA ZA KULEA NA KUTUNZA WASHIRIKI (II) (Na Mch. Amosi Lutebekela, 2019) §Katika uwasilishaji huu kutahusika na: 1) Kitabu cha Karani wa Kanisa 2) Majukumu mengine ya karani wa kanisa (baadhi) 3) Kinga / Tiba kwa washiriki wasiojulikana walipo 4) Utunzaji wa kumbukumbu 5) Mikakati ya kuwalea waumini wapya 6) Kuwarejesha / Kuwarudisha washiriki waliopotea A. KITABU CHA KARANI WA KANISA §Ushauri umetolewa kwamba kitabu kilichoandaliwa na Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati ndicho kitumiwe katika kuorodhesha majina ya washiriki wa kanisa…. §Kitabu hiki kitunzwe katika sanduku au kabati lenye kufuli. §Mara kwa mara majina yakaguliwe na mkuu wa konferensi, au katibu wake, kuhakikisha kwamba idadi ya washiriki iliyo katika kitabu ni sawa na ile iliyotumwa konferensi. oMwongozo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Toleo la 19, sahihisho la 2015, UK.236. Kitabu cha Karani wa Kanisa §Muundo wa Kitabu cha Karani wa Kanisa: MAPOKEO--iwe kushoto, MAONDOLEO--iwe kulia. §KITABU CHA KARANI WA KANISA KINA SEHEMU KUU NNE: 1) WALIOINGIA (MAPOKEO) NA MAONDOLEO 2) MAHUDHURIO KATIKA MEZA YA BWANA 3) HABARI ZA BARAZA ZA KANISA 4) HABARI ZA MATENDO YA KANISA Kitabu cha Karani wa Kanisa 1. MAPOKEO NA MAONDOLEO oMAPOKEO, uingizaji wa majina kitabuni ---iwe kwa herufi kubwa (Mwongozo wa Kanisa, 2015, UK.236) oMAPOKEO. Kuna njia tatu za kuingia ushirika wa kanisa mahalia [i.Kwa Ubatizo, ii.Kwa Mikono, iii.Kwa Barua]. Kila muumini huingia ushirika wa kanisa mahalia kwa njia mojawapo ya hizo. oMAPOKEO. Kuna sehemu tatu za kujaza tarehe --(i)Baraza, (ii)Mashauri, (iii)Alivyoingia –[Kwa Ubatizo au Kwa Mikono au Kwa Barua] Kitabu cha Karani wa Kanisa oUandishi wa majina kwenye MAPOKEO ni kwa kadri mshiriki alivyoingia, si kwa alfabeti. oUandishi wa majina kwenye MAPOKEO ni majina kamili kwa herufi kubwa, vifupisho viepukwe. oUandishi wa majina kwenye MAPOKEO, kila mshiriki awe na namba ya ushirika. oTaarifa ya washiriki inapoandaliwa mwishoni mwa robo, ni vyema kuhakiki idadi halisi kwa fomula ifuatayo: MAPOKEO – MAONDOLEO = IDADI HALISI Kitabu cha Karani wa Kanisa oKila aliyebatizwa ni haki kupewa cheti cha ubatizo na kadi ya ushirika (Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.236) oKumpokea mshiriki kwa mikono (kukiri imani), uangalifu mkubwa unatakiwa (Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.56) vJina huandikwa katika Kitabu cha Karani wa Kanisa mara moja tu hadi kufungwa kwa kitabu mwishoni mwa muhula wa miaka mitano…. Kitabu cha Karani wa Kanisa §Kanisa linapopangwa, kanisa walikotoka hujaza Maondoleo kwa Barua; kanisa lililopangwa hujaza Mapokeo kwa Barua. §kanisa linapopangwa, kanisa wanakotoka tarehe huonekana maeneo matatu upande wa maondoleo (Baraza, Mashauri, Barua) §Kanisa linapopangwa, washiriki wa kanisa lililopangwa tarehe huonekana eneo moja tu – Mapokeo kwa Barua. § Kinachoandikwa kwenye njia mshiriki aliyopokelewa kanisani (kwa ubatizo au kwa mikono au kwa barua) ni tarehe siyo alama ya vema. Kitabu cha Karani wa Kanisa §MAONDOLEO. Kuna njia nne za maondoleo: i. Kwa Barua (kuhama), ii. Kwa Mauti, iii. Kwa Kuasi, iv. kwa Kutojulikana Aliko. §MAONDOLEO. Kuna sehemu tatu za kujaza tarehe: (i)Baraza, (ii)Mashauri, (iii)Alivyoondoka –[Kwa Barua (kuhama), au Kwa Kuasi, au kwa Kutojulikana Alipo ]. oMaondoleo kwa Barua, tarehe hujazwa baada ya kupata mrejesho toka kanisa alilohamia. oMaondoleo kwa Mauti, hakuna tarehe ya baraza wala mashauri; ni tarehe ya kifo tu. (Taz. (Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.61) Kitabu cha Karani wa Kanisa oKuondolewa kwa Kuasi, maelekezo katika Mwongozo wa Kanisa kuhusu Marudi ya Kanisa YAZINGATIWE. (Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, Sura ya 7). oKuondolewa kwa Kutojulikana Aliko, maelekezo katika Mwongozo wa Kanisa kuhusu muda wa kuwatafuta washiriki walioonekana kuwa hawajulikani waliko YAZINGATIWE. [Washiriki Wanaohama Bila Taarifa]. (Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.74). Kitabu cha Karani wa Kanisa §KUPOKELEWA au KUONDOLEWA kwa Mshiriki ni kwa kura ya kanisa tu au kwa kifo. o“Majina huingizwa au kuondolewa kwa kura ya kanisa tu au kwa kifo.” – Mwongozo wa kanisa,…2015, uk.61. qKitabu kipya cha karani wa kanisa kinapoandikwa mwanzoni mwa muhula wa miaka mitano, majina ya wote walioondolewa ushirika [kwa barua (kuhama), kwa mauti, kwa kuasi, kwa kutojulikana walipo], huachwa kwenye kitabu kilichofungwa. Kitabu cha Karani wa Kanisa ¨Kila mshiriki aliyepokelewa kanisani [Kwa Ubatizo au Kwa Mikono au Kwa Barua], kuwepo agenda na miniti kwenye vikao viwili – Baraza la Kanisa na Mashauri ya Kanisa (Mkutano Mkuu wa Kanisa). ¨Kila mshiriki aliyeondolewa ushirika [Kwa Barua au Kwa Kuasi au Kwa Kutojulikana Aliko], kuwepo agenda na miniti kwenye vikao viwili – Baraza la Kanisa na Mashauri ya Kanisa (Mkutano Mkuu wa Kanisa). § Kinachoandikwa kwenye njia mshiriki aliyoondolewa ushirika (kwa barua au kwa mauti au kwa kuasi au kwa kutojulikana aliko) ni tarehe siyo alama ya vema. Kitabu cha Karani wa Kanisa ¨USHIRIKA WAKATI WA UHAMISHO §“Kwa hali yo yote ile, karani wa kanisa analotokea mshiriki,hataliondoa jina la mshiriki katika kumbukumbu za washiriki mpaka ipokelewe sehemu ya barua ya uhamisho inayothibitisha kuwa mshiriki huyo amepokelewa katika ushirika wa kanisa analohamia. §Karani, wazee, mchungaji na mwenyekiti wa konferensi wote wanawajibika kuhakikisha kuwa makanisa yote yanafuata utaratibu huu.” § Mwongozo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.59. Kitabu cha Karani wa Kanisa o“Mara kwa mara washiriki waelekezwe wajibu wao wa kuhakikisha kwamba ushirika wao uko katika kanisa la mahali wanapoishi. Maelezo ya kuhamisha washiriki yaliyomo katika mwongozo huu yazingatiwe sana. • Inawapasa makarani wa kanisa kuhakikisha kwamba maombi ya uhamisho yanafanywa upesi.” (Mwongozo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.241). §“Mshiriki akiondolewa katika ushirika wa kanisa kwa kura ya kanisa, karani wa kanisa atamwarifu kwa kumwandikia barua.” (Mwongozo wa Kanisa, 2015, uk.236). [Tazama pia uk. 75]. Kitabu cha Karani wa Kanisa 2. MAHUDHURIO KATIKA MEZA YA BWANA oOrodha ya majina iwe sawa na ya kwenye MAPOKEO…. oJina huandikwa mara moja tu kitabuni hadi kufungwa kwa kitabu mwishoni mwa muhula wa miaka mitano…. oZingatia ujazaji wa mahudhurio ya Meza ya Bwana kwa muhula husika… [mfano: 2016, 2017, 2018, 2019, 2020]; kila robo kwa wakati. oUjazaji: Weka alama ya vema kwenye kisanduku mbele ya jina kwa robo husika ya mwaka husika; usiweke tarehe. oAliyeshiriki Meza ya Bwana nje ya kanisa lenye ushirika wake, taarifa imfikie karani wake wa kanisa ili amjazie kumbukumbu. Kitabu cha Karani wa Kanisa 3. HABARI ZA BARAZA ZA KANISA oVipengele muhimu vya kukumbuka: i. Aina ya kikao: Baraza la Kanisa au Mkutano Mkuu wa kanisa; [Kikao cha Wazee,…kumbukumbu zake hazitunzwi katika kitabu hiki] ii. iii. iv. v. vi. Mahali kikao kilipofanyikia; Tarehe ya kikao; Waliohudhuria; Wasiohudhuria kwa taarifa; Wasiohudhuria bila taarifa; Kitabu cha Karani wa Kanisa oOmbi la ufunguzi na mwombaji oFungu la ufunguzi wa kikao na mnenaji oOmbi la kufunga na mwombaji oOrodha ya agenda …. oMuhutasari huandikwa kwa kifupi ---agenda na azimio… [soma zaidi Mwongozo wa Karani wa Kanisa] oAliyeomba ombi la kufunga…. oMwenyekiti wa kikao na Katibu wa kikao --- [Sahihi / Jina /Wadhifa / Tarehe] Kitabu cha Karani wa Kanisa ¨Kuhusu uandishi wa kumbukumbu za vikao: oKumbukumbu za vikao vya Baraza la Kanisa vyote, maalumu na vya dharura huandikwa katika kitabu hiki. oKumbukumbu za vikao vya Mkutano Mkuu wa Kanisa (Mashauri ya Kanisa) vyote, maalumu na vya dharura huandikwa katika kitabu hiki oUandishi wa Miniti za vikao kitabuni iwe kwa muhtasari kwa kadri inavyowezekana. oIkumbukwe kuwa kumbukumbu za vikao vya wazee haziandikwi kwenye Kitabu cha Karani wa Kanisa. Kitabu cha Karani wa Kanisa oKarani wa kanisa anashauriwa kuandika miniti katika kitabu cha karani wa kanisa mara baada ya kikao, ili kuepuka kusahau mpangilio mzuri wa muhtasari. §Mfano wa uandishi wa muhtasari wa baraza: • Mfano wa 1: • AGENDA: MWAKILISHI KATIKA MKUTANO MKUU WA KONFERENSI. oIliamuriwa: Kumchagua ndugu Philip Kiboko kuliwakilisha Kanisa katika mkutano mkuu wa Konferensi wa mwaka 2015. Kitabu cha Karani wa Kanisa Mfano wa 2: • AGENDA: KWAYA YA KANISA KWENDA KUREKODI oIliamriwa: Kuiruhusu kwaya ya kanisa kwenda Dar es Salaam kurekodi nyimbo katika Studio ya Morning Star Radio kati ya Januari 25-29 kwa gharama zao wenyewe. §Lakini yapo maamuzi ambayo kwa sababu ya uzito wake au kwa kuwa yanahitaji kuonesha kiini na sababu za kufikia maamuzi hayo, huwa inatakiwa kueleza kwa kifupi sababu zilizopelekea kufikia maamuzi hayo. Kitabu cha Karani wa Kanisa •Mfano wa 3: oKwa kuwa ndugu Machomane Tabia Mbaya amekiuka amri ya saba inayokataza uzinzi; na kwa kuwa kosa lake limekuwa la wazi na limeleta aibu kwa kanisa; na kwa kuwa taratibu zote za kumsaidia kwa mujibu wa Mathayo 18 zimefuatwa kikamilifu, Iliamuriwa: Kuondoa jina la Machomane Tabia Mbaya kwenye kitabu cha ushirika wa Kanisa. Kitabu cha Karani wa Kanisa 4. HABARI ZA MATENDO YA KANISA §Hapa, huorodheshwa wote walioondolewa ushirika [kwa barua, kwa mauti, kwa kuasi, kwa kutojulikana walipo]. §Zingatia kumbukumbu zifuatazo: oTarehe ya Baraza…. oNamba ya ushirika…. oJina la mshiriki…. oShauri na Tarehe yake…. oTendo la Kanisa….. • Kwa mauti, hakuna tarehe ya baraza, shauri, wala tendo. Kitabu cha Karani wa Kanisa oShauri na Tarehe yake. üShauri ni ile sababu iliyopelekea maondoleo; MFANO: i. Uzinzi / Uongo / Wizi / Kuvunja Sabato / Kukana Imani (N.k.) --- [ikiwa ndiyo sababu ya maondoleo]. ii. Uhamisho ---- [ikiwa ndiyo sababu ya maondoleo]. iii. Kutojulikana Aliko --- [ikiwa ndiyo sababu ya maondoleo]. üTarehe ni ile ambayo Mashauri ya Kanisa ilifanya mjadala na maamuzi juu ya shauri husika. Inaandikwa mbele ya shauri. oMshiriki akifa, hakuna shauri, maana hakuna mjadala; huandikwa Mauti na tarehe aliyokufa. Kitabu cha Karani wa Kanisa oTendo la Kanisa. üTendo ni uamuzi uliochukuliwa kwa kupiga kura, •MFANO: i. Kuondolewa ushirika wa kanisa ii. Kuhamisha ushirika wa kanisa iii. Kuondolewa ushirika wa kanisa oMshiriki akifa, hakuna tendo, maana hakuna kupiga kura; huandikwa tu Kifo B. MAJUKUMU MENGINE YA KARANI WA KANISA (baadhi) oHushughulikia uhamisho wa washiriki… (Mwongozo wa Kanisa, 2015, 57-62) • “Mara kwa mara washiriki waelekezwe wajibu wao wa kuhakikisha kwamba ushirika wao uko katika kanisa mahalia wanaposali. Maelezo ya kuhamisha washiriki yaliyomo katika Mwongozo wa Kanisa yazingatiwe.” – Mwongozo wa Kanisa, 2015, 241. • “Washiriki wanaohamia eneo jingine kwa zaidi ya miezi sita hawana budi kuomba barua ya uhamisho mara moja.” – Mwongozo wa Kanisa, 2015, uk.57. Majukumu Mengine ya Karani wa Kanisa oHujaza Fomu ya Miito ya Hudumu baada ya wahudumu wanaoitwa kupitishwa na baraza la kanisa….kisha kuiwasilisha Konferensi kwa wakati. oKuhesabu waliohudhuria ibada Sabato ya 2 na ya 7 ya robo oKujaza kwa ubora taarifa ya washiriki ya kila robo na kuiwasilisha kwa mchungaji kwa wakati… oKuwasiliana na washiriki wasiohudhuria kanisani…. (Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.94,211) oNa majukumu mengine kama yalivyoainishwa kwenye Mwongozo wa Kanisa na Mwongozo wa Karani wa Kanisa…. C. KINGA KWA WASHIRIKI WASIOJULIKANA WALIPO A. Jinsi ya kupunguza au kuondoa changamoto ya washiriki kutojulikana walipo? 1. Kutendea haki kazi ya baraza ya kupitia majina ya washiriki angalau mara moja kwa mwaka…(Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.155). 2. Kuweka utaratibu wa kuandika kumbukumbu pana za mshiriki, § MFANO: i. Jina (majina matatu)___________________ ii. Jinsia _______ Hali ya ndoa ____________ Kinga kwa Washiriki Wasiojulikana Walipo iii. Tarehe ya kuzaliwa ________________________ iv. Mahali alipozaliwa ________________________ v. Makazi / Mahali anapoishi ___________________ vi. Mahali pa kazi na kazi ______________________ vii. Namba ya simu ___________________________ viii. Anuani ya barua pepe _____________________ ix. Dini au dhehebu la awali ____________________ x. Jina la ndugu au jamaa ya karibu ______________ Kinga kwa Washiriki Wasiojulikana Walipo xi. Mawasiliano ya ndugu au jamaa ya karibu ______________ xii. Mahali anapoishi ndugu au jamaa ya karibu____________ xiii. Mshiriki wa SDA anayemfahamu ____________________ xiv. Mawasiliano ya mshiriki wa SDA anayemfahamu _______ xv. Tarehe na mahali alibatizwa ________________________ xvi. Jina la mchungaji aliyembatiza _____________________ 3. Washiriki wakumbushwe kuwa, mshiriki anapoondoka sehemu fulani ni juu yake kulitaarifu kanisa (mzee au karani wa kanisa lake) mahali pale atakapokuwa. Kinga kwa Washiriki Wasiojulikana Walipo o“Mshiriki anapohamia mahali pengine, inampasa karani wa kanisa lenye taarifa za ushirika wake kumwandikia katibu wa konferensi husika akiomba mchungaji wa eneo hili jipya amtembelee mshiriki huyo ili kufanikisha uhamisho wa ushirika wake…” o“Washiriki wanaohamia kwenye eneo lingine kwa zaidi ya miezi sita hawana budi kuomba barua ya uhamisho mara moja”. (Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.57). D. UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU (RECORD MANAGEMENT) §Utunzaji wa kumbukumbu (Record Management) ni suala muhimu sana kanisani kama ilivyo serikalini au katika jamii… i. Hufaa kuwa rejea mgogoro unapotokea… ii. Hufaa kuwa rejea kwa mfanya utafiti… §Zingatia: Kumbukumbu zinaongezeka ubora au thamani kwa kadri muda unavyoondelea…. Utunzaji wa Kumbukumbu ¨Karani Hutunza Kumbukumbu---(tazama: Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.94-95, 210). ¨“Karani huandika kumbukumbu za kanisa, ambazo hazina budi kuhifadhiwa vizuri.” (Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.94). ¨“Kumbukumbu za washiriki hazina budi kutunzwa kwa usahihi na kuboreshwa kila wakati ili kuonesha hali rasmi ya washiriki.” (Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.210). ¨Kitabu cha Karani wa Kanisa kitunzwe wapi? (Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.236). Utunzaji wa Kumbukumbu §Mahali gani zinatunzwa nyaraka za kanisa? 1) Nakala ya mauziano ya kiwanja cha kanisa… 2) Nakala ya hati miliki ya kiwanja cha kanisa… üUnunuzi wa viwanja vya kanisa, jina liandikwe la Trustee siyo la kanisa mahalia. Jina linaloandikwa ni: oTHE REGISTERED TRUSTEE OF SEVENTH-DAY ADVENTIST CHURCH OF TANZANIA • Na kwamba, manunuzi ya kiwanja cha kanisa au shamba, uongozi wa serikali wa eneo husika uhusishwe… Utunzaji wa Kumbukumbu 3) Cheti cha kuwekwa wakfu kanisa mahalia… 4) Historia ya kanisa mahalia….iwe endelevu…. 5) Barua mbalimbali toka au kwenda konferensi… 6) Barua mbalimbali toka au kwenda serikalini… 7) Nakala za barua za walioondolewa ushirika kwa marudi… 8) Taarifa mbalimbali ziendazo ngazi za juu za kanisa…. 9) Mpango mkakati wa kanisa mahalia ….. Utunzaji wa Kumbukumbu 10) Mchoro unaoonesha matumizi ya kiwanja cha kanisa – [Master Plan]. 11) Miongoni mwa kumbukumbu zipasazo kutunzwa kwa makini sana ni MUHTASARI ZA VIKAO – BARAZA LA KANISA NA MKUTANO MKUU WA KANISA. 12) Kila kanisa mahalia liwe na historia ya kanisa mahalia husika. Historia iwe endelevu, tangu kupangwa oNa kadhalika. ¨ZINGATIA: Wakati wa makabidhiano kwa uongozi mpya – kuwepo na orodha ya vinavyokabodhiwa kwa kiongozi mpya…. Utunzaji wa Kumbukumbu §Mahali gani zinatunzwa mali za kanisa? üVifaa vya Meza ya Bwana…. üKitabu cha orodha ya vifaa vya kanisa… üMiongozo ya kanisa na miongozo ya idara …. üVitabu vya taarifa…. üVifaa vya idara ya vijana… üVifaa vya idara ya watoto… üNa kadhalika. Utunzaji wa Kumbukumbu §Kila kanisa mahalia liwe na chumba maalumu chenye kabati la kutunzia vifaa vya kanisa na nyaraka za kanisa. §kila kanisa mahalia liwe na ofisi za kanisa ---- ofisi ya mchungaji, ofisi ya karani wa kanisa, ofisi ya wazee wa kanisa, ofisi ya mashemasi, ofisi ya mhazini, n.k. §Kila kanisa mahalia limwezeshe karani wa kanisa kuwa na faili mbalimbali za kutosha kutunzia nyaraka mbalimbali za kanisa. Utunzaji wa Kumbukumbu §Kila kanisa mahalia, kwa kadri inavyowezekana, liwe na kompyuta kwa ajili ya ofisi ya karani wa kanisa kutumia, pamoja na kuweka kumbukumbu ‘kidigitari’…. §Kumbukumbu za Orodha ya Washiriki zinapowekwa kidigitali, mpangilio uliowekwa na Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati uzingatiwe. §Kila karani wa kanisa mahalia awe na uwezo wa kuwasajili washiriki wa kanisa lake kwenye mfumo wa kanisa – ACMS (Adventist Church Management System). Utunzaji wa Kumbukumbu §Kuwe na uangalifu mkubwa katika kuchagua au kutengeneza mahali salama pa kutunzia mali na nyaraka za kanisa… §Kila kanisa mahalia liwe na utaratibu wa namna ya kutunza kumbukumbu za muda mrefu (archive)– ‘hard’ & ‘soft’. vIkiwa, kwa sababu fulani, imelazimu Kitabu cha Karani wa Kanisa au nyaraka / vifaa vya kanisa kutunzwa kwa mtu binafsi badala ya ofisi ya kanisa, kuwepo ridhaa ya kanisa kupitia vikao vyake. §KUMBUKA: §“Sehemu kubwa ya ufanisi wa shughuli za kanisa hutegemea karani. Kutokana na umuhimu na upekee wa majukumu ya ofisi hii, ni vyema kuchagua mtu ambaye anaweza kuchaguliwa tena ili kuwe na mwendelezo katika uhifadhi na utoaji wa taarifa.” – Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19, sahihisho la 2015, uk.93. §Karani wa kanisa ni miongoni mwa maofisa wa kanisa mahalia wanaofanya kazi kwa karibu sana na wazee wa kanisa na mchungaji. §Karani wa kanisa, ili afanye kazi yake kwa ufanisi, anatarajiwa: 1. Ajitoe kikamilifu 2. Awe makini katika utendaji wake 3. Awe mwaminifu na mwadilifu 4. Awe tayari kutumika 5. Awe mwenye kumbukumbu nzuri/asiwe msahaulifu 6. Awe mfuatiliaji mzuri wa maamuzi 7. Awe anayependa kushirikiana na wengine 8. Awe mtunza siri. §UJUMBE MUHIMU KWA KARANI WA KANISA: • “Aandamaye haki na Fadhili, Ataona uhai na haki na heshima.” (Mit.21:21) • “Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.” (Mit.18:10) E. MIKAKATI YA KUWALEA WAUMINI WAPYA ¨Mshiriki mpya ni mtoto mchanga aliyezaliwa katika familia ya kanisa; hivyo, 1) Asiachwe kujitafutia chakula yeye mwenyewe… 2) Asiachwe kujivalisha nepi/pampasi yeye mwenyewe …. 3) Asiachwe kujitengenezea mfumo wa maisha… §Vile tuwafanyiavyo watoto wanaozaliwa katika familia zetu, hali kadhalika katika familia ya Mungu… §Baada ya kuwabatizwa, waumini wapya wafundishwe kuyashika yote Yesu aliyoyaamuru (Mt.28:18-20) Kuwalea Waumini Wapya §Ufundishaji wa waumini wapya uzingatie, oKuwaanzishia chakula chepesi kabla ya kigumu – 1Kor.3:2; Ebr.5:13; 1Pet.2:2. oWaumini wapya wakuzwe katika mafundisho ya Imani za Msingi za Waadventista wa Sabato. Wafundishwe mfumo wa kanisa sambamba na Imani za Msingi. oWaumini wapya wafundishwe Viwango vya Maisha ya Kikristo …. (Rum.12:1-2) [Taz. Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, Sura ya 12.] oWaumini wapya wafundishwe Karama za Roho na Huduma…. Kuwalea Waumini Wapya oWaumini wapya wafundishwe namna ya kumshuhudia Yesu, kuhudumu kanisani, mahusiano…, uchumi…,… oWaumini wapya wasajiliwe katika idara na vyama kanisani… oWaumini wapya wafundishwe kumtegemea Mungu nyakati zote – za raha na za shida… oHadi hapa, sasa waumini wapya wanaweza kufundishwa masomo ya unabii wa Biblia…. (2Pet.1:19) oSasa si watoto wadogo tena bali ni watu wazima katika Kristo, ambao wameyabatilisha mambo ya kitoto… (1Kor.13:11) Kuwalea Waumini Wapya ¨Katika hili, uongozi wa kanisa unatazamiwa: 1) Kuwaimarisha waumini wapya katika imani na ushirika… Kuwapa mafunzo juu ya maisha ya Kikristo… {Mchungaji + Wazee wa Kanisa} …. 2) Kuwatumia washiriki wa zamani kuwasaidia washiriki wapya kukua …. Urafiki na kutumia karama zao za kiroho kulea na kuimarisha wachanga… Kuwa kielelezo katika tabia/mwenendo 3) Kuhusisha idara za kanisa katika kulea --- Hasa: (i) Huduma za Wanawake (AWM), (ii) Chama cha Wanaume Waadventista (AMO), (iii) Huduma za Vijana Waadventista, (iv) Huduma za Watoto. ü Hii ni kwa sababu washiriki wa kanisa ni wanaume au wanawake au vijana au watoto. Kuwalea Waumini Wapya 4) Kuwahusisha waumini wapya katika shughuli na programu za kanisa…. Huduma za ibada, Kujifunza Biblia, Kwaya ya kanisa, Kushuhudia, na Ushirika, … o Kwa kuhusishwa, waumini wapya huweza kukuza mahusiano na kugundua na kutumia karama za Roho. 5) Kuwasajili katika vikundi vidogo… Mf. Vikosi vya Shule ya Sabato; Vikosi vya kujifunza Biblia, vikosi vya kushuhudia, vikosi vya kusaidia, vikosi vya maombi, n.k. o Mpango huu ulikuwa sababu ya kukua haraka kwa kanisa la mitume… Kuwalea Waumini Wapya vMoja ya jambo muhimu kwa vikosi vidogo vya nyumbani--hukuza ushirika wa kina miongoni mwa washiriki / waumini. 6) Kuwatembelea nyumbani …. Kuomba nao, kujifunza nao, kuwashauri, na kuwatia moyo…. qMuumini mpya anaweza kuwa na mapungufu kama ilivyo kwa mtoto katika familia…AFUNDISHWE… AVUMILIWE….ASAIDIWE KUKUA…. oYohana 21:15-17 “…wana-kondoo…” F. KUWARUDISHA WASHIRIKI WALIOPOTEA KUWARUDISHA WASHIRIKI WALIOPOTEA §Suala la kumrejesha mshiriki aliyepotea ni: •Agenda ya Yesu mwenyewe…. Luka 15:3-7; 19:10. •Agizo la Mungu la enzi zote…...Eze.3:17-21. §Tafakari mazingira ya kondoo aliyepotea na mtafutaji (Luka 15:3-7): oMtafutaji alikuwa mwenye huruma kwa kondoo aliyepotea. Kuwarudisha Washiriki Waliopotea oHakumshutumu kwa upotevu wala hakumgombeza oAlipompata, alimkumbatia kwa upendo mwingi…., na kufurahi na wote…(taz. Luka 15:5-6, 7) §Yesu akitoa mfano wa kondoo aliyepotea na moyo wa mtafutaji, alitoa kielelezo juu ya: oKile alichofanya kwa jamii ya mwanadamu ….. Filp.2:5-8…. oKile kanisa na kila muumini twapaswa kufanya kwa mshiriki aliyetanga mbali kimaadili…Eze.3:17-21 Kuwarudisha Washiriki Waliopotea oMungu ndiye alifanya juhudi ya kumtafuta Adamu baada ya dhambi kumtenga na Mungu -- Adamu, uko wapi?...Mwa.3:9. §Tafakari juu ya moyo wa baba wa mwana mpotevu aliporudi nyumbani – Lk.15:20-24. 1) Hakumgombeza wala kumshutumu …. 2) Alimhurumia …. 3) Alimhudumia kwa upendo…. oNdivyo itupasavyo kuwatendea washiriki walioliacha kanisa wanaporejea kanisani. Kuwarudisha Washiriki Waliopotea ¨Ziko sababu zinazofanya washiriki kupoa kiroho/kurudi nyuma/kupotea; (taz. Mwongozo wa Mzee, 136). §Ili kuwarejesha; kwanza watambue, kisha watembelee. oHapa ni mashauri saba kuongoza safari yako: 1) Uliza maswali kwa busara…. 2) Sikiliza kwa makini tena kwa maombi majibu wanayoyatoa…. Kuwarudisha Washiriki Waliopotea 3) Usilalie upande wo wote katika maongezi yako…. 4) Heshimu usiri…. 5) Waombee…. 6) Waalike warejee kanisani… 7) Uwapende…. F1. BAADHI YA SABABU ZA BAADHI YA WASHIRIKI KUASI 1. Malezi hafifu kwa washiriki wapya: • Chakula hafifu cha kiroho i.e. mahubiri na mafundisho yasiyolenga mahitaji au yasiyoandaliwa vyema. • Kutopata joto (urafiki)toka kwa washiriki wa zamani. • Kutotembelewa na kutiwa moyo. • Kutoshirikishwa katika programu mbalimbali ndani ya kanisa. Baadhi ya Sababu za Baadhi ya Washiriki Kuasi 2. Baadhi ya watu kujiunga na kanisa kwa matarajio mbalimbali, tofauti na kumfuta Yesu…. 3. Kutokuwepo na ratiba nzuri ya viongozi wa kanisa kutembelea washiriki…. 4. Washiriki kutojihusisha na jukumu la kumshuhudia Yesu… Baadhi ya Sababu za Baadhi ya Washiriki Kuasi 5. Kwa nini baadhi ya vijana huliacha kanisa… oKutotembelewa na kutiwa moyo…. oKutoshirikishwa katika programu mbalimbali ndani ya kanisa… au Huduma zao kutothaminiwa…. oKutowapatia semina/masomo maalumu kulingana na rika zao… oKukumbwa na shinikizo rika…. oKutotiwa moyo katika kukabili changamoto za ujana… Baadhi ya Sababu za Baadhi ya Washiriki Kuasi 6. Matatizo ya kiutamaduni na kijamii, oMfano: i. Ndoa kuvunjika….au kuwa na migogoro isiyo na ufumbuzi… ii. Kufiwa, au kuuguza muda mrefu bila kuona joto la kanisa…. iii. Uchumi kuporomoka…. iv. Ndoa na mwenye imani tofauti…, • Na kadhalika…. Baadhi ya Sababu za Baadhi ya Washiriki Kuasi 7. Kukosekana au kupungua kwa ibada katika familia…. 8. Kuchelewa kushughulikia dhambi za wazi… 9. Kushughulika na masumbufu ya maisha haya na kukosa muda kwa mambo ya milele... 10. Upendo kupoa miongoni mwa washiriki… hivyo ubaguzi – kikabila, kiuchumi, kielimu, kijinsia, kirika, n.k. 11. Mahusiano hafifu katika ndoa …. makwazo… 12. Hali ngumu ya kiuchumi hupelekea baadhi ya washiriki kufanya kazi na siku ya Sabato, wengine kuliacha kanisa. Baadhi ya Sababu za Baadhi ya Washiriki Kuasi 13. Matatizo ya kiutawala kanisani…. 14. Kutokukubaliana na Kanuni za Kanisa katika masuala fulani… 15. Washiriki kutokuwa wachunguzi wa Maandiko Matakatifu, hivyo kutegemea tu kile asemacho mhubiri. Akipotosha andiko, nao hupotoshwa…. 16. Ushuhuda wa mwenendo mbaya ambao washiriki wapya huupokea (kuuona) kutoka kwa washiriki wa zamani. Baadhi ya Sababu za Baadhi ya Washiriki Kuasi 17. Manung’uniko/makwazo tokana na utendaji unaokinzana na taratibu na mfumo wa kanisa…. Mfano: o upotevu wa fedha za kanisa, o washiriki kutopewa taarifa ya mapato na matumizi, o viongozi kutotunza siri za waumini, o dhambi miongoni mwa viongozi, o ubaguzi katika kuhudumia washiriki wakati wa mahitaji, o masengenyo/umbea/masingizio, o kiongozi au mhubiri kunena kwa kuaibisha/kudhalilisha muumini au mgeni. F2. NAMNA YA KUPUNGUZA UASI KANISANI 1. Uangalifu mkubwa uchukuliwe wakati wa kuandaa na kupima wabatizwa… 2. Viongozi wa kanisa kutembelea washiriki ili kuongea nao, kuomba nao, kufahamu mahitaji/madhaifu yao, na kupanga jinsi ya kuwasaidia…. ¨Kuzuru nyumba za washiriki kwa utaratibu uliopangwa; ¨Kuzuru nyumba za wenye shida maalumu, mf: wagonjwa, wakongwe, yatima, wajane, wagane, wafiwa;… Namna ya Kupunguza Uasi Kanisani ¨Kuzuru familia zilizopata mtoto karibuni (ndani ya robo); ¨Kuzuru ndoa zilizofungwa karibuni (ndani ya robo); ¨Tambua washiriki wasiohudhuria ibada mara kwa mara, watembelewe mara kwa mara,-hasa na mashemasi wa maeneo husika. 3. Mahubiri na mafundisho yaliyoandaliwa vyema … . 4. Kuimarisha huduma ya kushuhudia. Kuwepo na semina ya namna ya kushuhudia. Kila familia/kanisa liwe kituo cha uinjilisti na kila huduma ya ibada iwe ya kuongoa roho kwa Kristo. Namna ya Kupunguza Uasi Kanisani 5. Wahubiri wapewe semina ya namna ya kuhubiri ili wahubiri wawe walishaji … . 6. Kutoa ushauri kwa mtu mmoja mmoja… 7. Washiriki wafundishwe elimu ya uchumi… (jinsi ya kupata mali na jinsi ya kutumia) 8. Malezi kwa washiriki wapya, vijana na watoto kanisani yaimarishwe … Namna ya Kupunguza Uasi Kanisani 9. Washiriki wafundishwe / wakumbushwe umuhimu wa kumtegemea Mungu nyakati njema na nyakati mbaya. … . 10. Washiriki wafundishwe na kutiwa moyo kumshuhudia Kristo kwa maneno na matendo(mtindo wa maisha unaomwakisi Kristo). Madarasa ya Shule ya Sabato yawe timu za kushuhudia na za malezi. Makanisa yanayoshuhudia, maasi hupungua. Namna ya Kupunguza Uasi Kanisani 11. Kila Mwadventista wa Sabato ajifunze kuishi sawa na ujumbe wetu. •Washiriki wapya waone ushuhuda hai kwa washiriki wa zamani. •Utepetevu usipewe nafasi, viongozi waangalie walinzi walegevu Isa.49:22; 62:10; Yer.4:6; Eze.33:1-9; Isa.56:10-11. Namna ya Kupunguza Uasi Kanisani 12. Kuwepo na mikutano ya uamsho daima kwa ajili ya ukuaji kiroho wa waumini. Mikutano iwe na maandalizi na mpangilio mzuri unaovutia… [Programu zinazovutia] 13. Viongozi wa kanisa kuwashirikisha vijana na watoto katika huduma za ibada na shughuli mbalimbali za kanisa… Watalipenda kanisa. 14. Viongozi wa kanisa (wachungaji, wazee wa kanisa, …) watumie vyema miongozo ya kanisa katika uongozi wa kanisa la Mungu… Namna ya Kupunguza Uasi Kanisani 15. Viongozi wa kanisa kushughulikia dhambi kwa wakati kwa upendo. [Kuendelea kumpenda mkosaji huku ukishughulikia kosa lake…] 16. Kushughulikia changamoto za kiutamaduni na kijamii zinapotokea miongoni mwa waumini, kwa wakati na bila upendeleo au ubaguzi… Mfano: i. Ndoa kuvunjika ---- kutiwa moyo kuyakabili mazingira mapya…, na maombezi. ii. Kufiwa na mwenzi --- kutiwa moyo kuyakabili mazingira mapya…, na maombezi. Namna ya Kupunguza Uasi Kanisani iii. Kufiwa, au kuuguza muda mrefu --- kutembelewa na kutiwa moyo…, na maombezi. iv. Uchumi kuporomoka --- kutembelewa na kutiwa moyo…, na maombezi. v. Ndoa na mwenye imani tofauti --- ushauri na kutiwa moyo…, na maombezi. vi. Vijana me/ke wenye changamoto za kupata wenzi -- ushauri na kutiwa moyo…, na maombezi. vii. Wanandoa waliochelewa kupata mtoto ---- ushauri na kutiwa moyo…, na maombezi. §USHAURI: oKarani wa kanisa azingatie maelekezo yaliyoainishwa katika andiko hili ambayo yatasaidia kuongoza safari ya utendaji wake. oKarani wa kanisa asome na kufanyia kazi maelekezo ya kazi yake kama yalivyoandikwa katika Mwongozo wa Kanisa na Mwongozo wa Karani wa Kanisa. oMzee wa kanisa awe na Mwongozo wa Kanisa na Mwongozo wa Mzee na aliongoze kanisa kama ilivyoelekezwa katika miongozo hiyo…. Awe pia na miongozo ya idara zote za kanisa. §Majukumu yote haya na mengine yahusuyo KULEA na KUTUNZA washiriki, “Tunayaweza yote katika Yeye atutiaye nguvu” ….. §MUNGU ATUBARIKI SANA TUNAPOVUTA PAMOJA KATIKA UTUMISHI SHAMBANI MWAKE ILI KUMWANDALIA KRISTO BIBI ARUSI ASIYE NA MAWAA… oHii ni sehemu ya pili ya Semina za Kulea na Kutunza Washiriki. oIliyoandaliwa na kuwasilishwa na Mch. Amosi Lutebekela, Katibu Mkuu – Konferensi ya Mashariki-Kati mwa Tanzania (ECT). oWakati wa semina za kulea na kutunza washiriki mwaka 2019 katika makanisa/mitaa ya Konferensi ya Mashariki-Kati mwa Tanzania (ECT).