IJUMAA Ijumaa ilianza bila ya mbwembwe. Niliamka nikiwa na tamaa ya kuwa mikononi na katika sita kwa sita ya aina yake na Freddy Mjamaika wangu toka Uluguru. Katika mawazo yangu na hisia zangu zote Freddy alikuwa ni Mjamaika daima kwani hata Kiswahili chake bado kina lafudhi kali ya Kijamaika. Hivyo niliamka nikiwa na matamanio ya ajabu. Unajua kuna wakati wanawake tunaamka asubuhi ukiwa na hamu ya kufanya mapenzi ambayo mfano wake hakuna, ni hamu ambayo inapenya kwenye mifupa na mishipa, inaacha alama kwenye chembechembe za damu na endapo unapata nafasi ya kupata cha kuamkia basi kinakuwa cha kutiana kucha na kuumana meno. Hivyo ndivyo nilivyo amka asubuhi ya Ijumaa. Nilitamani kile alichokianzisha jana pale Blue Pearl angekimalizia kuanzia asubuhi ile. Uzuri nikuwa kuliko ilivyo kawaida Waziri aliondoka mapema kwa ajili ya kusimamia maandalizi ya mwisho ya sherehe za Muungano kesho yake. Nilimaliza mambo ya hapo nyumbani kama kwenye saa tatu hivi nikawa nimedhamiria ikifika saa tano niwe ninaondoka hapo kuelekea Saloon. Nilikuwa na miadi kule ya saa nane za mchana. . Sijui kitu gani kilikuwa kimenishikilia kwani nilijisikia hamu ya kumtumia Freddy sms ya kumjulia hali au nifanye tu ili niweze kuwasiliana naye. Ningeweza kumpigia hata hivyo niliamua kumtumia ujumbe mfupi wa simu: Mimi:Mambo Freddy, za asubuhi! Haikuchukua muda mrefu nikapata majibu yake. Moyo uliniruka kwa furaha. Nilikuwa kama mtoto wa sekondari aliyepata ujumbe toka kwa rafiki yake wa kiume. Niliacha mambo mengine nikaenda kukaa sebuleni. Tukaanza kuandikiana jumbe fupi fupi – angalau kwa mawazo yangu. Yeye: Hi Clementina! how are you? Mimi: I’m fine, thank you. How about you? Yeye: I’m better now. Mambo vipi darling? Kusoma hilo neno “darling” kwenye simu yangu nilijisikia furaha. Nilijisikia nahitajiwa na ninapendwa. Mimi: Pouwa tu, nasikia raha yaani umechukua muda kuwa na mimi. Yeye: Mambo mengine nafikiri njama zinafanyika mbinguni! Mimi mwenyewe nimefurahi wewe kunitafuta na kunipata. Milele nitashukuru. Huyu kijana alikuwa ni mjuzi wa maneno; alikuwa anajua kuyapanga na yakaa vizuri kama Ukuta Mkuu wa China. Niliona raha moyoni. Tukaendelea kubadilishana sms kwa muda kidogo. Yeye: Nimebakia kujiuliza ulikuwa wapi muda wote wa maisha yangu Clementina? Mimi: mhh.... sijui nilikuwa wapi..au labda tuseme..wewe ndio ulikuwa umejificha wapi siku zote? Nilijicheka kidogo. Niliendelea kumuandikia. Muda huo niliweza kusikia sauti ya magari yakipita si mbali sana na nyumbani na watumishi walikuwa wakifanya shughuli zao na mtumishi wetu wa ndani alikuwa akifanya shughuli za usafi. Niliona hapo sebuleni hapafai nikaamua kupanda gorofani chumbani ili niwe katika faragha yangu, maana kijoto kilianza kunipanda taratibu. Mimi: sijui hata nikuambie nini mpenzi Freddy, nadhani tukubali kuwa kila kitu kina muda wake..na muda ndio umewadia Yeye:: Lazima nikiri Clementina kuwa japo kule kunigonga niliona ni mojawapo ya mikosi mikubwa kunikuta maishani na niliilaani siku ile lakini sasa naamini yawezekana ile ilikuwa ni mpango tu wa Jah kukuleta wewe maishani mwangu, Namshukuru Jah Rastafari! Nilitamani kucheka kwa sababu huyo Jah miye ndiye nilikuwa namsikia kwake. Na kama kweli huyo Jah ndiye anafanya mambo kama haya basi na mimi niko tayari kumuunga mkono! M: Usinikumbushe tena siku ile dear, ilikuwa moja ya siku ngumu sana kwangu....sijui hata niliingiwa na nini hadi nikakukosea heshima kiasi kile.....please usikumbushie tena tafadhali. Y: Kwangu ni siku ya kukumbuka milele siwezi kuisahau kwani ni kama chungu-tamu, na nakuomba usiisahau kwani tutakaa tucheke kila tukiikumbuka. Nakusihi usijisikie tena vibaya kwani ulichodhania ni kibaya yawezekana kimerudi kuwa chema! M: Huenda uko sahihi..lakini.......anyway basi ibakie utakavyo japo najisikia mkosaji sana Y: Kwanini tena na wakati umeshaniomba msamaha na nimekubali na daima sitashikilia siku ile dhidi yako. Nataka ufurahi kuwa nami, Tina. Nilifurahia alivyoniita “Tina”. M: Ok dear.... asante sana kwa kunisamehe... Y: Unafanya nini Ijumaa hii au Daktari ndio kakubana? M: Ijumaa..... sijapanga chochote bado... si unajua toka siku ile..nimekuwa kama nimechanganyikiwa vile na kama nisingefanikiwa kukuona ingekuwa vipi. Labda ingekuwa ni kama deni ambalo anayetakiwa kulipwa haonekani. Y: Niambie ingekuwaje darling? M: Sitaki hata kufikiria maana huenda ningefanya kitu ambacho kingeshangaza walimwengu! Y: Like what dear? I'm interested to know now. M: Mhhh..you may not like what I would have done hahaha huenda ningetafuta watu wakusake wakuteke nyara... hahaha. Love can make you go crazy unamkumbuka yule kijana aliyem shoot rais au sijui ni pope kisa alikuwa anampenda Brooke Shields miaka ya nyuma kidogo? Y: Duh.. ndio ile ilikuwa tradegy! Lakini kwa kweli ungefanya hivyo sijui ingekuwaje lakini nitafurahi milele kwani uliamua kunitafuta. Hivi uliponikosa pale ulijisikiaje? lol M: nilijiskia kuishiwa nguvu lakini moyo ukaniambia dont give up; nikapata nguvu mpya. Muda ukapita kidogo bila kupokea majibu yake. Nikawa na wasiwasi nini kimemkuta au nimesema kitu gani kibaya. Nikaanza kuingiwa na wasiwasi. Nikamtumia ujumbe mwingine. M: Mbona umekuwa kimya ghafla Freddy, umekumbuka nini? Y: Hapana nilitingwa kidogo hapa usiwe na wasiwasi. Unajua nakumbuka kama kwenye movie ulivyotokea pale hotelini jana, nikilinganisha na ulivyonigonga utadhani ni tofauti ya mbingu na nchi! M: Hahahah...kwanini unasema hivyo? Y: Ni kama nimewaona watu wawili tofauti! - sura yako ya hasira na ghadhabu na sura yako ya ucheshi na upendo ni kama sura za watu wawili tofauti kabisa. Sijui uliamkia upande gani ile Jumatatu? LOL M: Kweli mtu kabla hujafahamiana naye kwa karibu usimhukumu hata mimi siku ile nilikuona tofauti kabisa. Sidhani nilivyokuona ningetegemea hata siku moja kuwa tungeweza kuwa tumekaa pamoja na kufanya yale tuliyoyafanya jana. Nilijisikia aibu kufikiria maana katika maisha yangu yote sijawahi kufanya kitu cha kuthubutu kama kile. Yaani kumuacha mtu anichezee kwenye mazingira kama hayo na tena nikafurahia hata sielewi kama ni jinni mahaba ndio limenishika au ndio mwanzo wa mtu mzima kurukwa na akili. Y: Teh teh teh niambie ulinionaje aada ya kunibamiza hadi nikasikia kizunguzungu mwenzio? M: Nilikuona kama mmoja wa wahuni wa mjini. Si unajua tena .... ila kuna kitu kilinigusa...wakati nakufokea... ulivyokaa kimya na kunitazama machoni..macho yako yalinifanya nisikie kuchomeka moyoni kiana..nikaona upande wako mwingine Freddy, mtu mwenye utu...sikustahili kukushushia maneno yale hata kidogo. Na niliporudi nyumbani ile pica ikazidi kujirudia ikaniingia akilini, mawazoni hadi nikajikuta nakuwazia zaidi ya nilivyopaswa.kweli nilisikia aibu lakini.....basi! Y: hahahahaha M: Usicheke Freddy! Y: Pole nacheka kwa sababu umesema uliniwaza usivyopasa!; uliwaza nini? Kwa sekunde chache nilitaka kumsimulia jioni ile ya kujipa raha. Nilitaka kumuelezea kila fikra chafu na kila mguso wa mahaba niliojipa mwenyewe. Natamani ningemwambia kumuelezea kwa kina. M: mhhhh! we acha tu maana.. kweli hata siku moja NEVER SAY NEVER! litakapokupata la kukupata ndipo utajishangaa kama ninavyojishangaa mimi sasa.. kwa mara ya kwanza katika maisha yangu... nilitafakari maana ya utu... Y: Kusema kweli nilichokiona machoni mwako siku ile ilikuwa ni uchungu. Nilikuwa na uhakika mmoja kuwa nilikuwa naadhibiwa kwa makosa ya mwingine, sijui huko ulikokuwa unatoka kuna mtu alikutibua au nini lakini macho yalijaa uchungu kweli! M: Utu siyo kitu wala vitu kama ulijua....lakini labda tuyaache hayo tuongee yetu mimi na wewe.. Y: Hamna neno siku moja labda utaniambia kwani natamani nikufariji na kukufanya ujisikie kupendwa na kuthaminiwa mpenzi. M: Asante Freddy, kumbe uko mwelewa kiasi hiki pia?! Nitakupenda zaidi kwa hili...maisha yanachekesha sana..hivi..duniani kuna furaha ya kweli? wewe unafikiria je? Sijui hata kwanini nilimuuliza juu ya jambo hilo. Mawazo yangu yalikuwa yanazama sana katika maisha ya mbeleni lakini wakati huo huo nilikuwa nimejikuta nimenaswa katika mtego ambao umeniletea furaha katika namna na jinsi ambayo kamwe sikuitarajia. Kumbuka ni mke wa waziri mimi! Y: Naamini furaha ipo hasa ukiruhusu uipate kwani maisha yana vizuizi vingi sana vya kuzuia watu kupata furaha! M: Kwa mfano vitu gani hivyo vyenye kuzuia furaha? Y: Vitu kama maumivu ya moyo, machungu ya maisha, na mambo ambayo watu wengine hufanya dhidi yetu huharibu uwezekano wa mtu kupata furaha. Na hii ndio sababu wakati mwingine ni kupata vitu kinyume cha matukio hayo kutafungua furaha tena maishani. M: Kweli kabisa. Maumivu ya moyo usiseme wala usiombee.... yanamtafuna mtu polepole na kuwa kama mchwa anavyotafuna gogo... unashangaa siku moja gogo kubwa la mti linadondoka...na kuacha watu wakishangaa. Lakini si ndio maisha Freddy:? kuna mabonde, milima, mito,miteremko nakadhalika Y: Ni kweli lakini katika maisha hatutafuti mabonde na milima tunatakiwa kutafuta na kukwepa hayo na hatutakiwi kuyalazimisha. Na ni vizuri kuhakikisha hatuwi hivyo kwa watu wengine. I promise my dear sitakuwa mlima na na mabonde kwako! M: Hahaha Freddy, hebu acha utani... unajua una utani sana wewe huwezi kutabiri...unajua mwanzo wa kila uhusiano kuna ahadi nyingi sana. Umenikumbusha kitu.. Y: Nimekukumbusha nini Darling? M: Hahahahahhah... Y: Mbona unanicheka tena? M: Sikucheki wewe mpenzi...najicheka mwenyewe lakini hebu tuyaache hayo... nataka tuongee yetu. Y: Haya we, niko wako wangu. Una siri nyingi wewe! Unajipamba kwa ajili ya kesho? M: Mhhhh.... kujipamba... hiyo muhimu. Si unajua tena mwanamke kujipamba ni wajibu. Y: Unanitamanisha kwa hilo wazo tu. Ulinitamanisha sana jana na sasa nataka kuchonga mzinga kabisa. M: Ni nini kilikutamanisha zaidi.... hebu niambie ukweli mpenzi Y: Kwanza una macho mazuri sana, sauti yako ndio kabisa, na una namna ya kunifanya niwe kama kipepeo kwenye mshumaa wa moto, naungua na kuteketea mbele zako. M: Hahahahah wewe bwana!! Una maneno wewe! Tena mazito.... hebu niambie ukweli wako..Who is Freddy?sidhani huyu Freddy nimeshamfahamu... there is something that u r not telling me, u sound kama mshairi, mtunzi n.k Y: Unataka kujua nini hasa? M: Hebu nipe historia fupi ya maisha yako.... kuna mystery fulani about you. Y: Utajua mengi ukiwa umelala pembeni yangu kesho usiku; nitajibu maswali yako yote. Naomba nibakie hivyo hivyo "mysterious". Hata mimi nahisi kuna siri nyuma yako na natamani uniambie kila kitu. M: Hahaha...you are impossible! lakini kama unavyosema..tutapata muda wa kufahamiana zaidi. Y: Siyo kufahamiana tu, kujuana kabisa! In the biblical sense! LOL M: hahaha ati kujuana! we mchokozi kwelikweli! I won’t mind unijue! Y: Ndiyo kujuana kabisa, nataka nijue kila nchi ya mwili wako, kila chembe ya ngozi yako, kila mguno, kila sauti, kila utamu na kila kitu thats you! M: oh my! unanimaliza kwa maneno yako mpenzi. Unanigusa kwa nmna ya pekee. Sikumbuki ni lini liwahi kujisikia hivi tena baada ya miaka mingi sana. Y: natumaini utakuwa ni mwanzo tu wa safari ndefu ya furaha ya mapenzi kati yangu na wewe. And I’m looking forward! M: Nahitaji furaha hiyo..nahitaji kujisikia napendwa... nahitaji nami kupenda, kumpenda mtu atakayeitikia pendo na mapenzi yangu.....mwenye kuthamini penzi... mwenye kunielewa...mwenye kunigusa hisia zangu zilizoanza kufifia Freddie. Unanielewa lakini? Y: Nakuelewa kila kitu Tina, najisikia pungufu mbele zako nataka ni kupe mapenzi yangu yote. Sijui kama nastahili. Najiuliza katika mawazo yangu ninastahili vipi moyo wako? Nastahili vipi hata kukugusa. Ni kama mtumwa kukaribishwa chumbani kwa malkia, nitawezaje kuvuka kizingiti cha mlango? Nilipoyasoma maneno hayo nilijisikia uchungu. Yalinigusa moyoni na kunifanya nijisikie mnyonge. Sikutaka kijana huyo ajisikie duni mbele zangu. Maneno yake yalikuwa kama misumari ya moto. Nilitamani angekuwa karibu nimhakikishie kuwa upendo haujali hayo mengine yote. M: Jamani Freddy! usinitie unyonge, kwanini unasema hivyo? Y: Ningekuwa katika sehemu nyingine nisingeshangaa lakini hii bahati hii kwanini naistahili mimi? Clementina unaweza kuwa na mtu yeyote unayemtaka au anayekutaka na nina uhakika wapo wengi ambao wangeweza kabisa kuwa na wewe, kwanini mtu kama mimi? Hii unajua kina dada wangapi huwawanapita pale kibandani wakiona rasta zangu tu wanaona ni "mvuta bangi"? na hata hawanitazami tena? M: Kwani hata ingekuwa malkia..milango si inaingilika tu? umesahau kule Uingereza miaka ya 90? Unajua maisha yako complicated. Kuna so many people who are so lonely hutajua mpaka usikie hadithi zao hao wanaokupita kila siku pale kibandani huenda wana matatizo yao mengi mno kiasi kwamba.... hitaji la kumpenda mtu ni kitu cha mwisho kukifikiria au hitaji la kupendwa siyo kipaumbele. Unanipata lakini? Y: Nakupata, unajua sijawahi kufikiria hilo. Mara nyingi nafikiria wanaringa na wana nyodo, au ndio mbwembwe zenyewe au ndiyo yanaitwa mapozi! Kumbe huwezi kuwahukumu watu kwa kuwaangalia tu. M: Usihukumu kabisa! Mimi nimeshajifunza hili somo siku nyingi! Zamani nilikuwa na vipimo vyangu vya kupima watu na mambo wayafanyayo siku hizi nimeacha kabisa kwa sababu kila kitu kinachofanywa na binadamu kina maelezo tena pengine mazito yenye kuingia akilini sana. Huwezi kuhukumu mtu na matendo yake kwa kutumia kipimo standard kwa watu wote. Y: Jamani Clementina umejaa hekima kama ulivyojaa uzuri! M: Mbona hata mimi nakuona una hekima sana..ndio maana pale mwanzo nikakuuliza huyu Freddy ni nani ? maisha yana mengi ndani yake...ndio maana wenzetu husema " live your life to the fullest" Y: Kwa kweli with you now.. I intend to. Nilikuwa nimekata tamaa sana na maisha. M: ni kwa sababu watu tunaishi sehemu ndogo sana ya maisha yanavyotakiwa yawe kwa sababu mbalimbali. Unanishawishi kuendeleza swali langu kwako.... who is this Freddy jamani? Nilituma ujumbe huo kabla sijasoma ujumbe wake wa awali. Nilipouona ulinigusa na kunishtua kidogo. M: Ulitaka kukata tamaa kwanini? Y: Kwa sababu sikuamini mtu anaweza kuingia katika maisha yako na kupindua kabisa fikra zote ulizokuwa nazo kuhusu mapenzi. M: oh... tell me more, please. M. Hata mimi tena zaidi. Nashukuru kunipa kampani. Y: Tina, naweza kukuomba kukuuliza jambo moja very private? Moyo ulinidunda tena, sijui anataka kuniuliza nini. Ulipita muda na muda ulikuwa umeanza kukaribia kwenye saa tano hivi ili nianze msafara wa kwenda Saloon. Nilishangaa mbona amechelewa kunijibu. M: Freddy, umekaa kimya.... nimekukumbusha kitu kibaya? haya tuache topic hii... Y: Jamani, hapana mtoto alikuwa ananisumbua hapa kidogo. Tutazungumza sana huko mbeleni Tina usiwe na shaka. M: Mtoto? una mtoto? Y: Ndiyo wa miaka 6 aliachwa na mama yake.Nilikuambia jana umeshasahau? M: Sikumbuki..si unajua jana. Jana ilikuwa siku tofauti sana. LOL Y: Kweli nilikuchanganya wangu. Sasa ya kesho kweli ndio utakumbuka?LOL M: Jamani..unaninyanyasa sasa! leo nimeshatulia..nitakumbuka Y: Hahaha sawasawa. Basi nikuache na miye nijiandae hapa na shughuli fulani fulani, nakusubiri kwa hamu sana kesho. Ukipata muda usiku nipigie nina hamu ya kusikia sauti yako kabla sijaenda kulala maana jana ulinipa ndoto tamu sana! M: sawa mpenzi, na miye naelekea Saloon! Kuna sherehe kubwa kesho. Y: Oh yeah, wapi tena? M: Si kwako! Y: Safi kabisa, tuna mengi ya kuongea basi. Nimefurahi sana kuchat na wewe darling M: Uliza tu usiwe na shaka. Y: Naomba ukija uje ukiwa umenyoa nywele zote za mwili ubakie na hizo za kichwani tu M: Mmmh.. yaani zote? Y: Ndiyo zote, if you don’t mind. Si unajua mambo ya Brazilian? M: Ndiyo. Nilijihisi kutetemeka. Sikuelewa alikuwa anafikiria vitu gani au ameniuliza hivyo kwa sababu gani. Lakini aliuliza kwa namna nzuri kiasi kwamba vyovyote alivyokuwa anafikiria nilikuwa niko tayari. Y: Basi hilo tu nakuomba, hutajutia. M. Done. Tuliagana kwa maneno mengine na mimi nikajiandaa kutoka pale nyumbani na kuanza kuelekea Saloon ya Bantu maeneo ya Morocco/Kawawa karibu na Pub ya PR. Moyoni nilikuwa na wazo moja tu nalo lilikuwa Jumamosi. Nilipanga nitakaporudi nyumbani kutoka Saloon nijifungie bafuni nijinyoe kila kitu. Nilijicheka nilipowasha gari kwa mawazo hayo. Lakini nilipania lolote litakalokuwa, lazima nishiriki kikamilifu katika sherehe za Muungano. Siku ilikuwa inaenda pole pole mno nilijiambia nikiishika barabara ya Morogoro. Ningekuwa na uwezo ningeiruka Ijumaa niwe Jumamosi! Nikakumbuka msemo wa wahenga. Mvumilivu hula mbivu. Au huliwa! ***