Uploaded by Daniel Ephraim

======SEMINA ZA KULEA NA KUTUNZA WASHIRIKI (II)=======

advertisement
SEMINA ZA KULEA NA KUTUNZA WASHIRIKI (II)
(Na Mch. Amosi Lutebekela, 2019)
§Katika uwasilishaji huu kutahusika na:
1) Kitabu cha Karani wa Kanisa
2) Majukumu mengine ya karani wa kanisa (baadhi)
3) Kinga / Tiba kwa washiriki wasiojulikana walipo
4) Utunzaji wa kumbukumbu
5) Mikakati ya kuwalea waumini wapya
6) Kuwarejesha / Kuwarudisha washiriki waliopotea
A. KITABU CHA KARANI WA KANISA
§Ushauri umetolewa kwamba kitabu kilichoandaliwa na
Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati ndicho kitumiwe
katika kuorodhesha majina ya washiriki wa kanisa….
§Kitabu hiki kitunzwe katika sanduku au kabati lenye
kufuli.
§Mara kwa mara majina yakaguliwe na mkuu wa
konferensi, au katibu wake, kuhakikisha kwamba idadi
ya washiriki iliyo katika kitabu ni sawa na ile iliyotumwa
konferensi.
oMwongozo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Toleo la 19, sahihisho la
2015, UK.236.
Kitabu cha Karani wa Kanisa
§Muundo wa Kitabu cha Karani wa Kanisa:
MAPOKEO--iwe kushoto, MAONDOLEO--iwe kulia.
§KITABU CHA KARANI WA KANISA KINA
SEHEMU KUU NNE:
1) WALIOINGIA (MAPOKEO) NA MAONDOLEO
2) MAHUDHURIO KATIKA MEZA YA BWANA
3) HABARI ZA BARAZA ZA KANISA
4) HABARI ZA MATENDO YA KANISA
Kitabu cha Karani wa Kanisa
1. MAPOKEO NA MAONDOLEO
oMAPOKEO, uingizaji wa majina kitabuni ---iwe kwa
herufi kubwa (Mwongozo wa Kanisa, 2015, UK.236)
oMAPOKEO. Kuna njia tatu za kuingia ushirika wa kanisa
mahalia [i.Kwa Ubatizo, ii.Kwa Mikono, iii.Kwa Barua].
Kila muumini huingia ushirika wa kanisa mahalia kwa njia
mojawapo ya hizo.
oMAPOKEO. Kuna sehemu tatu za kujaza tarehe --(i)Baraza, (ii)Mashauri, (iii)Alivyoingia –[Kwa Ubatizo au
Kwa Mikono au Kwa Barua]
Kitabu cha Karani wa Kanisa
oUandishi wa majina kwenye MAPOKEO ni kwa kadri
mshiriki alivyoingia, si kwa alfabeti.
oUandishi wa majina kwenye MAPOKEO ni majina
kamili kwa herufi kubwa, vifupisho viepukwe.
oUandishi wa majina kwenye MAPOKEO, kila mshiriki
awe na namba ya ushirika.
oTaarifa ya washiriki inapoandaliwa mwishoni mwa
robo, ni vyema kuhakiki idadi halisi kwa fomula
ifuatayo: MAPOKEO – MAONDOLEO = IDADI HALISI
Kitabu cha Karani wa Kanisa
oKila aliyebatizwa ni haki kupewa cheti cha
ubatizo na kadi ya ushirika (Mwongozo wa Kanisa, Toleo la
19, Sahihisho la 2015, uk.236)
oKumpokea mshiriki kwa mikono (kukiri imani),
uangalifu mkubwa unatakiwa (Mwongozo wa Kanisa,
Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.56)
vJina huandikwa katika Kitabu cha Karani wa
Kanisa mara moja tu hadi kufungwa kwa kitabu
mwishoni mwa muhula wa miaka mitano….
Kitabu cha Karani wa Kanisa
§Kanisa linapopangwa, kanisa walikotoka hujaza
Maondoleo kwa Barua; kanisa lililopangwa hujaza
Mapokeo kwa Barua.
§kanisa linapopangwa, kanisa wanakotoka tarehe
huonekana maeneo matatu upande wa maondoleo
(Baraza, Mashauri, Barua)
§Kanisa linapopangwa, washiriki wa kanisa lililopangwa
tarehe huonekana eneo moja tu – Mapokeo kwa Barua.
§ Kinachoandikwa kwenye njia mshiriki aliyopokelewa kanisani
(kwa ubatizo au kwa mikono au kwa barua) ni tarehe siyo alama
ya vema.
Kitabu cha Karani wa Kanisa
§MAONDOLEO. Kuna njia nne za maondoleo: i. Kwa
Barua (kuhama), ii. Kwa Mauti, iii. Kwa Kuasi, iv. kwa
Kutojulikana Aliko.
§MAONDOLEO. Kuna sehemu tatu za kujaza tarehe:
(i)Baraza, (ii)Mashauri, (iii)Alivyoondoka –[Kwa Barua
(kuhama), au Kwa Kuasi, au kwa Kutojulikana Alipo ].
oMaondoleo kwa Barua, tarehe hujazwa baada ya
kupata mrejesho toka kanisa alilohamia.
oMaondoleo kwa Mauti, hakuna tarehe ya baraza wala
mashauri; ni tarehe ya kifo tu. (Taz. (Mwongozo wa Kanisa,
Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.61)
Kitabu cha Karani wa Kanisa
oKuondolewa kwa Kuasi, maelekezo katika
Mwongozo wa Kanisa kuhusu Marudi ya Kanisa
YAZINGATIWE. (Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19, Sahihisho la
2015, Sura ya 7).
oKuondolewa kwa Kutojulikana Aliko, maelekezo katika
Mwongozo wa Kanisa kuhusu muda wa kuwatafuta
washiriki walioonekana kuwa hawajulikani waliko
YAZINGATIWE. [Washiriki Wanaohama Bila Taarifa].
(Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.74).
Kitabu cha Karani wa Kanisa
§KUPOKELEWA au KUONDOLEWA kwa Mshiriki ni kwa
kura ya kanisa tu au kwa kifo.
o“Majina huingizwa au kuondolewa kwa kura ya kanisa
tu au kwa kifo.” – Mwongozo wa kanisa,…2015, uk.61.
qKitabu kipya cha karani wa kanisa kinapoandikwa
mwanzoni mwa muhula wa miaka mitano, majina
ya wote walioondolewa ushirika [kwa barua (kuhama),
kwa mauti, kwa kuasi, kwa kutojulikana walipo], huachwa
kwenye kitabu kilichofungwa.
Kitabu cha Karani wa Kanisa
¨Kila mshiriki aliyepokelewa kanisani [Kwa Ubatizo au
Kwa Mikono au Kwa Barua], kuwepo agenda na miniti
kwenye vikao viwili – Baraza la Kanisa na Mashauri
ya Kanisa (Mkutano Mkuu wa Kanisa).
¨Kila mshiriki aliyeondolewa ushirika [Kwa Barua au
Kwa Kuasi au Kwa Kutojulikana Aliko], kuwepo agenda
na miniti kwenye vikao viwili – Baraza la Kanisa na
Mashauri ya Kanisa (Mkutano Mkuu wa Kanisa).
§ Kinachoandikwa kwenye njia mshiriki aliyoondolewa ushirika
(kwa barua au kwa mauti au kwa kuasi au kwa kutojulikana
aliko) ni tarehe siyo alama ya vema.
Kitabu cha Karani wa Kanisa
¨USHIRIKA WAKATI WA UHAMISHO
§“Kwa hali yo yote ile, karani wa kanisa analotokea
mshiriki,hataliondoa jina la mshiriki katika kumbukumbu
za washiriki mpaka ipokelewe sehemu ya barua ya
uhamisho inayothibitisha kuwa mshiriki huyo
amepokelewa katika ushirika wa kanisa analohamia.
§Karani, wazee, mchungaji na mwenyekiti wa konferensi
wote wanawajibika kuhakikisha kuwa makanisa yote
yanafuata utaratibu huu.”
§ Mwongozo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Toleo la 19, Sahihisho la
2015, uk.59.
Kitabu cha Karani wa Kanisa
o“Mara kwa mara washiriki waelekezwe wajibu wao
wa kuhakikisha kwamba ushirika wao uko katika
kanisa la mahali wanapoishi. Maelezo ya kuhamisha
washiriki yaliyomo katika mwongozo huu yazingatiwe
sana.
• Inawapasa makarani wa kanisa kuhakikisha kwamba
maombi ya uhamisho yanafanywa upesi.” (Mwongozo wa
Kanisa la Waadventista wa Sabato, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.241).
§“Mshiriki akiondolewa katika ushirika wa kanisa kwa
kura ya kanisa, karani wa kanisa atamwarifu kwa
kumwandikia barua.” (Mwongozo wa Kanisa, 2015, uk.236).
[Tazama pia uk. 75].
Kitabu cha Karani wa Kanisa
2. MAHUDHURIO KATIKA MEZA YA BWANA
oOrodha ya majina iwe sawa na ya kwenye MAPOKEO….
oJina huandikwa mara moja tu kitabuni hadi kufungwa kwa
kitabu mwishoni mwa muhula wa miaka mitano….
oZingatia ujazaji wa mahudhurio ya Meza ya Bwana kwa muhula
husika… [mfano: 2016, 2017, 2018, 2019, 2020]; kila robo kwa
wakati.
oUjazaji: Weka alama ya vema kwenye kisanduku mbele ya jina kwa
robo husika ya mwaka husika; usiweke tarehe.
oAliyeshiriki Meza ya Bwana nje ya kanisa lenye ushirika wake,
taarifa imfikie karani wake wa kanisa ili amjazie kumbukumbu.
Kitabu cha Karani wa Kanisa
3. HABARI ZA BARAZA ZA KANISA
oVipengele muhimu vya kukumbuka:
i. Aina ya kikao: Baraza la Kanisa au Mkutano Mkuu wa kanisa;
[Kikao cha Wazee,…kumbukumbu zake hazitunzwi katika kitabu hiki]
ii.
iii.
iv.
v.
vi.
Mahali kikao kilipofanyikia;
Tarehe ya kikao;
Waliohudhuria;
Wasiohudhuria kwa taarifa;
Wasiohudhuria bila taarifa;
Kitabu cha Karani wa Kanisa
oOmbi la ufunguzi na mwombaji
oFungu la ufunguzi wa kikao na mnenaji
oOmbi la kufunga na mwombaji
oOrodha ya agenda ….
oMuhutasari huandikwa kwa kifupi ---agenda na
azimio… [soma zaidi Mwongozo wa Karani wa Kanisa]
oAliyeomba ombi la kufunga….
oMwenyekiti wa kikao na Katibu wa kikao --- [Sahihi /
Jina /Wadhifa / Tarehe]
Kitabu cha Karani wa Kanisa
¨Kuhusu uandishi wa kumbukumbu za vikao:
oKumbukumbu za vikao vya Baraza la Kanisa vyote,
maalumu na vya dharura huandikwa katika kitabu hiki.
oKumbukumbu za vikao vya Mkutano Mkuu wa Kanisa
(Mashauri ya Kanisa) vyote, maalumu na vya dharura
huandikwa katika kitabu hiki
oUandishi wa Miniti za vikao kitabuni iwe kwa
muhtasari kwa kadri inavyowezekana.
oIkumbukwe kuwa kumbukumbu za vikao vya wazee
haziandikwi kwenye Kitabu cha Karani wa Kanisa.
Kitabu cha Karani wa Kanisa
oKarani wa kanisa anashauriwa kuandika miniti katika
kitabu cha karani wa kanisa mara baada ya kikao, ili
kuepuka kusahau mpangilio mzuri wa muhtasari.
§Mfano wa uandishi wa muhtasari wa baraza:
• Mfano wa 1:
• AGENDA: MWAKILISHI KATIKA MKUTANO MKUU WA
KONFERENSI.
oIliamuriwa: Kumchagua ndugu Philip Kiboko kuliwakilisha
Kanisa katika mkutano mkuu wa Konferensi wa mwaka 2015.
Kitabu cha Karani wa Kanisa
Mfano wa 2:
• AGENDA: KWAYA YA KANISA KWENDA KUREKODI
oIliamriwa: Kuiruhusu kwaya ya kanisa kwenda Dar es
Salaam kurekodi nyimbo katika Studio ya Morning Star
Radio kati ya Januari 25-29 kwa gharama zao wenyewe.
§Lakini yapo maamuzi ambayo kwa sababu ya uzito
wake au kwa kuwa yanahitaji kuonesha kiini na
sababu za kufikia maamuzi hayo, huwa inatakiwa
kueleza kwa kifupi sababu zilizopelekea kufikia
maamuzi hayo.
Kitabu cha Karani wa Kanisa
•Mfano wa 3:
oKwa kuwa ndugu Machomane Tabia Mbaya
amekiuka amri ya saba inayokataza uzinzi; na
kwa kuwa kosa lake limekuwa la wazi na limeleta
aibu kwa kanisa; na kwa kuwa taratibu zote za
kumsaidia kwa mujibu wa Mathayo 18
zimefuatwa kikamilifu, Iliamuriwa: Kuondoa jina
la Machomane Tabia Mbaya kwenye kitabu cha
ushirika wa Kanisa.
Kitabu cha Karani wa Kanisa
4. HABARI ZA MATENDO YA KANISA
§Hapa, huorodheshwa wote walioondolewa ushirika [kwa
barua, kwa mauti, kwa kuasi, kwa kutojulikana walipo].
§Zingatia kumbukumbu zifuatazo:
oTarehe ya Baraza….
oNamba ya ushirika….
oJina la mshiriki….
oShauri na Tarehe yake….
oTendo la Kanisa…..
• Kwa mauti, hakuna tarehe ya baraza, shauri, wala tendo.
Kitabu cha Karani wa Kanisa
oShauri na Tarehe yake.
üShauri ni ile sababu iliyopelekea maondoleo; MFANO:
i. Uzinzi / Uongo / Wizi / Kuvunja Sabato / Kukana Imani
(N.k.) --- [ikiwa ndiyo sababu ya maondoleo].
ii. Uhamisho ---- [ikiwa ndiyo sababu ya maondoleo].
iii. Kutojulikana Aliko --- [ikiwa ndiyo sababu ya maondoleo].
üTarehe ni ile ambayo Mashauri ya Kanisa ilifanya mjadala na
maamuzi juu ya shauri husika. Inaandikwa mbele ya shauri.
oMshiriki akifa, hakuna shauri, maana hakuna mjadala;
huandikwa Mauti na tarehe aliyokufa.
Kitabu cha Karani wa Kanisa
oTendo la Kanisa.
üTendo ni uamuzi uliochukuliwa kwa kupiga kura,
•MFANO:
i. Kuondolewa ushirika wa kanisa
ii. Kuhamisha ushirika wa kanisa
iii. Kuondolewa ushirika wa kanisa
oMshiriki akifa, hakuna tendo, maana hakuna
kupiga kura; huandikwa tu Kifo
B. MAJUKUMU MENGINE YA KARANI WA KANISA (baadhi)
oHushughulikia uhamisho wa washiriki… (Mwongozo wa
Kanisa, 2015, 57-62)
• “Mara kwa mara washiriki waelekezwe wajibu wao wa
kuhakikisha kwamba ushirika wao uko katika kanisa mahalia
wanaposali. Maelezo ya kuhamisha washiriki yaliyomo katika
Mwongozo wa Kanisa yazingatiwe.” – Mwongozo wa Kanisa, 2015,
241.
• “Washiriki wanaohamia eneo jingine kwa zaidi ya miezi
sita hawana budi kuomba barua ya uhamisho mara
moja.” – Mwongozo wa Kanisa, 2015, uk.57.
Majukumu Mengine ya Karani wa Kanisa
oHujaza Fomu ya Miito ya Hudumu baada ya
wahudumu wanaoitwa kupitishwa na baraza la
kanisa….kisha kuiwasilisha Konferensi kwa wakati.
oKuhesabu waliohudhuria ibada Sabato ya 2 na ya 7 ya robo
oKujaza kwa ubora taarifa ya washiriki ya kila robo na
kuiwasilisha kwa mchungaji kwa wakati…
oKuwasiliana na washiriki wasiohudhuria kanisani….
(Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.94,211)
oNa majukumu mengine kama yalivyoainishwa kwenye
Mwongozo wa Kanisa na Mwongozo wa Karani wa Kanisa….
C. KINGA KWA WASHIRIKI WASIOJULIKANA WALIPO
A. Jinsi ya kupunguza au kuondoa changamoto ya
washiriki kutojulikana walipo?
1. Kutendea haki kazi ya baraza ya kupitia majina ya
washiriki angalau mara moja kwa mwaka…(Mwongozo wa
Kanisa, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.155).
2. Kuweka utaratibu wa kuandika kumbukumbu pana za
mshiriki,
§ MFANO:
i. Jina (majina matatu)___________________
ii. Jinsia _______ Hali ya ndoa ____________
Kinga kwa Washiriki Wasiojulikana Walipo
iii. Tarehe ya kuzaliwa ________________________
iv. Mahali alipozaliwa ________________________
v. Makazi / Mahali anapoishi ___________________
vi. Mahali pa kazi na kazi ______________________
vii. Namba ya simu ___________________________
viii. Anuani ya barua pepe _____________________
ix. Dini au dhehebu la awali ____________________
x. Jina la ndugu au jamaa ya karibu ______________
Kinga kwa Washiriki Wasiojulikana Walipo
xi. Mawasiliano ya ndugu au jamaa ya karibu ______________
xii. Mahali anapoishi ndugu au jamaa ya karibu____________
xiii. Mshiriki wa SDA anayemfahamu ____________________
xiv. Mawasiliano ya mshiriki wa SDA anayemfahamu _______
xv. Tarehe na mahali alibatizwa ________________________
xvi. Jina la mchungaji aliyembatiza _____________________
3. Washiriki wakumbushwe kuwa, mshiriki
anapoondoka sehemu fulani ni juu yake kulitaarifu
kanisa (mzee au karani wa kanisa lake) mahali pale
atakapokuwa.
Kinga kwa Washiriki Wasiojulikana Walipo
o“Mshiriki anapohamia mahali pengine, inampasa
karani wa kanisa lenye taarifa za ushirika wake
kumwandikia katibu wa konferensi husika akiomba
mchungaji wa eneo hili jipya amtembelee mshiriki
huyo ili kufanikisha uhamisho wa ushirika wake…”
o“Washiriki wanaohamia kwenye eneo lingine kwa
zaidi ya miezi sita hawana budi kuomba barua ya
uhamisho mara moja”. (Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19,
Sahihisho la 2015, uk.57).
D. UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU (RECORD MANAGEMENT)
§Utunzaji wa kumbukumbu (Record Management) ni
suala muhimu sana kanisani kama ilivyo serikalini au
katika jamii…
i. Hufaa kuwa rejea mgogoro unapotokea…
ii. Hufaa kuwa rejea kwa mfanya utafiti…
§Zingatia: Kumbukumbu zinaongezeka ubora au
thamani kwa kadri muda unavyoondelea….
Utunzaji wa Kumbukumbu
¨Karani Hutunza Kumbukumbu---(tazama: Mwongozo wa
Kanisa, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.94-95, 210).
¨“Karani huandika kumbukumbu za kanisa, ambazo
hazina budi kuhifadhiwa vizuri.” (Mwongozo wa Kanisa, Toleo
la 19, Sahihisho la 2015, uk.94).
¨“Kumbukumbu za washiriki hazina budi kutunzwa
kwa usahihi na kuboreshwa kila wakati ili kuonesha hali
rasmi ya washiriki.” (Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19, Sahihisho
la 2015, uk.210).
¨Kitabu cha Karani wa Kanisa kitunzwe wapi?
(Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19, Sahihisho la 2015, uk.236).
Utunzaji wa Kumbukumbu
§Mahali gani zinatunzwa nyaraka za kanisa?
1) Nakala ya mauziano ya kiwanja cha kanisa…
2) Nakala ya hati miliki ya kiwanja cha kanisa…
üUnunuzi wa viwanja vya kanisa, jina liandikwe la
Trustee siyo la kanisa mahalia. Jina linaloandikwa ni:
oTHE REGISTERED TRUSTEE OF SEVENTH-DAY
ADVENTIST CHURCH OF TANZANIA
• Na kwamba, manunuzi ya kiwanja cha kanisa au shamba,
uongozi wa serikali wa eneo husika uhusishwe…
Utunzaji wa Kumbukumbu
3) Cheti cha kuwekwa wakfu kanisa mahalia…
4) Historia ya kanisa mahalia….iwe endelevu….
5) Barua mbalimbali toka au kwenda konferensi…
6) Barua mbalimbali toka au kwenda serikalini…
7) Nakala za barua za walioondolewa ushirika kwa
marudi…
8) Taarifa mbalimbali ziendazo ngazi za juu za kanisa….
9) Mpango mkakati wa kanisa mahalia …..
Utunzaji wa Kumbukumbu
10) Mchoro unaoonesha matumizi ya kiwanja cha kanisa – [Master
Plan].
11) Miongoni mwa kumbukumbu zipasazo kutunzwa kwa makini
sana ni MUHTASARI ZA VIKAO – BARAZA LA KANISA NA MKUTANO
MKUU WA KANISA.
12) Kila kanisa mahalia liwe na historia ya kanisa mahalia husika.
Historia iwe endelevu, tangu kupangwa
oNa kadhalika.
¨ZINGATIA: Wakati wa makabidhiano kwa uongozi mpya –
kuwepo na orodha ya vinavyokabodhiwa kwa kiongozi mpya….
Utunzaji wa Kumbukumbu
§Mahali gani zinatunzwa mali za kanisa?
üVifaa vya Meza ya Bwana….
üKitabu cha orodha ya vifaa vya kanisa…
üMiongozo ya kanisa na miongozo ya idara ….
üVitabu vya taarifa….
üVifaa vya idara ya vijana…
üVifaa vya idara ya watoto…
üNa kadhalika.
Utunzaji wa Kumbukumbu
§Kila kanisa mahalia liwe na chumba maalumu chenye
kabati la kutunzia vifaa vya kanisa na nyaraka za
kanisa.
§kila kanisa mahalia liwe na ofisi za kanisa ---- ofisi ya
mchungaji, ofisi ya karani wa kanisa, ofisi ya wazee wa
kanisa, ofisi ya mashemasi, ofisi ya mhazini, n.k.
§Kila kanisa mahalia limwezeshe karani wa kanisa kuwa
na faili mbalimbali za kutosha kutunzia nyaraka
mbalimbali za kanisa.
Utunzaji wa Kumbukumbu
§Kila kanisa mahalia, kwa kadri inavyowezekana, liwe na
kompyuta kwa ajili ya ofisi ya karani wa kanisa kutumia,
pamoja na kuweka kumbukumbu ‘kidigitari’….
§Kumbukumbu za Orodha ya Washiriki zinapowekwa
kidigitali, mpangilio uliowekwa na Divisheni ya Afrika
Mashariki na Kati uzingatiwe.
§Kila karani wa kanisa mahalia awe na uwezo wa
kuwasajili washiriki wa kanisa lake kwenye mfumo wa
kanisa – ACMS (Adventist Church Management System).
Utunzaji wa Kumbukumbu
§Kuwe na uangalifu mkubwa katika kuchagua au
kutengeneza mahali salama pa kutunzia mali na nyaraka za
kanisa…
§Kila kanisa mahalia liwe na utaratibu wa namna ya kutunza
kumbukumbu za muda mrefu (archive)– ‘hard’ & ‘soft’.
vIkiwa, kwa sababu fulani, imelazimu Kitabu cha
Karani wa Kanisa au nyaraka / vifaa vya kanisa
kutunzwa kwa mtu binafsi badala ya ofisi ya kanisa,
kuwepo ridhaa ya kanisa kupitia vikao vyake.
§KUMBUKA:
§“Sehemu kubwa ya ufanisi wa shughuli za
kanisa hutegemea karani. Kutokana na
umuhimu na upekee wa majukumu ya ofisi
hii, ni vyema kuchagua mtu ambaye
anaweza kuchaguliwa tena ili kuwe na
mwendelezo katika uhifadhi na utoaji wa
taarifa.” – Mwongozo wa Kanisa, Toleo la 19, sahihisho la
2015, uk.93.
§Karani wa kanisa ni miongoni mwa maofisa wa kanisa
mahalia wanaofanya kazi kwa karibu sana na wazee wa
kanisa na mchungaji.
§Karani wa kanisa, ili afanye kazi yake kwa ufanisi,
anatarajiwa:
1. Ajitoe kikamilifu
2. Awe makini katika utendaji wake
3. Awe mwaminifu na mwadilifu
4. Awe tayari kutumika
5. Awe mwenye kumbukumbu nzuri/asiwe msahaulifu
6. Awe mfuatiliaji mzuri wa maamuzi
7. Awe anayependa kushirikiana na wengine
8. Awe mtunza siri.
§UJUMBE MUHIMU KWA KARANI WA KANISA:
• “Aandamaye haki na Fadhili, Ataona uhai na
haki na heshima.” (Mit.21:21)
• “Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki
huikimbilia, akawa salama.” (Mit.18:10)
E. MIKAKATI YA KUWALEA WAUMINI WAPYA
¨Mshiriki mpya ni mtoto mchanga aliyezaliwa katika
familia ya kanisa; hivyo,
1) Asiachwe kujitafutia chakula yeye mwenyewe…
2) Asiachwe kujivalisha nepi/pampasi yeye mwenyewe ….
3) Asiachwe kujitengenezea mfumo wa maisha…
§Vile tuwafanyiavyo watoto wanaozaliwa katika familia
zetu, hali kadhalika katika familia ya Mungu…
§Baada ya kuwabatizwa, waumini wapya wafundishwe
kuyashika yote Yesu aliyoyaamuru (Mt.28:18-20)
Kuwalea Waumini Wapya
§Ufundishaji wa waumini wapya uzingatie,
oKuwaanzishia chakula chepesi kabla ya kigumu –
1Kor.3:2; Ebr.5:13; 1Pet.2:2.
oWaumini wapya wakuzwe katika mafundisho ya Imani za
Msingi za Waadventista wa Sabato. Wafundishwe mfumo
wa kanisa sambamba na Imani za Msingi.
oWaumini wapya wafundishwe Viwango vya Maisha ya
Kikristo …. (Rum.12:1-2) [Taz. Mwongozo wa Kanisa, Toleo la
19, Sahihisho la 2015, Sura ya 12.]
oWaumini wapya wafundishwe Karama za Roho na
Huduma….
Kuwalea Waumini Wapya
oWaumini wapya wafundishwe namna ya kumshuhudia Yesu,
kuhudumu kanisani, mahusiano…, uchumi…,…
oWaumini wapya wasajiliwe katika idara na vyama
kanisani…
oWaumini wapya wafundishwe kumtegemea Mungu
nyakati zote – za raha na za shida…
oHadi hapa, sasa waumini wapya wanaweza kufundishwa
masomo ya unabii wa Biblia…. (2Pet.1:19)
oSasa si watoto wadogo tena bali ni watu wazima katika
Kristo, ambao wameyabatilisha mambo ya kitoto…
(1Kor.13:11)
Kuwalea Waumini Wapya
¨Katika hili, uongozi wa kanisa unatazamiwa:
1) Kuwaimarisha waumini wapya katika imani na
ushirika… Kuwapa mafunzo juu ya maisha ya Kikristo… {Mchungaji +
Wazee wa Kanisa} ….
2) Kuwatumia washiriki wa zamani kuwasaidia washiriki
wapya kukua …. Urafiki na kutumia karama zao za kiroho kulea na
kuimarisha wachanga… Kuwa kielelezo katika tabia/mwenendo
3) Kuhusisha idara za kanisa katika kulea --- Hasa: (i) Huduma
za Wanawake (AWM), (ii) Chama cha Wanaume Waadventista (AMO),
(iii) Huduma za Vijana Waadventista, (iv) Huduma za Watoto.
ü Hii ni kwa sababu washiriki wa kanisa ni wanaume au wanawake au
vijana au watoto.
Kuwalea Waumini Wapya
4) Kuwahusisha waumini wapya katika shughuli na
programu za kanisa…. Huduma za ibada, Kujifunza Biblia,
Kwaya ya kanisa, Kushuhudia, na Ushirika, …
o Kwa kuhusishwa, waumini wapya huweza kukuza mahusiano na
kugundua na kutumia karama za Roho.
5) Kuwasajili katika vikundi vidogo… Mf. Vikosi vya Shule ya
Sabato; Vikosi vya kujifunza Biblia, vikosi vya kushuhudia, vikosi
vya kusaidia, vikosi vya maombi, n.k.
o Mpango huu ulikuwa sababu ya kukua haraka kwa kanisa la
mitume…
Kuwalea Waumini Wapya
vMoja ya jambo muhimu kwa vikosi vidogo vya nyumbani--hukuza ushirika wa kina miongoni mwa washiriki / waumini.
6) Kuwatembelea nyumbani …. Kuomba nao, kujifunza
nao, kuwashauri, na kuwatia moyo….
qMuumini mpya anaweza kuwa na mapungufu kama
ilivyo kwa mtoto katika familia…AFUNDISHWE…
AVUMILIWE….ASAIDIWE KUKUA….
oYohana 21:15-17 “…wana-kondoo…”
F. KUWARUDISHA WASHIRIKI WALIOPOTEA
KUWARUDISHA WASHIRIKI WALIOPOTEA
§Suala la kumrejesha mshiriki aliyepotea ni:
•Agenda ya Yesu mwenyewe…. Luka 15:3-7; 19:10.
•Agizo la Mungu la enzi zote…...Eze.3:17-21.
§Tafakari mazingira ya kondoo aliyepotea na
mtafutaji (Luka 15:3-7):
oMtafutaji alikuwa mwenye huruma kwa kondoo
aliyepotea.
Kuwarudisha Washiriki Waliopotea
oHakumshutumu kwa upotevu wala hakumgombeza
oAlipompata, alimkumbatia kwa upendo mwingi…., na
kufurahi na wote…(taz. Luka 15:5-6, 7)
§Yesu akitoa mfano wa kondoo aliyepotea na moyo
wa mtafutaji, alitoa kielelezo juu ya:
oKile alichofanya kwa jamii ya mwanadamu ….. Filp.2:5-8….
oKile kanisa na kila muumini twapaswa kufanya kwa
mshiriki aliyetanga mbali kimaadili…Eze.3:17-21
Kuwarudisha Washiriki Waliopotea
oMungu ndiye alifanya juhudi ya kumtafuta Adamu baada
ya dhambi kumtenga na Mungu -- Adamu, uko
wapi?...Mwa.3:9.
§Tafakari juu ya moyo wa baba wa mwana
mpotevu aliporudi nyumbani – Lk.15:20-24.
1) Hakumgombeza wala kumshutumu ….
2) Alimhurumia ….
3) Alimhudumia kwa upendo….
oNdivyo itupasavyo kuwatendea washiriki walioliacha
kanisa wanaporejea kanisani.
Kuwarudisha Washiriki Waliopotea
¨Ziko sababu zinazofanya washiriki kupoa
kiroho/kurudi nyuma/kupotea; (taz. Mwongozo wa
Mzee, 136).
§Ili kuwarejesha; kwanza watambue, kisha
watembelee.
oHapa ni mashauri saba kuongoza safari yako:
1) Uliza maswali kwa busara….
2) Sikiliza kwa makini tena kwa maombi majibu
wanayoyatoa….
Kuwarudisha Washiriki Waliopotea
3) Usilalie upande wo wote katika
maongezi yako….
4) Heshimu usiri….
5) Waombee….
6) Waalike warejee kanisani…
7) Uwapende….
F1. BAADHI YA SABABU ZA BAADHI YA WASHIRIKI
KUASI
1. Malezi hafifu kwa washiriki wapya:
• Chakula hafifu cha kiroho i.e. mahubiri na mafundisho
yasiyolenga mahitaji au yasiyoandaliwa vyema.
• Kutopata joto (urafiki)toka kwa washiriki wa zamani.
• Kutotembelewa na kutiwa moyo.
• Kutoshirikishwa katika programu mbalimbali ndani ya
kanisa.
Baadhi ya Sababu za Baadhi ya Washiriki Kuasi
2. Baadhi ya watu kujiunga na kanisa kwa
matarajio mbalimbali, tofauti na kumfuta
Yesu….
3. Kutokuwepo na ratiba nzuri ya viongozi wa
kanisa kutembelea washiriki….
4. Washiriki kutojihusisha na jukumu la
kumshuhudia Yesu…
Baadhi ya Sababu za Baadhi ya Washiriki Kuasi
5. Kwa nini baadhi ya vijana huliacha kanisa…
oKutotembelewa na kutiwa moyo….
oKutoshirikishwa katika programu mbalimbali ndani
ya kanisa… au Huduma zao kutothaminiwa….
oKutowapatia semina/masomo maalumu kulingana
na rika zao…
oKukumbwa na shinikizo rika….
oKutotiwa moyo katika kukabili changamoto za
ujana…
Baadhi ya Sababu za Baadhi ya Washiriki Kuasi
6. Matatizo ya kiutamaduni na kijamii,
oMfano:
i. Ndoa kuvunjika….au kuwa na migogoro isiyo
na ufumbuzi…
ii. Kufiwa, au kuuguza muda mrefu bila kuona
joto la kanisa….
iii. Uchumi kuporomoka….
iv. Ndoa na mwenye imani tofauti…,
• Na kadhalika….
Baadhi ya Sababu za Baadhi ya Washiriki Kuasi
7. Kukosekana au kupungua kwa ibada katika familia….
8. Kuchelewa kushughulikia dhambi za wazi…
9. Kushughulika na masumbufu ya maisha haya na kukosa
muda kwa mambo ya milele...
10. Upendo kupoa miongoni mwa washiriki… hivyo ubaguzi –
kikabila, kiuchumi, kielimu, kijinsia, kirika, n.k.
11. Mahusiano hafifu katika ndoa …. makwazo…
12. Hali ngumu ya kiuchumi hupelekea baadhi ya washiriki
kufanya kazi na siku ya Sabato, wengine kuliacha kanisa.
Baadhi ya Sababu za Baadhi ya Washiriki Kuasi
13. Matatizo ya kiutawala kanisani….
14. Kutokukubaliana na Kanuni za Kanisa katika masuala
fulani…
15. Washiriki kutokuwa wachunguzi wa Maandiko
Matakatifu, hivyo kutegemea tu kile asemacho mhubiri.
Akipotosha andiko, nao hupotoshwa….
16. Ushuhuda wa mwenendo mbaya ambao washiriki
wapya huupokea (kuuona) kutoka kwa washiriki wa
zamani.
Baadhi ya Sababu za Baadhi ya Washiriki Kuasi
17. Manung’uniko/makwazo tokana na utendaji
unaokinzana na taratibu na mfumo wa kanisa….
Mfano:
o upotevu wa fedha za kanisa,
o washiriki kutopewa taarifa ya mapato na matumizi,
o viongozi kutotunza siri za waumini,
o dhambi miongoni mwa viongozi,
o ubaguzi katika kuhudumia washiriki wakati wa mahitaji,
o masengenyo/umbea/masingizio,
o kiongozi au mhubiri kunena kwa kuaibisha/kudhalilisha
muumini au mgeni.
F2. NAMNA YA KUPUNGUZA UASI KANISANI
1. Uangalifu mkubwa uchukuliwe wakati wa kuandaa
na kupima wabatizwa…
2. Viongozi wa kanisa kutembelea washiriki ili kuongea
nao, kuomba nao, kufahamu mahitaji/madhaifu yao,
na kupanga jinsi ya kuwasaidia….
¨Kuzuru nyumba za washiriki kwa utaratibu
uliopangwa;
¨Kuzuru nyumba za wenye shida maalumu, mf:
wagonjwa, wakongwe, yatima, wajane, wagane,
wafiwa;…
Namna ya Kupunguza Uasi Kanisani
¨Kuzuru familia zilizopata mtoto karibuni (ndani ya robo);
¨Kuzuru ndoa zilizofungwa karibuni (ndani ya robo);
¨Tambua washiriki wasiohudhuria ibada mara kwa mara,
watembelewe mara kwa mara,-hasa na mashemasi wa
maeneo husika.
3. Mahubiri na mafundisho yaliyoandaliwa vyema … .
4. Kuimarisha huduma ya kushuhudia. Kuwepo na semina ya
namna ya kushuhudia. Kila familia/kanisa liwe kituo cha
uinjilisti na kila huduma ya ibada iwe ya kuongoa roho kwa
Kristo.
Namna ya Kupunguza Uasi Kanisani
5. Wahubiri wapewe semina ya namna ya kuhubiri ili
wahubiri wawe walishaji … .
6. Kutoa ushauri kwa mtu mmoja mmoja…
7. Washiriki wafundishwe elimu ya uchumi… (jinsi ya
kupata mali na jinsi ya kutumia)
8. Malezi kwa washiriki wapya, vijana na watoto
kanisani yaimarishwe …
Namna ya Kupunguza Uasi Kanisani
9. Washiriki wafundishwe / wakumbushwe umuhimu
wa kumtegemea Mungu nyakati njema na nyakati
mbaya. … .
10. Washiriki wafundishwe na kutiwa moyo
kumshuhudia Kristo kwa maneno na matendo(mtindo
wa maisha unaomwakisi Kristo). Madarasa ya Shule ya
Sabato yawe timu za kushuhudia na za malezi.
Makanisa yanayoshuhudia, maasi hupungua.
Namna ya Kupunguza Uasi Kanisani
11. Kila Mwadventista wa Sabato ajifunze kuishi
sawa na ujumbe wetu.
•Washiriki wapya waone ushuhuda hai kwa
washiriki wa zamani.
•Utepetevu usipewe nafasi, viongozi waangalie
walinzi walegevu Isa.49:22; 62:10; Yer.4:6;
Eze.33:1-9; Isa.56:10-11.
Namna ya Kupunguza Uasi Kanisani
12. Kuwepo na mikutano ya uamsho daima kwa ajili ya
ukuaji kiroho wa waumini. Mikutano iwe na maandalizi na
mpangilio mzuri unaovutia… [Programu zinazovutia]
13. Viongozi wa kanisa kuwashirikisha vijana na watoto
katika huduma za ibada na shughuli mbalimbali za kanisa…
Watalipenda kanisa.
14. Viongozi wa kanisa (wachungaji, wazee wa kanisa, …)
watumie vyema miongozo ya kanisa katika uongozi wa
kanisa la Mungu…
Namna ya Kupunguza Uasi Kanisani
15. Viongozi wa kanisa kushughulikia dhambi kwa wakati
kwa upendo. [Kuendelea kumpenda mkosaji huku
ukishughulikia kosa lake…]
16. Kushughulikia changamoto za kiutamaduni na kijamii
zinapotokea miongoni mwa waumini, kwa wakati na bila
upendeleo au ubaguzi… Mfano:
i. Ndoa kuvunjika ---- kutiwa moyo kuyakabili
mazingira mapya…, na maombezi.
ii. Kufiwa na mwenzi --- kutiwa moyo kuyakabili
mazingira mapya…, na maombezi.
Namna ya Kupunguza Uasi Kanisani
iii. Kufiwa, au kuuguza muda mrefu --- kutembelewa
na kutiwa moyo…, na maombezi.
iv. Uchumi kuporomoka --- kutembelewa na kutiwa
moyo…, na maombezi.
v. Ndoa na mwenye imani tofauti --- ushauri na kutiwa
moyo…, na maombezi.
vi. Vijana me/ke wenye changamoto za kupata wenzi -- ushauri na kutiwa moyo…, na maombezi.
vii. Wanandoa waliochelewa kupata mtoto ---- ushauri
na kutiwa moyo…, na maombezi.
§USHAURI:
oKarani wa kanisa azingatie maelekezo
yaliyoainishwa katika andiko hili ambayo yatasaidia
kuongoza safari ya utendaji wake.
oKarani wa kanisa asome na kufanyia kazi
maelekezo ya kazi yake kama yalivyoandikwa katika
Mwongozo wa Kanisa na Mwongozo wa Karani wa
Kanisa.
oMzee wa kanisa awe na Mwongozo wa Kanisa na
Mwongozo wa Mzee na aliongoze kanisa kama
ilivyoelekezwa katika miongozo hiyo…. Awe pia na
miongozo ya idara zote za kanisa.
§Majukumu yote haya na mengine yahusuyo
KULEA na KUTUNZA washiriki, “Tunayaweza
yote katika Yeye atutiaye nguvu” …..
§MUNGU ATUBARIKI SANA TUNAPOVUTA
PAMOJA KATIKA UTUMISHI SHAMBANI
MWAKE ILI KUMWANDALIA KRISTO
BIBI ARUSI ASIYE NA MAWAA…
oHii ni sehemu ya pili ya Semina za Kulea na Kutunza
Washiriki.
oIliyoandaliwa na kuwasilishwa na Mch. Amosi
Lutebekela, Katibu Mkuu – Konferensi ya Mashariki-Kati
mwa Tanzania (ECT).
oWakati wa semina za kulea na kutunza washiriki mwaka
2019 katika makanisa/mitaa ya Konferensi ya
Mashariki-Kati mwa Tanzania (ECT).
Download